Magufuli ameonyesha nchi inaendeshwa na Mamlaka na si wenye fedha kama ilivyozoeleka

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
Huko nyuma nchi yetu iliendeshwa na fedha (wenye fedha). Sasa ameingia Rais anayetaka NCHI IENDESHWE NA MAMLAKA. Wenye fedha wameona wakatingisha kiberiti kupitia sukari. Sio mbali watanyooka. Na wameshaanza kunyooka, sukari imeshaanza kushuka leo wengi tumenunua sukari kwa sh. 2000 tu kwa kilo.

Uganda iliwahi kutokea. Wenye mabasi wakagoma. Ndani ya mwezi Museven akatelemsha mabasi mia tatu. yalipoanza kutoa huduma nao wakayarudisha. Yanaendelea mpaka sasa. Hao wenye mabasi hawathubutu tena kugoma. Na hao wa sukari watanyoosha mikono si mbali.

Asante Rais Magufuli kwa kuwanyoosha na endelea kuwanyoosha usirudi nyuma, watanzania tupo pamoja nawe.
 
Ni wehu ndo wanaweza kushindana na serikali. Wao waliona wanaweza kumbe dunia hii kila kitu ni fursa, hawa wafanyabiashara uchwara wa Tz wakizingua mbona nchi jirani wanalitamani sana soko letu lenye takribani 50m?

Ni suala la kuwabonyeza tu leteni mitaji yenu mutengeneze pesa alafu uje uone wanavyoingia kama mshare unaelekea porini.

Biashara ya leo ni fursa tu, mitaji inatembea na kuzungushwa, wao wakijifanya kujitoa kwenye biashara wajiandae kupotea kabisa, watalia wao.

Leo angalia baada ya makampuni ya saruji kuongezeka jamaa wanaanza kulia na bei, hakuna namna, ulizoea kuhodhi soko sasa washindani wameingia, ni lazima upunguze bei la sivyo utajifuta mwenyewe.

Huo ndo uchumi harisi na ndo ushindani, na ndo faida kwetu sisi watumiaji. Hutaki unachapa laba, unajiweka kando ili wanaoweza wachangamkie fursa
 
awamu hii lb7 wanatakiwa kufanya mambo 3
1.kusifu
2.kuabudu
3.kushangilia
chunguza tu nyuzi zao utakuta wameangukia kwenye moja kati ya hayo
 
Hakika Ngosha anawakomesha ile Mbaya. Anajua jinsi ya kucheza hili gemu
Ha ha ha ha we mdada huwa nakulingamisha na audio CD inayobadilika kulingana na takwa la msikilizaji.....

Ulisifia ya kule Leo unayaponda kwa ya huku!!!
 
Huko nyuma nchi yetu iliendeshwa na fedha (wenye fedha). Sasa ameingia Rais anayetaka NCHI IENDESHWE NA MAMLAKA. Wenye fedha wameona wakatingisha kiberiti kupitia sukari. Sio mbali watanyooka. Na wameshaanza kunyooka, sukari imeshaanza kushuka leo wengi tumenunua sukari kwa sh. 2000 tu kwa kilo.

Uganda iliwahi kutokea. Wenye mabasi wakagoma. Ndani ya mwezi Museven akatelemsha mabasi mia tatu. yalipoanza kutoa huduma nao wakayarudisha. Yanaendelea mpaka sasa. Hao wenye mabasi hawathubutu tena kugoma. Na hao wa sukari watanyoosha mikono si mbali.

Asante Rais Magufuli kwa kuwanyoosha na endelea kuwanyoosha usirudi nyuma, watanzania tupo pamoja nawe.

Serikali kushika udalali na kuagiza tanni maelfu Sukari toka nje tayari imetingishika hizo pesa zingeagiza madawa na vitendanishi, zingejenga barabara au watu wangepewa mikopo badala ya kutumika kununulia SUKARI.

Sasa tumeanza kusikia Tetesi za Mafuta ya kupikia, serikali pia itaanza kuagiza ikitoka ikitoka hiyo pia umeanza kusikia habari za,mafuta Dizel na Petrol kuanza kupanda nayo yataadimika.

Mwisho wa siku wanapogombana mafahali wawili ziumiazo ni nyasi. Mwananchi ndio anataabika kwa vitu hivi kiadimika na kupanda.

Kumbuka Serikali wakati inaagiza hizi ni dharula na pesa haipo kwenye bajeti Mwisho wa,siku huduma za Jamii zitadorola Sana na wananchi wataamua wenyewe baada ya Miaka 5.
 
Mkuu kabla ya kuandika fikiria kidogo.
 
