Magreth sitta, mkuchika, kapuya, chegeni wapeta

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Monday, 01 October 2012 07:50

Waandishi wetu, Dar na mikoani

NDOTO za Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye za kuwania Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu ujao, zimeingia doa baada ya kushindwa katika uchaguzi wa Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) kupitia Wilaya ya Hanang, Mkoa wa Manyara.

Sumaye ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Jimbo hilo la Hanang kwa kipindi kirefu hadi mwaka 2005, ameshindwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji na Uwekezaji), Dk Mary Nagu ambaye amegeuka kuwa mmoja wa hasimu wake wa kisiasa katika siku za karibuni, mbali ya kuwa na mahusiano mazuri kwa miaka mingi.

Taarifa za Sumaye kushindwa zilianza kuvuja mapema hata kabla ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi huo saa 10:00 alfajiri jana, kwani baadhi ya wapambe wake walilazimika kuondoka katika ukumbi uliokuwa ukifanyika uchaguzi huo.
Msimamizi wa uchaguzi huo ulianza kufanyika juzi asuhubi, Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Erasto Mbwilo akitangaza matokeo hayo alisema Sumaye alipata kura 481 huku Dk Nagu akiibuka mshindi kwa kupata kura 648.

Mgombea mwingine, aliyekuwa anawania nafasi hiyo, Leonce Marmo Bura alitangaza kujitoa mapema ili apate fursa ya kugombea nafasi ya Ujumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa ambao alishinda.


Dk Nagu tangu awali alionekana kuungwa mkono na wajumbe wengi wa mkutano huo hali ambayo ilimfanya wakati wa kujieleza asiulizwe maswali huku mwenzake Sumaye akibanwa kwa maswali mengi.


Hata hivyo, uhodari za Sumaye, kujibu maswali hayo kwa kiasi fulani ulionekana kutaka kubadili hali ya upepo katika mkutano huo, lakini wakati wa kupiga kura nguvu ya Waziri Dk Nagu ilionekana kurejea upya.


Mvutano kati ya Sumaye na Nagu ulianza kuonekana hivi karibuni baada ya kikao cha kamati ya siasa ya Wilaya kilichofanyika Septemba 2, mwaka huu kupitisha jina la Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye na Leonsi Marmo huku la Nagu likiondolewa kufuatia kudaiwa kuwa na majukumu mengi ya kikazi ikiwamo Ubunge na Uwaziri.

Hata hivyo, Nagu alikata rufaa katika Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Manyara ambayo ilirejesha jina lake.

Kushindwa kwa Sumaye kupata nafasi hiyo kunaonyesha ni kikwazo kipya kwake kama ataamua kuwania Urais kupitia chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kwa mara nyingine.


Sumaye ambaye amekuwa Waziri Mkuu katika utawala wote wa Serikali ya awamu ya tatu ya Rais Benjamin Mkapa aliwania Urais kupitia chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, akishindana na Rais Jakaya Kikwete, Waziri Mkuu Mstaafu, Dk Salim Ahmed Salim, Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela, Dk Abdallah Kigoda na Profesa Mark Mwandosya.


Hata hivyo, pamoja na kwamba hajaweka wazi kuwa atagombea tena katika uchaguzi wa mwaka 2015, lakini watu walio karibu na mwanasiasa huyo wamekuwa wakieleza kuwa anajiandaa kugombea tena nafasi hiyo.


Juzi wakati akijieleza mbele ya wajumbe wa mkutano huo, Sumaye alionekana kushangazwa na hatua ya Dk Nagu kugombea nafasi hiyo, hali akijua kuwa yeye ni Waziri na hivyo kwa utaratibu ndani ya CCM ni mjumbe moja kwa moja wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC).


Kwa upande wa Dk Nagu ambaye aliachiwa kugombea ubunge wa jimbo hilo na Sumaye mwaka 2005, katika siku za karibuni amekuwa akitamba kuwa ni Simba jike, alitumia dakika tatu za kujieleza kukanusha uvumi kuwa ametumwa na makundi mengine ndani ya CCM ili kumzuia Sumaye asiwe Mjumbe wa NEC ikiwa ni harakati za kugombea Urais mwaka 2015.


Chemba

Nec: Mbunge wa Kondoa Kusini, Juma Nkamia ameibuka kidedea kwa kuwashinda, Fredrick Duma na Said Sambala.

