Magufuli acha vitisho, sisi ni watu wazima

Magufuli acha vitisho, sisi ni watu wazima

Shark

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2010
Posts
29,973
Reaction score
30,154
MAGUFULI ACHA VITISHO, TUMEBALEHE KIAKILI

Ni zaidi ya mara tatu mgombea wa CCM anasikika kwenye mikutano akiwataka watu wasifanye mabadiliko kwani yanaweza kutokea mambo kama ya Libya, hii ni dhahiri ya kwamba CCM hawana pakutokea maana wameona kuhubiri ubaguzi kumefeli, kuwatumia viongozi wa upinzani kumefeli na sasa wanawatisha wapiga kura kwa hoja za kitoto, hili nalo linafeli. CCM na Magufuli mnapaswa kujua yafuatayo:-
1. Libya Ghadafi aliingia kwa mtutu wa bunduki na ametolewa kwa mtutu wa bunduki, sisi kwetu tunapiga kura tena kwa amani.

2. Huu sio uchaguzi wa kwanza kufanyika Tanzania na tumekuwa tukipata viongozi kwa amani, mwaka huu kipi cha ajabu?

3. Hatuwezi kufikia walipo libya sababu ya undugu uliopo miongoni mwetu licha ya tofauti za vyama hata ndani ya familia.

4. Ni ujinga kuhubiri kwamba ukipewa ridhaa utafanya mabadiliko ndani ya chama na serikali halafu wakati huo huo unawatisha wananchi wasifanye mabadiliko.

Uhai unapotaka kutoka lazima kutapatapa, mabadiliko mwaka huu ni lazima.

Kwa hisani ya DAMAS DAMIAN,
Korogwe
 
Last edited by a moderator:
CCM kwa sasa wanataka kuwafanya watanzania malofa kila kitu...tumeamka aisee...hatudanganyiki...liwalo na liwe sisi ni mabadiliko tu.
 
Kwa hatua tuliyofikia ktk nchi yetu tunatakiw kutoshabikia vyama kwa kila jambo. Nionavyo mm niwakati wa kumuweka kiongoz msafi ili kurudsha iman kwa wananchi.
 
ni mwaka wa mabadiliko ccm wao walie tu,habari za mjini ni lowassa mabadiliko ,mabadiliko lowassa
 
Kwa hatua tuliyofikia ktk nchi yetu tunatakiw kutoshabikia vyama kwa kila jambo. Nionavyo mm niwakati wa kumuweka kiongoz msafi ili kurudsha iman kwa wananchi.

Ila mambo ya kutufananisha na Libya yamepitwa na wakati. TV na Radio ziko kila mahali, na zilionyesha na kutangaza yaliyotokea Libya. Kamwe hayawezi kua sawa na yaliyoko hapa kwetu Tanzania.
 
Hii hotuba inukuliwe ili mambo yakiharibika tuwajibishane
 
Kwa katiba ya sasa ambapo rais ni kila kitu, lowasa hafai kuwa rais, atachukuaba ardhi yote huku akijifanya mwekezaji. Asubiri tukipata katiba mpya tutamchagua.
 
Kwa katiba ya sasa ambapo rais ni kila kitu, lowasa hafai kuwa rais, atachukuaba ardhi yote huku akijifanya mwekezaji. Asubiri tukipata katiba mpya tutamchagua.

Mchagueni Lowasa hatakuwa mzigo kwa serikali amesema atapunguza mshahara wa rais (mshahara wake) kutoka sh. 400,000,000/- hadi sh.2,000,000/- hanaga ubinafsi ndio maana hutoa misaada kwa wahitaji.
 
Magufuli anajua kuwa anamsaidia Lowassa ili aje kukumbukwa kwenye baraza la mawaziri.
 
Back
Top Bottom