Nadhani unakosa weledi (Professionalism) katika mambo ya Biashara na Uchumi. Unapokuwa na Watu maskini wasio na mitaji ujue hautafika popote katika kuwaletea watu wako maendeleo.

Serikali ikiwa na fedha pekee yake haiwezi kufanya lolote kama katika soko la ndani hakuna bidhaa muhimu kwa maisha ya watu.

Na pale serikali inapojichukulia maamuzi ya kufanya biashara kwa kuagiza bidhaa na kuwauzia wananchi, basi inakuwa inafanya kosa la kiufundi, kwani wananchi wote watakaa na kusubiri Serikali yao iwafanyie. Hapo ajira na Mapato kwa wananchi yanapungua.

Vichocheo vya kukua kwa uchumi hutegemea sana wananchi wenyewe kufanya biashara. Serikali inayoua mitaji ya wananchi wake kwa kutaifisha, ni serikali mfu isiyokuwa na maono thabiti ya kuboresha maisha ya watu wake.

Kuna kanuni ya "Multiplier & Acceleration" katika uchumi na biashara ambapo, kadri wananchi wenyewe (na sio serikali) wanavyobadilishana fedha na bidhaa, kunakuza ajira na ongezeko la thamani, ambayo ndio huzaa faida na kodi ya ongezeko la thamani (VAT) na Kodi ya Mapato (Income Tax). Faida (Profit) kwa Mwananchi na kodi kwa Serikali haziwezi kuwepo endapo Serikali yenyewe itaamua kufanya bisahara na kuwakatisha tamaa wananchi wajasiriamali, kwa au kutaifisha Mali zao au serikali kushindana nao kufanya biashara.

Maamuzi ya kukurupuka kuwazuia wafanya biashara kuagiza sukari toka nje, ili hali uzalishaji wa ndani ukiwa duni, yalisababisha uhaba wa sukari usio wa lazima, ambapo leo serikali hiyo hiyo imeamua yenyewe kuagiza tena sukari, badala ya kuwaachia wananchi kisha yenyewe (Serikali) ikajikita kusimamia Ubora, kukusanya kodi na kuimalisha ulinzi kwa raia na Mali zao.

Serikali nzima ya awamu ya Tano, itulize mzuka, iache kukurupuka, itulie na ifanya maamuzi kwa hekima, busara na weledi.
Tena Kiongozi yeyote wa umma anapotoa hotuba na matamko kwa umma, basi afanye hivyo kwa sauti tulivu yenye uelekeo wa kuleta suluhisho na matumaini kwa wananchi. Ubabe na Majigambo si jambo jema kwa kiongozi wa umma. Na hao unaowagombeza kama watoto jua kwamba wana ndugu jamaa na marafiki. Kumbuka cheo ni dhamana na kuna maisha nje na baada ya Ofisi.
 
Huko nyuma nchi yetu iliendeshwa na fedha (wenye fedha). Sasa ameingia Rais anayetaka NCHI IENDESHWE NA MAMLAKA. Wenye fedha wameona wakatingisha kiberiti kupitia sukari. Sio mbali watanyooka. Na wameshaanza kunyooka, sukari imeshaanza kushuka leo wengi tumenunua sukari kwa sh. 2000 tu kwa kilo.

Uganda iliwahi kutokea. Wenye mabasi wakagoma. Ndani ya mwezi Museven akatelemsha mabasi mia tatu. yalipoanza kutoa huduma nao wakayarudisha. Yanaendelea mpaka sasa. Hao wenye mabasi hawathubutu tena kugoma. Na hao wa sukari watanyoosha mikono si mbali.

Asante Rais Magufuli kwa kuwanyoosha na endelea kuwanyoosha usirudi nyuma, watanzania tupo pamoja nawe.
Kumbe Serikali zilizopita zilikuwa zinaongozwa na wenye fedha duuuh afadhali umetufungua macho jinsi Serikali hii ya ccm inavyoendesha nchi
 
Eti nchi inaendeshwa kwa mamlaka! Mamlaka gani ya kuwaogopa akina lugumi, wezi wa escrow, wakwapuzi wa UDA na PRIDE, walionunua boti bovu la shilingi bilioni 8? Acha kutufanya Watanzania wapumbavu kwa kuja kuandika pumba zisizo na kichwa wala miguu. Hakuna mamlaka yoyote zaidi ya udikteta wa kutaka kulidhibiti Bunge kwa kila hali na sera za kukurupuka ambazo ndiyo chanzo pekee cha ukosefu wa sukari nchini. Uongo wako peleka Lumumba siyo hapa.

