Olumolongez
JF-Expert Member
- Dec 19, 2015
- 818
- 299
Acha JPM afagie na kupanga nyumba yake kwanza ili siku ataanza kwenda huko nje baada ya kufagia na kupanga nyumba yake vizuri ili akaongeze huo ujuzi mwingine ili akirudi aboreshe zaidi. Ni kukosa busara kuanza kwenda kutembelea tembelea majirani wakati nyumba yako ni chafu. Sipingani na wewe.Katika sifa kadhaa za mgombea urais kwa tiketi ya ccm huwa ipo ya awe na uzoefu wa masuala ya kimataifa.
sifa hii kwa JPM ilifumbiwa macho,
Nyerere baada ya kusoma nchini alikwenda makerere Uganda na baadae uingereza kunoa Bongo mwinyi alishawahi kukaa Misri ubalozini kwa miaka kadhaa,Mkapa ndio usiseme canada na marekani amekaa sana,JK ziara zake nje ya nchi akiwa foreign affairs minister kwa miaka kumi na miaka kumi ya urais wake ni sawa na kukaa nje miaka mitano,(siungi mkono,it was too much)
JPM alikanyaga Dar es salaam kwa mara ya kwanza mwaka 1984 alipokuwa anakuja kujaza fomu ya kujiunga na UDSM,tangu hapo hajawahi kukaa nje ya nchi kwa zaidi ya mwezi mmoja Amezunguka vichochoro vyote vya Tanzania alipokuwa waziri wa ujenzi akikagua barabara,kazi aliyoiweza kuliko mawaziri wote tangu uhuru .
Back to the point,mimi nimezaliwa Dar Es Salaam na enzi za ujana wangu nilikuwa najiona mtoto wa mjini sana ila siku nilipokanyaga Manhattan mwaka 2002 nilijiona ni mshamba sana kila kitu nilikiona ni kipya na tangu siku hiyo nikajua Dar Es Salaam sio jiji bali ni mji tu.
Wazungu wanakitu wanaita exposure , huwa ni shule tosha kwa tuliosoma zamani tunajua ,mtu wa mtwara kuchaguliwa sekondari wilaya ya Ngara japo kwa upande mmoja ilichangiwa na uhaba wa shule ila ilitusaidia sana,kwa sasa kuna wanafunzi wanazaliwa ndani ya wilaya x,primary mpaka sekondari anasomea ndani ya wilaya hiyohiyo na chuo cha ualimu hapo hapo na anakuja kufundisha shule ndani ya wilaya hiyohiyo ,huyu anakosa exposure atakuwa mshamba tu.
Pia kwa waliopitia vyuo vikuu vya Tanzania mtagundua kuwa lecturers walipata elimu yao nchini bila kwenda nje ya nchi huwa wanakamata sana wanafunzi wakati wa mitihani kuliko walimu waliosomea nje.(sina uhakika kama kutumbua majipu yanhusiana na kukosa exposure )
JPM anasema anataka Tanzania iwe nchi ya viwanda sasa nashangaa itakuwaje nchi ya viwanda wakati anawakimbia wazungu ambao ndio wenye technology ya viwanda,kama hadi pampas za watoto tunaagiza tukubali hatuwezi kujenga viwanda bila kuwa karibu na wazungu,awakaribishe wakae mezani waongee dili win win based business,wanatuhitaji pia bado tunawahitaji,ndio maana Nyerere na kuwatimua kote waingereza alifia kwao akukubali kufia Muhimbili
Pia JPM amekaliliwa akisema Dar ndio kioo cha Tanzania ndio maana anataka kujenga daraja toka cocobeach mpaka ocean road,hii ni kukosa exposure,nchi za watu maendeleo huwa yanakuwa balanced na pia fursa zinakuwa balanced kila sehemu kupunguza msongamano wa watu kwenye miji fulani,kuna baadhi ya nchi watu hawataki kuishi miji mikuu kwani fursa ziko kila kona,Juzi tumesikia kuwa Obama atakuwa rais wa pili wa marekani kuishi washngtone baada ya kustaafu na hii ni kwa sababu watoto wake bado wapo shule,other wise angerudi kwao chicago,JK wakati anakabidhi ikulu na kutuaga kuwa anarudi kijijini helicopter ilimpeleka Msoga mchana jioni akarudi nayo Dar.
