Magufuli ana ubavu wa kuvunja Bunge kama anavyodai?

mpk

JF-Expert Member
Sep 26, 2012
3,115
3,863
Gazeti linaloheshimika nchini na linatoka kila wiki limeandika taarifa za kuwepo mpango wa wabunge wa CCM kutofautiana na Rais kwa sababu ya wenzao kutiwa msukosuko na TAKUKURU na wengine kufikishwa mahakamani. Mi pia ni shuhuda kwamba mpango huo upo na unaratibiwa na mawaziri wawili vijana toka serikalini mwake.

Na ni kweli wanataka kutumia upinzani lakini si wale wabunge wanaotajwatajwa. Mawaziri hao wamechukizwa sana na wanachosema Rais "hashauriki" na amekuwa akifanya maamzi magumu tena hadharani pasipo kushirikisha baraza lake la mawaziri. Ndipo mkakati ukasukwa kwa kuwatumia wabunge ambao wamechukizwa na kitendo cha Rais kuingilia maslahi yao.

Lakini bwana mkubwa aliunasa mtandao huo na akaamua kumpigia Ndugai na kumwambia kama wakiendeleza mkakati wao atavunja bunge ili aone wangapi watarudi (hii ni kwa mujibu wa gazeti hilo).

Inasemekana pia alimuonya Ndugai kutotetea wabunge wanaohojiwa na vyombo mbali mbali akisema "hiyo ni mijizi achana nayo" anakaririwa.

Swali langu ni je Magufuli ana ubavu wa kulivunja bunge turudi kwenye uchaguzi?
 
Anao uwezo,maana hata bajeti isipopita Rais anatakiwa kuvunja Bunge na kuitisha uchaguzi,ila swali ni je ana moyo huo sio uwezo huo
Nia anaweza kuwa nayo na kikatiba anaruhusiwa, mi nimeuliza ana ubavu huo?
 
Kwanza tu hiyo kauli kuwa aone ni wangapi watarudi inanipa mashaka kama hao jamaa walishinda bila mizengwe.......CCM hakuna wa kumtisha mwenzake, kila itu anajua udhaifu wa jirani yake.......kazi kweli kweli.
 
wabunge hao, wajipime! ikiwa bunge litavunjwa leo nani atarudi tena bungeni, yupi anakubalika zaidi,kati yao na Rais Magufuri
 
Back
Top Bottom