Mwenyekiti: Shaban Kilalo amepita amepita bila ya kupigwa.

Wajumbe wa Mkutano Mkuu Taifa: Waliochaguliwa ni Msonga Swedi, Mwanaharusi Bato, Mary Mkanya, Halifa Nyasuka na Ally Dosa.

Uyui
Nec: Mlolwa Beatus ameshinda nafasi hiyo na kumbwaga Mbunge wa Igalula, Dk Athumani Mfutakamba na Nhumbi Nhumbi.


Mwenyekiti: Aliyechaguliwa nafasi ya Mwemyekiti ni Mussa Ntimizi kwa kuwashinda, Abdallah Kazwika na Hamisi Bundala.


Urambo

Nec: Mbunge wa Viti Maalum CCM, Margreth Sitta alibuka kidedea nafasi ya ujumbe wa Nec kwa kuwashinda Weston Chokala na Hamis Malunkwi.


Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa: Waliochaguliwa ni Dk Zakaria Mganilwa, Adamu Malukwi, Emmanuel Gembe,
Anna Magoha na Blandina Lawi.


Uchumi na Fedha: aliyeshinda ni Francis Kasanga na katika Uenezi nafasi hiyo imechukuliwa na Paul Shija.

Kaliua
Uchaguzi katika Wilaya ya Kaliua umeingia dosari baada ya namba iliyotangazwa na msimamizi wa uchaguzi, kuwa ni 770, lakini baada ya kupiga kura na kuhesabiwa zilifika 919 kukiwa na ongezeko la kura 149 ambazo hazikujulikana zilikotoka.

Hatua hiyo ilisababisha vurugu kubwa iliyotulizwa na askari polisi waliokuwa na silaha za moto na kufanikiwa kukamata vijana wawili waliofikishwa kituo cha polisi.

Kufutia hali hiyo, Hamis Madili aliyegombea nafasi ya uenyekiti na Gulamsen Dewji aliyekuwa akichuana na Athuman Kapuya katika nafasi ya Nec walipinga matokeo hayo.

Mwenyekiti Wilaya: Katika nafasi ya Mwenyekiti Elias Kaseko aliibuka mshindi kwa kumshinda Hamis Madili.
Nec: KKapuya ameibuka kidedea na kuwaacha Dewji na Musa Kichari.

Kibaha
Nec: Nafasi hiyo imekwenda kwa Rugemalira Rutatina ambaye amewashinda Rashid Bagdela na Kepteni Fratern Kiwango.

Wajumbe Mkutano Mkuu Taifa: Waliochaguliwa ni Catherine Katele, Joseph Chale, Jumanne Mangala, Mohammed Mpaki na Kepteni Fratern Kiwango.

Kilosa
Mweyekiti: Nassoro Udulele ameibuka kidedea baada ya kumshinda Christopher Wegga aliyekuwa akitetea kiti chake.
Nec: Aliyeshinda nafasi hiyo ni DK Chisuligwe Kadudu kwa kuwashinda Hamadi Lila na Theophil Nangusu.

Masasi
Mwenyekiti:Kazumali Malilo ameibuka mshindi akitetea kiti chake kwa kumbwaga Andrew Kasawala.
Nec: Nafasi ya Nec imechukuliwa na Pole Pole baada ya kumbwaga mpinzani wake kada wa chama hicho, Ketty Kamba.


Newala

Mwenyekiti: Ali Sadi ameibuka mshindi.
Nec: Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), George Mkuchika ameshinda nafasi ya Nec kwa kuwabwaga Abdallah Napinda (267) na Shaibu Namkuna (261).


Tandahimba

Mwenyekiti: Abdul Namtula ameibuka mshindi baada ya kumbwaga Sophia Makonyola aliyekuwa anatetea nafasi hiyo.

Nec: Balozi Rashid Makame amechaguliwa kuchukua nafasi ya Nec baada ya kuwashinda Namyundu Salum na Lihundu Samli.

Mtwara Mjini

Mwenyekiti: Ali Mussa Chikanwene ameibuka kidedea baada ya kuwashinda nYusuf Mineng'ene, Hawa Mangasala na Bakari Mbwana.Nec: Godbless Kweka ametangazwa mshindi baada ya kuwabwaga Saidi Swalehe, Phiri Makaburi na Ernest Haule.


Mtwara Vijijini

Mwenyekiti: Ali Komba ameibuka mshindi baada ya kumshinda Ahmadi Likomba.