Tanzania sio Dar tu
Pia exposure inasaidia kuimprove lugha za kigeni,hili sitaki kuliongelea sana hapa nisije kuchafua jukwaa
aende akaibe au akanunue technologyKwahyo aende US, China kufanyaje labda zaidi ya kutembeza bakuli. Bila kujijenga ki ndani na kuimarisha mambo ya ndani ka elimu, miundo mbinu hata ahamie China nothing will change sasa nyie waumini wakuwa dependence ndo mnataka awe mzururaji mbona mlikuwa MNA mnanga mkwere
mkapa na JK walitumia vibaya exposure yao wakawa vibaraka wa wazungu wakachemsha JPM awekinyume nao awakomalie wazungu wasitunyonye kila mtu afaidikeSikatai ila hao tangia wawekeze wameacha technology gani kama huko migodini je niwa Tanzania wangapi wanaruhisiwa kupata hyo knowledge wanayoitumia ka sikuajiri experts kutoka nchini kwao na Watanzania kuwa vibarua tu. Nenda huko gesi ilipovumbuliwa ka kuna Mtanzania ana ruhusiwa kijua kinachoendelea. China, Singapore, Taiwani, south Korea tulikua almost the same ila nao wametuacha mbali. Wale walirndeleza internal capability, innovation na Ku ji invest kwenye elimu na kupata experts. Ili kuendelea lazima tuendeleze wazawa kwa kuwazesha. Na tutumie foreign experts kubenefit nchi sio makampuni yao
Ni hilo pia na lingine ni kutuambia kuwa amefika ManhattanNa hilo la mwisho unalo dai hutaki kuliongelea sana ndio hasa target yako umezunguka weee!.
Yeye ataibàje bila kuwa na vision ya kitaifa ya kimaendeleo na Ku invest kwenye technical change na implementations ya issue zetu. Bila hivo kamwe tusipovifuata hatutapiga hatua hata akia nje ya nchi. Aanzie ndaniaende akaibe au akanunue technology
Wanasema fumbo mfumbe mjinga mwerevu hung'amua.ahahahaha nisipo huko jamani
Jk yeye alikua ka ndege angani na kula bataz had kubembeamkapa na JK walitumia vibaya exposure yao wakawa vibaraka wa wazungu wakachemsha JPM awekinyume nao awakomalie wazungu wasitunyonye kila mtu afaidike
Jk yeye alikua ka ndege angani na kula bataz had kubembea kah magufuli akomae na huku ndanimkapa na JK walitumia vibaya exposure yao wakawa vibaraka wa wazungu wakachemsha JPM awekinyume nao awakomalie wazungu wasitunyonye kila mtu afaidike
Hivi hao wenye exposure na wanaojuana na akina Obama wamelisaidia nini Taifa hili?Magufuli Diplomasia ya nje anajuana na Raila Odinga tu..!!
mtoa mada hajaongelea kuhusu masuala ya lugha bali technology ya wenzetu kuwa ipo juu kuliko afrikaWw ulioandika mm cjakuelawa unamaanisha nini kama lugha ya kingereza cc sio waingereza wananchi tunataka vitendo na uchapakazi ndio maana tuliokua na viongozi wabovu kwa kuangalia kingereza anagalia wabunge wameishia kidacho cha nne tazama wanavyotoa mada zilizomakini wakati hao walisoma masomo ya juu na mavyeti kibao wanafanya utumbo kila cku.mtu hajatoa mada wala kijibu hoja mpaka kikao kinakwisha na kingereza kama amezaliwa nacho acha hizo kingereza nikama lugha nyingine.cc tunataka kiongozi atakaeweza kuingoza vile tunavyotaka wananchi hasa wakipato cha chini nafikiri tumempata maraisi watatu wamepita lkn hawawezi kumfikia Magufuli ni mtu aliyejitolea muanga juu ya nchi yake.Mungu mpe maisha marefu.
Rais wetu anajua matatizo yetu. Yaani kutatua matatizo ya ndani ya nyumba yako mpaka uende kwa jirani? Mathalan ndani hakuna chumvi wala sukari na chanzo cha ukosefu huo unakijua kuwa mkeo anachepusha matumizi ya lazima na kupeleka kwenye upatu. Hapo bado unahitaji msaada wa jirani?
Mbona JK alipofululiza safari za nje ulimuunga mkonoRais wetu anajua matatizo yetu. Yaani kutatua matatizo ya ndani ya nyumba yako mpaka uende kwa jirani? Mathalan ndani hakuna chumvi wala sukari na chanzo cha ukosefu huo unakijua kuwa mkeo anachepusha matumizi ya lazima na kupeleka kwenye upatu. Hapo bado unahitaji msaada wa jirani?
Sefue tupo huku kwa jf?Subiri feedback yako muda sio mrefu!
Vijijini ndiko kuna wawekezaji?amalize exposure ya vijijini tanzania ndiyo atoke nje..