Magufuli alikuwa muongo sana

Enzi hizo alikuwa akijisifia kwenye hotuba zake eti uchumi unakua kwa 7.3% kila mwaka! Na wakati hali ilikuwa ni tete kweli kweli, kiasi cha kufikia hatua ya kuzinguana na IMF!

Kwenye kampeni alikuja na milioni 50 kila Kijiji!!

Alitudanganya bei ya sukari eti aliikuta ikiwa tsh elfu 5 na hivyo akafanikiwa kuishusha mpaka tsh 3000!

Na ilikuwa ukimpinga tu, kesho unashangaa uko Mahakama ya Kisutu kwa kosha la uhujumu uchumi, utakatishaji fedha na kuendesha genge la uhalifu! Kesi haina dhamana, unaishia jela!

Alifurahi huyo alipoambiwa eti Tanzania imepanda na kuwa nchi ya uchumi wa kati! Dah! Miccm ilitulingishia kipindi hicho!! We acha tu!!
Lakini ni IMF hao hao walithibitisha Tanzania kuingia uchumi wakati kutokana na ukuaji wa uchumi, ilikadiliwa Tz ingeingia uchumi wa Kati mwaka 2025, ikawahi miaka 5 kabla.
 
Ni lini mishahara ililipwa tarehe 15 au 20 ya mwezi unaofuata?

Mimi sikumbuki aisee kwenye utawala wa Kikwete sikumbuki nasisitiza kama kuna mtu anakumbuka aniambie.

View attachment 1831163
Kwa miaka ya nyuma kidogo,mishahara ilikuwa inachelewa kweli. Japo si kwa kiwango hicho. Alipoingia Mkapa,mambo yakabadilika,yeye alisema mishahara itoke kabla ya tarehe 25 ya kila mwezi. Kikwete akajitahidi ila kuna wakati ilikuwa inaenda mpaka tarehe 29 hadi 30 na kwa baadhi ya Halmashauri mpaka tarehe 5.

Alipoingia Magu,sisi tulikuwa tunapata kila tarehe 20,waalimu 21 au 22,na mara chache sana iliwahi kufika tarehe 25 au 26.

Ila sasa,ni UDUNYA kushangilia mshahara kuingia sijui tarehe 15 au ngapi.
Ni kushikiwa akili tu.
Mtu akikulipa mshahara tarehe 10,mpaka tarehe 10 tena ni mwezi mmoja(siku 30).
Akikulipa tarehe 20,mpaka tarehe 20 bado ni mwezi tu.

Huu ujinga wa wanasiasa kutuona wajinga kwakujidai kutuwahishia mishahara ilhali tunaupata kila mwisho wa mwezi ni UPUMBAVU,na kwa bahati mbaya unashangiliwa na watumishi wa umma.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
33 Reactions
Reply
Back
Top Bottom