Magufuli acha vitisho, sisi ni watu wazima

Magufuli acha vitisho, sisi ni watu wazima

Kwa hatua tuliyofikia ktk nchi yetu tunatakiw kutoshabikia vyama kwa kila jambo. Nionavyo mm niwakati wa kumuweka kiongoz msafi ili kurudsha iman kwa wananchi.


uweke kiongozi msafi toka chama kichafu?
by the way ni usafi UPI unaoungelea...maana kama kashfa na ufisadi tunazisikia wote wakisemwa kuwa nazo....unataka kumaanisha nini?
ni wakati watanzania tukafanya mabadiliko.....makubwa ya kuondoa chama hiki kilichooza kabisa...sio kuchafuka tu.
 
Kwa hatua tuliyofikia ktk nchi yetu tunatakiw kutoshabikia vyama kwa kila jambo. Nionavyo mm niwakati wa kumuweka kiongoz msafi ili kurudsha iman kwa wananchi.
Imami irudi wapi? Huyo mnayetuambia ni msafi anawatisha Watu na vita. Kama CCM ikishindwa na kuachia Madaraka vita itatoka wapi? Mambo hayo yatatokea tu endapo CCM itashindwa Kisha igome kushuka chini.
 
huo mtaji wao wa kura milioni sita lazima tugawane mwaka huu
 
Lakin kwanin wamejaa hofuu,mpaka meingne anadai chaguo lake likipita atalala kwa amani WHYYY KUNA UTATA HAPO
 
MAGUFULI ACHA VITISHO, TUMEBALEHE KIAKILI

Ni zaidi ya mara tatu mgombea wa CCM anasikika kwenye mikutano akiwataka watu wasifanye mabadiliko kwani yanaweza kutokea mambo kama ya Libya, hii ni dhahiri ya kwamba CCM hawana pakutokea maana wameona kuhubiri ubaguzi kumefeli, kuwatumia viongozi wa upinzani kumefeli na sasa wanawatisha wapiga kura kwa hoja za kitoto, hili nalo linafeli. CCM na Magufuli mnapaswa kujua yafuatayo:-
1. Libya Ghadafi aliingia kwa mtutu wa bunduki na ametolewa kwa mtutu wa bunduki, sisi kwetu tunapiga kura tena kwa amani.

2. Huu sio uchaguzi wa kwanza kufanyika Tanzania na tumekuwa tukipata viongozi kwa amani, mwaka huu kipi cha ajabu?

3. Hatuwezi kufikia walipo libya sababu ya undugu uliopo miongoni mwetu licha ya tofauti za vyama hata ndani ya familia.

4. Ni ujinga kuhubiri kwamba ukipewa ridhaa utafanya mabadiliko ndani ya chama na serikali halafu wakati huo huo unawatisha wananchi wasifanye mabadiliko.

Uhai unapotaka kutoka lazima kutapatapa, mabadiliko mwaka huu ni lazima.

Kwa hisani ya DAMAS DAMIAN,
Korogwe

Hats Mimi nimeliona hilo. Hizi naweza kusema ni kampeni za kimpumbavu na kilofa kabisa.
 
Last edited by a moderator:
Hats Mimi nimeliona hilo. Hizi naweza kusema ni kampeni za kimpumbavu na kilofa kabisa.
Ni Sera za walioishiwa hoja. Pengine wananchi tunaonekana wajinga kua tunaamini kila kitu hatuchambui taarifa.
 
Back
Top Bottom