Nec: Salehe Livanga amechaguliwa kuwa mwakilishi wa Nec katika wilaya hiyo baada ya kuwashinda Alhaji Mpeme na Salehe Nandieti.

Nanyumbu

Mwenyekiti: Muhata Masusa amewashinda Ali Dua na Chibwana Mtimbe.
Nec: Hassan Kambutu ameibuka mshindi baada ya kuwaacha nyuma Rajabu Mrope, Linga Mpwanya na Mwema Issa.


Nyasa

Nec: Nafasi hiyo imechukuliwa na Mbunge wa Mbinga Magharibi, Kepteni John Komba baada ya kumbwaga Mwenyekiti wa Bodi ya Kahawa Tanzania, Adolph Kumburu.


Mwenyekiti: Nafasi hya Mwenyekiti imechukuliwa na Francis Homanga aliyewashinda Essau Milinga na Severin Kapecha.


Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa: Waliochaguliwa ni Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, Erenest Kahindi, Edna Hyera, Grace Haule, Adam Mhaiki na Erenest Hyera.

Mbarali
Mwenyekiti: Aliyechaguliwa kushika nafasi ya mwenyekiti ni Mathayo Mwangomo baada ya kuwashinda Ignas Pesipesi Mgao na Benedict Masuhva.


Nec: Geofrey Mwangulumbi amechaguliwa kuwa mshindi wa nafasi ya Nec baada ya kuwashinda wapinzani wake Paul Kitha na Hanji Godigodi.


Busega

Nec: Mbunge wa zamani wa Jimbo la Busega Dk Raphael Chegeni ameibuka kidedea baada ya kuwashinda Amos Onesmo na Witnes Mahela

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa: Waliochaguliwa ni Mkuu wa Wilaya ya Busega, Paul Mzindakaya, Meya wa Jiji la Mwanza, Stanslaus Mabula, John Lukale, Witnes Mahela, Josia Ngela na Hamis Haruna.


Nyamagana

Nec: Mbunge wa zamani wa Jimbo la Nyamagana, Lawrence Masha ameibuka mshindi katika nafasi hiyo kwa kuwabwaga wapinzani wake, James Bwire, Bikhu Kotecha (83) na Ngofilo Masalu.


Mwenyekiti: Mwanahabari Raphael Shilatu ameshinda nafasi ya Mwenyekiti baada ya kuwashinda wapinzani wake Mashaka Kaguna, Yahya Nyaonge na Joseph Bupamba.


Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa: Waliochaguliwa ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Baraka Konisaga, Frola Mgabe, Joseph Kahungwa, John Malogoi na Saimon Ntambi.


Tarime

Mwenyekiti: Rashidi Bogomba ametetea kiti chake baada ya kumshinda Mwita NewLand.
Nec: Christopher Gachuma ameibuka kidedea katika nafasi ya Nec katika wilaya hiyo baada ya kumshinda Mairo Marwa.

Butiama

Mwenyekiti: Yohane Mirumbe amechaguliwa kushika nafasi ya mwenyekiti katika Wilaya ya Butiama.
Nec: Marwa Siagi ameshinda nafasi ya Nec katika wilaya hiyo.


Rorya

Mwenyekiti: Samwel Kiboye.
Nec: Thobias Laya.


Rufiji

Mwenyekiti: Hakimu mstaafu wa Mahakama za Mwanzo Ramadhani Ngayunga kwa kumshinda Mrisho Matimbwa na Bakari Msati.


Nec: Uwesu Msumi ameshinda nafasi hiyo kwa kuwabwaga aliyekuwa mbunge wa zamani wa Rufiji, Bakari Mbonde na Shabani Ngarambe.


Temeke

Nec: Phares Magesa amembwaga Issa Mangungu. Mwenyekiti: Ameshinda Yahaya Sikunjema.
Wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa, Asha Mlawa, Lucy Kanyopa, Hadija Maganga, Issa Zahoro na Mpanjila.


Habari hii imeandaliwa na Mustapha Kapalata, Tabora, Mussa Juma, Hanang, Joseph Lyimo, Fadhil Rashid, kilosa, Abdallah Bakari,Mtwara, Joyce Joliga, Songea, Godfrey Kahango, Mbarali, Sheilla Sezzy, Mwanza, Amini Yasini, Rufiji, Nora Damian, Dar,
 
Back
Top Bottom