Magufuli aagiza wanafunzi wasafiri bure

Magufuli aagiza wanafunzi wasafiri bure

Huwenda wakazi wa Kigamboni nao wakapata hiyo nafuu au inaweza tafsirika kuna Double Standard kwa watanzania ambao katiba yao inasema wote ni sawa.Kwa Mh.Magufuli tendo hili linaweza kumkosesha kura za wale wanaotumia vivuko vya serikali huku wanalipia kama kigamboni,pangani nk..nk.Kama wanafunzi ni tegemezi,siyo wa huko Mtwara tu,hata wa Dar ni tegemezi.Ama kwa hakika Mwenyezimungu akita lake jambo hakuna wa kulipinga,hebu ona mtu anavyogawa watu ambao anategemea watampigia kura.
 
Kigamboni wanamsubiri kwa hamu Mheshimiwa, masharti ni lazima apige mbizi kama kweli anazitaka kura zao.
 
Ameanza kutoa Ahadi za Rushwa kama la daraja la mbutu Igunga wakati Wa uchaguzi siyo !!!
 
ktk sheria za uchaguz hii ni rushwa!
 
Unaweza dhani ana huruma sana kumbe ni mbinu ya kisiasa tu. Kama kweli anajali kiasi hiki, mbona wale wengine aliwaambia wapige mbizi? Kweli siasa!!!

Hana JIpya huyu mtendaji! HUku alikosema wapige mbizi wanafunzi hupanga foleni wakivuka kwenda mjini kwenye magari yao ya shule! Hufika shuleni wamechelewa sana huku wale waheshimiwa wakipita njia ambayo haihitaji kusubiri! Huyu jamaa amesababisha wazazi wa watoto waliokuwa wanavuka toka Kigamboni kuja mjini kuwahamishia Kigamboni sababu ya mipangilio yake kuwa mibovu! HAFAI KWA LOLOTE HUYU MAGUFURI!
 
Huwenda wakazi wa Kigamboni nao wakapata hiyo nafuu au inaweza tafsirika kuna Double Standard kwa watanzania ambao katiba yao inasema wote ni sawa.Kwa Mh.Magufuli tendo hili linaweza kumkosesha kura za wale wanaotumia vivuko vya serikali huku wanalipia kama kigamboni,pangani nk..nk.Kama wanafunzi ni tegemezi,siyo wa huko Mtwara tu,hata wa Dar ni tegemezi.Ama kwa hakika Mwenyezimungu akita lake jambo hakuna wa kulipinga,hebu ona mtu anavyogawa watu ambao anategemea watampigia kura.

Anapagawa huyu jamaa sasa hivi ndio anajitia huruma kwa watanzania! Akiwa waziri alikuwa na kauli za kikatili sana! Anabomoa nyumba na anasema hatulipi! Alipofika kigamboni akasema wapige mbizi anasahau kuwa kuna wanafunzi ambao husoma mjini na wanahitaji special care kwa maana ya magari yao yawe yanapitishwa barabara isiyo na msongamano! Mpaka leo tunavyo andika hapa watoto husota kwenye foleni na hufika shule wamechelewa na kurudi nyumbani nako hufika wamechelewa! Watoto wengi kulingana na kadhia hii na kupandishiwa gharama za magari yao wameshindwa kumudu gharama hizo na wengi wameamua kuahama shule na kusoma shule za kigamboni! Huyu MAGUFURI SIYO KABISA! Anafaa kuwa mtendaji na siyo mtawala au kiongozi!
 
hakuwambia kama hawana nauli wapige mbizi?
 
Hv mtwara wao hawajui kupiga mbizi au msimu huu kauli inabidi tuzichunge?
 
Washauri wa Mh Magufuli wanamwingiza mjini. Kwa mujibu wa sheria ahadi hii ni rushwa unless anarejea kitu kilichokuwepo kama sera au kinatekelezwa huko nyuma. Yawezekana hashauriwi au hashauriki!
 
angalau nimepata nafasi ya kukomenti kwa mgombea wa CCM maana natauzi habari yake sioni humu
 
Hawa wa Mtwara wana bahati, wenyewe hawajaambiwa wakishindwa kulipa nauli wapige mbizi??
 
C.C.M ni mamaster mind wa siasa za bongo..wao hudeal zaidi na uhalisia kuliko maneno
 
Unaweza kukuta hao walemavu hata 100 hawafiki.
 
Baada ya uchaguzi wanafunzi watasafiri bure hata kwenye ndege
 
Sawa tuwalipia kwenye PAYE hamna shida ila tukutane October
 
kivuko kimegharimu milioni tatu na laki tatu (3300000 ) /= tu!!!!!!! tafadhali acha masiala,au umekosea kutaipu. Uwenda ulitakakusema bilioni 3.3.

Nilijua Mimi Pekeangu Ndio Sijaelewa Milioni Tatu!! Alafu Watu Hawana Kivuko Toka Uhuru!! Ebu Mtoa Mada Tueleweshe Vizuri Kama Umekosea Kuiandika Au Ndio Hiyohiyo
 
Back
Top Bottom