Nyenyere
JF-Expert Member
- Sep 9, 2010
- 14,842
- 10,765
Wakuu, niko Rachel bar Moshibar .- Ukonga. Pembeni yangu kuna watu watano wanapata bia. Katika hali ya kustaajabisha namsikia jamaa mmoja akilaani kitendo cha mh. rais kufuta sherehe za uhuru. Anaelezea jinsi gani rais anavyojijengea chuki na watumishi wa umma. Jamaa anahitimisha kwa kutolea mfano yeye akiwa daktari kwenye sherehe za uhuru hutoka na shilingi laki tatu. Anajiapiza kuwa Magufuli atarogwa kwa sababu hii ya kuwanyima ulaji.
Baada ya kuyasikia haya nasema moyoni mwangu, bado safari ni ndefu sana kufikia mageuzi ya kweli. Juzi nilimsikia mama mmoja akilalamika kuwa mwalimu mkuu (shule hakutaja ) alimwambia wazi wazi kwamba kitendo cha kuondoa michango na tuition mashuleni hakikubaliki. Kwamba walimu hawajafurahi hata kidogo, kisha akamwahidi mama huyo kuwa baada ya miezi sita mtakuja kutupigia magoti mkiomba tuition.
Hivi watanzania tumekuwaje hasa!? Unataka nini? Mbona inavyoonekana "wasomi" ndio wanageuka kikwazo kwa mabadiliko chanya? Kundi la wasomi limegeuka kuwa wapigania maslahi binafsi. Tutafika kweli!!?
Mungu mtie nguvu rais wetu, tuko pamoja naye. Amina