Magufuli ampiku Lowasa urais 2015

Magufuli ampiku Lowasa urais 2015

Dubidu

Member
Joined
Dec 12, 2012
Posts
22
Reaction score
5
Msafara wa Magufuli waacha gumzo
Wajameni ndo kusema watu wa kanda ya ziwa wanamthamini mtu huyu kwa nafasi ya juu kabisa (Urais) hata kabla ya uchaguzi 2015?
Story nzima hapa chini, kazi twende!
MSAFARA wa Waziri wa Ujenzi, John Mgaufuli umeacha maswali jijini Mwanza baada ya kuwa na magari 26, viongozi mbalimbali wa mkoa na kusindikizwa na kuongozwa na pikipiki inayoongoza msafara wa viongozi wa kitaifa akiwa Rais.​
Magufuli ambaye alikuwa katika ziara ya kikazi mkoani Mwanza kwa ajili ya kuangalia barabara ya kutoka uwanja wa Ndege kwenda Igombe ambayo inapaswa kufungwa kupisha ujenzi wa upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mwanza, mbali na kusindikizwa na gari la kamanda wa polisi wa mkoa, pia kila alipopita kulikuwa na askari wa usalama barabarani ambao walikuwa wakizuia magari kuruhusu msafara wake kupita.​
Msafara huo ulianzia ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Mwanza na kuelekea Igogo saa 3:14 asubuhi kwa ajili ya kukagua ujenzi wa barabara zilizojengwa kwa mawe, kwanza ulitanguliwa na pikipiki ya Jeshi la Polisi iliyokuwa ikisafisha njia na kufuatiwa na gari la Kamanda wa Polisi ambalo lilikuwa limewasha taa na kufuatiwa na gari la Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na nyuma yake gari la Waziri Magufuli na kisha magari mengine ambayo idadi yake ilikuwa zaidi ya 26.​
Mbali na kutanguliwa na magari, pikipiki hiyo ya kingora pia katika makutano ya Barabara ya Nyerere na Bungando walikuwa wameandaliwa askari wa usalama barabarani kuzuia magari ili msafara huo kupita pamoja na njia nyingine zinazoingia katika barabara hiyo.​
Source: Mwananchi, 12 January 2013​
 
Kwani kushangiliwa ndo kukubalika? Mwenziye ana mtandao mpana...
 
Mie tangu Magufuli asimamie uuzaji wa kijambazi wa nyumba za umma kwa wabunge na mawaziri wa CCM sina hamu naye. Kwa ufupi hakuna mtu wa maana kwenye CCM. Wote ni wachafu mafisadi na mafisi so to speak.
 
Hana jeuri hiyo. Amedanganywa na Odinga, mbinu za Kenya hazifai hapa.
Labda Mamvi aamue kutokugombea. Mpaka sasa Mamvi ndio Prezidaa 2015.
 
Hana jeuri hiyo.Amedanganywa na Odinga, mbinu za Kenya hazifai hapa.
Labda Mamvi aamue kutokugombea. Mpaka sasa Mamvi ndio Prezidaa 2015.

Kwa CCM hakuna uchaguzi wa haki ................. wanajifanyia mambo yao kutokana na upepo wanavyouona wenyewe. Ndiyo maana JK akampiku Salim kama vile amekaa. Kama mtandao ungekuwa unafanya kazi basi Malecela angekuwa Rais 1995. Ingawa hapo mtasema ni KJN ndiye alizuia. Waulize Wanzenji .............. CCM huwa inawafanya nini vipenzi wao ... wakifika Dodoma?? Huoni Babu yao kakazana na Urais wa ZNZ mapaka kaishia magogoni kwa deputy!! Chezea CCM wewe!!
 
Niliwahi kuona hivyo hapa Dar ila kunakuwa na mojawapo wa maofisa wakubwa wa balozi hapa nchini/nje ambao kwa hadhi yao wanapewa escort ya pikipiki.
 
Mkuu habari ndiyo hiyo. JPM anapiga jalamba. Huyu ni compromising candidate na ana kete ya kukubalika kwa wananchi walio wengi.

Ki ukweli hata mimi namkubali lakini tatizo wanaomkubali siyo wenye maamuzi
ya kumpitisha kugombea kwenye chama chake, kumbuka hana mtandao ndani
ya chama na siasa za Tanzania ni za fitna, labda utaratibu ubadilike...
 
Naogopa wasije wakampa sumu mara ya pili maana mpinzani wake can't stand anything on his way..
 
Magufuri hana lolote, kashfa ya kuuza nyumba za Serikali itamuandama popote.
 
Hivi suala la Magufuli kuwa na msafara wa magari mengi unatusaidia nini watanzania ambao hajala, hajui pa kulala, amekosa ada ya watoto maana shule zimefunguliwa, jamani tuangalie na mambo ya msingi ya kujadili na sio msafara wa kiongozi fulani, tunapotezeana muda tu hapa.
 
Msafara wa magufuli waacha gumzo
Wajameni ndo kusema watu wa kanda ya ziwa wanamthamini mtu huyu kwa nafasi ya juu kabisa (Urais) hata kabla ya uchaguzi 2015 ?​
Story nzima hapa chini, kazi twende!​
MSAFARA wa Waziri wa Ujenzi, John Mgaufuli umeacha maswali jijini Mwanza baada ya kuwa na magari 26,viongozi mbalimbali wa mkoa na kusindikizwa na kuongozwa na pikipiki inayoongoza msafara wa viongozi wa kitaifa akiwa Rais.​
Magufuli ambaye alikuwa katika ziara ya kikazi mkoani Mwanza kwa ajili ya kuangalia barabara ya kutoka uwanja wa Ndege kwenda Igombe ambayo inapaswa kufungwa kupisha ujenzi wa upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mwanza, mbali na kusindikizwa na gari la kamanda wa polisi wa mkoa, pia kila alipopita kulikuwa na askari wa usalama barabarani ambao walikuwa wakizuia magari kuruhusu msafara wake kupita.​
Msafara huo ulianzia ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Mwanza na kuelekea Igogo saa 3:14 asubuhi kwa ajili ya kukagua ujenzi wa barabara zilizojengwa kwa mawe, kwanza ulitanguliwa na pikipiki ya Jeshi la Polisi iliyokuwa ikisafisha njia na kufuatiwa na gari la Kamanda wa Polisi ambalo lilikuwa limewasha taa na kufuatiwa na gari la Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na nyuma yake gari la Waziri Magufuli na kisha magari mengine ambayo idadi yake ilikuwa zaidi ya 26.​
Mbali na kutanguliwa na magari, pikipiki hiyo ya kingora pia katika makutano ya Barabara ya Nyerere na Bungando walikuwa wameandaliwa askari wa usalama barabarani kuzuia magari ili msafara huo kupita pamoja na njia nyingine zinazoingia katika barabara hiyo.​
Source : Mwananchi, 12 January 2013​
Wote ni magamba ila gamba moja limefanana na gamba la kobe, ukiliondoa kobe anakufa.
 
Hamna jamani, jamaa kiutendaji nampa 85% yuko vizuri nao polisi wameonesha hisia zao kwa rais ajaye si vibaya kwa wana CCM wameshtuka.
 
Back
Top Bottom