Huko nyuma nchi yetu iliendeshwa na fedha (wenye fedha). Sasa ameingia Rais anayetaka NCHI IENDESHWE NA MAMLAKA. Wenye fedha wameona wakatingisha kiberiti kupitia sukari. Sio mbali watanyooka. Na wameshaanza kunyooka, sukari imeshaanza kushuka leo wengi tumenunua sukari kwa sh. 2000 tu kwa kilo.

Uganda iliwahi kutokea. Wenye mabasi wakagoma. Ndani ya mwezi Museven akatelemsha mabasi mia tatu. yalipoanza kutoa huduma nao wakayarudisha. Yanaendelea mpaka sasa. Hao wenye mabasi hawathubutu tena kugoma. Na hao wa sukari watanyoosha mikono si mbali.

Asante Rais Magufuli kwa kuwanyoosha na endelea kuwanyoosha usirudi nyuma, watanzania tupo pamoja nawe.
 
Serikali kushika udalali na kuagiza tanni maelfu Sukari toka nje tayari imetingishika hizo pesa zingeagiza madawa na vitendanishi, zingejenga barabara au watu wangepewa mikopo badala ya kutumika kununulia SUKARI.

Sasa tumeanza kusikia Tetesi za Mafuta ya kupikia, serikali pia itaanza kuagiza ikitoka ikitoka hiyo pia umeanza kusikia habari za,mafuta Dizel na Petrol kuanza kupanda nayo yataadimika.

Mwisho wa siku wanapogombana mafahali wawili ziumiazo ni nyasi. Mwananchi ndio anataabika kwa vitu hivi kiadimika na kupanda.

Kumbuka Serikali wakati inaagiza hizi ni dharula na pesa haipo kwenye bajeti Mwisho wa,siku huduma za Jamii zitadorola Sana na wananchi wataamua wenyewe baada ya Miaka 5.
Kwani hivyo vitu vikija serikali inagawa bure?
 
Safi saaana. na kuna wanasiasa uchwara wakataka tumia hii loophole. Of course kwenye mabadiliko kuna shida zinaweza kutokea lakini zinavumilika sasa kukosa sukari wiki kadhaa ndio iwe issue?!?!?! Magufulo Go tuko pamoja na wewe!
 
Serikali kushika udalali na kuagiza tanni maelfu Sukari toka nje tayari imetingishika hizo pesa zingeagiza madawa na vitendanishi, zingejenga barabara au watu wangepewa mikopo badala ya kutumika kununulia SUKARI.

Sasa tumeanza kusikia Tetesi za Mafuta ya kupikia, serikali pia itaanza kuagiza ikitoka ikitoka hiyo pia umeanza kusikia habari za,mafuta Dizel na Petrol kuanza kupanda nayo yataadimika.

Mwisho wa siku wanapogombana mafahali wawili ziumiazo ni nyasi. Mwananchi ndio anataabika kwa vitu hivi kiadimika na kupanda.

Kumbuka Serikali wakati inaagiza hizi ni dharula na pesa haipo kwenye bajeti Mwisho wa,siku huduma za Jamii zitadorola Sana na wananchi wataamua wenyewe baada ya Miaka 5.
"Mpiga ngumi ukutani huumiza mkonowe" WATANYOOKA TU.. MH Rais Magufuli wananchi tuko nyuma yako na tunazidi kukuombea. Endelea kurudisha nidhamu na heshima ya Watanzania na nchi yao. Wao ni wachache nasi ni wengi.
 
Serikali kushika udalali na kuagiza tanni maelfu Sukari toka nje tayari imetingishika hizo pesa zingeagiza madawa na vitendanishi, zingejenga barabara au watu wangepewa mikopo badala ya kutumika kununulia SUKARI.

Sasa tumeanza kusikia Tetesi za Mafuta ya kupikia, serikali pia itaanza kuagiza ikitoka ikitoka hiyo pia umeanza kusikia habari za,mafuta Dizel na Petrol kuanza kupanda nayo yataadimika.

Mwisho wa siku wanapogombana mafahali wawili ziumiazo ni nyasi. Mwananchi ndio anataabika kwa vitu hivi kiadimika na kupanda.

Kumbuka Serikali wakati inaagiza hizi ni dharula na pesa haipo kwenye bajeti Mwisho wa,siku huduma za Jamii zitadorola Sana na wananchi wataamua wenyewe baada ya Miaka 5.
wacha tutaabike lakini mwisho wasiku dola ndio inaongoza taifa sio walioweka serikali mfukoni
 
Back
Top Bottom