Magufuli ampiku Lowasa urais 2015

Magufuli ampiku Lowasa urais 2015

Hana jeuri hiyo.Amedanganywa na Odinga, mbinu za Kenya hazifai hapa.
Labda Mamvi aamue kutokugombea. Mpaka sasa Mamvi ndio Prezidaa 2015.

MIE NAMUOMBEA MAMVI aka E LOWASA ASIMAMISHWE ILI ITUWIE URAISI KUICHUKUA NCHI KUPITIA KWA JEMEDARI WETU CHADEMA, DR W SLAA, EH MOLA TNAMTAKA FISADI PIA GAMBA LOWASA MABADILIKO YAWEZE KUTIMIA
 
Magufuli mchapa kazi mahiri sana. Hata akiamua kugombea anafaa. Lowassa naye ni mzuri sana pia. Ni mchapa kazi na mfatiliaji. Ana mtazamo wa kimaendeleo. Kwa maoni yangu hawa watu wasisimame/wasigombee wote. Asimame mmoja, halafu mwingine awe waziri mkuu. Hapo nchi itaendelea. Nawapenda na kuwakubali wote kwa utendaji kazi wao.
 
Sidhani kama taarifa hizi ni nzuri kwa CDM.. MAGUFULI hana mpinzani nchini hapa.
Hofu yangu ni MAFISADI nguli wa CCM kama watampitisha kwa kuhofia mwisho wao...
I PRAY FOR HIM..
 
Kwa haya uliyoandika sio bure, ni lazima tu utakuwa na matatizo ya akili!

Mkuu, Binafsi mimi nilikuwa mfuasi mkubwa sana wa Mamvi kuhusu U-Presidar mwaka 2015 lakini nimebaini hawezi kupambana na Dk.Slaa kwa spidi waliyonayo CHADEMA hivi sasa ingawa anakubalika ndani ya chama,lakini naomba nikupe siri moja inayoendelea chini kwa chini hivi sasa katika ukanda wa Ziwa,kuna taarifa nilizipta kutoka kwa baadhi ya vigogo ambao wako kanda ya ziwa kwa upande wa CCM kwamba wameanza mchakato wa kuhakikisha rais wa mwaka 2015 anatokea kanda hiyo.

Na mtu pekee ambaye wamemuona anafaa kwa nafasi hiyo na anaweza kuuzika kwa wnanchi ama kusimama na CHADEMA ni JPM, mchakato umeanza tayari na mapro wa eneo hilo wanadaiwa kwamba tayari wamelifikisha suala hilo kwa JK na kumweleza ambapo taarifa zinaeleza kwamba pamoja na kwamba yeye binafsi alikuwa hampendi JPM tangu alipoingia IKULU,amekubaliana na mapro hao na ameanza kumtengenezea njia.

Madai haya hayajathibitishwa lakini yamezagaa sana kwa maeneo ya Kanda ya Ziwa,kwa hiyo naweza kukubaliana na wale ambao wanatabiri kwamba JPM atagombea urais 2015,na akitia tu mguu anaweza kuibuka kidedea.
 
Hata akipitishwa Magufuli lazma ubunge CDM tushinde hvyo serikali itakua ya mseto
 
kwakifupi ccm kila m2 ananuka rushwa hadi wajumbe wa nyumba kumi.hakuna na wala sijaona m2 msafi alafu akawa bado yupo ccm huyu atakuwa mnafiki 2.
 
suala la usalama wa barabara ni la magufuli akiwa kama waziri ujenzi kwa hiyo ni wajibu wa serikali kuweka ulinzi juu yake na siyo kwamba anafaa kuwa Rais, no
 
Mbwembwe za kinafiki.Magamba hata wafanye nini walishaharibu tangu zamani.Hafai hata tone kuwa rais wa nchi hii.
Msafara wa magufuli waacha gumzo
Wajameni ndo kusema watu wa kanda ya ziwa wanamthamini mtu huyu kwa nafasi ya juu kabisa (Urais) hata kabla ya uchaguzi 2015 ?

Story nzima hapa chini, kazi twende!


MSAFARA wa Waziri wa Ujenzi, John Mgaufuli umeacha maswali jijini Mwanza baada ya kuwa na magari 26,viongozi mbalimbali wa mkoa na kusindikizwa na kuongozwa na pikipiki inayoongoza msafara wa viongozi wa kitaifa akiwa Rais.

Magufuli ambaye alikuwa katika ziara ya kikazi mkoani Mwanza kwa ajili ya kuangalia barabara ya kutoka uwanja wa Ndege kwenda Igombe ambayo inapaswa kufungwa kupisha ujenzi wa upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mwanza, mbali na kusindikizwa na gari la kamanda wa polisi wa mkoa, pia kila alipopita kulikuwa na askari wa usalama barabarani ambao walikuwa wakizuia magari kuruhusu msafara wake kupita.

Msafara huo ulianzia ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Mwanza na kuelekea Igogo saa 3:14 asubuhi kwa ajili ya kukagua ujenzi wa barabara zilizojengwa kwa mawe, kwanza ulitanguliwa na pikipiki ya Jeshi la Polisi iliyokuwa ikisafisha njia na kufuatiwa na gari la Kamanda wa Polisi ambalo lilikuwa limewasha taa na kufuatiwa na gari la Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na nyuma yake gari la Waziri Magufuli na kisha magari mengine ambayo idadi yake ilikuwa zaidi ya 26.

Mbali na kutanguliwa na magari, pikipiki hiyo ya king’ora pia katika makutano ya Barabara ya Nyerere na Bungando walikuwa wameandaliwa askari wa usalama barabarani kuzuia magari ili msafara huo kupita pamoja na njia nyingine zinazoingia katika barabara hiyo.

Source : Mwananchi, 12 January 2013​
 
JPM ankubalika kuliko unavyosema toa kauli y ilmradi ushabiki nambie nani kama yeye hata hao ambao wanatumia nguvu kubwa kujitangaza kisiasa toka vyma vyoote vikubwa?
 
Aaaaaaaaaaaaaah wapi,thiitih am ni yale maneno y wapita nji hhahahah
 
CCM ikimteua Magufuli kuwa mgombea wao itakuwa imejihakilishia kuendelea kuongoza atleast 2015-2020


Kimsingi uchaguzi utabakia tu kwenye nafasi za Ubunge na Udiwani tu,kwani Rais atakuwa tayari anajulikana kama ilivyokuwa kwenye uchaguzi wa 2005.
 
Mambo bado CCM vita vya urais subiri mapigo EL si mtu wa mchezo
 
Magufuri hana lolote, kashfa ya kuuza nyumba za serikali itamuandama popote.
Magufuri kumfananisha na Lowasa ni sawa na kulinganisha ardhi na mbingu,kimsingi LOWASA ni jembe,ni kiongozi safi Maufuli hamfikii hata kwa chembe
 
its better to have hiv positive in your blood more than to have chadema ideas in your brain
 
hata akipitishwa magufuri lazma ubunge cdm 2shnde hvyo serikali itakua ya mseto

kwa namna yeyote serikali ijayo lazima itakua ya mseto.na rais ajae atoke ccm au cdm hawezi akawa na mamlaka kama marais waliopita,atakua rais dizaini ya mwai kibaki.
 
Back
Top Bottom