Mohammed Hamad
JF-Expert Member
- Jan 17, 2011
- 3,988
- 1,304
- Thread starter
-
- #61
Bora iweke moyoni , hiyo siri mwana flani
Siri ibaki sirini, siyo tena hadharani
Hapo utaweza wini, ewe mtunzi makini
Shairi lako halijakamilika japo nimekupa thanksShukran sana mkuu hata mie nakukubali
Umepewa utu wema,
Wenye thamani daima,
Moyo wangu wanituma,
Sifazo kukupatia.
Nimetoa changamoto, naomba nguvu tilia,
Mambo yame motomoto, na sote kujisikia
WomanOfSubstance umeuanza mpito............
Shairi lako halijakamilika japo nimekupa thanks
Wiselady m'baya, ninasema hadharani,
Hatufai kwenye kaya, amekosa shukurani
Ameikosa hidaya, si mtu mwenye ubani
Na ukuu wa wilaya, haupati asilani
Atabaki anagwaya, hata aende shambani,
Hata aende Ulaya, atakuwa kisirani
Kabila yangu Mhaya, Bukoba napatamani,
Akipenda kuwa yaya, simpeleki nyumbani,
Atakuja sota waya, atoe jasho kwapani,
Mbona wanitisha, ewe uloleta tungo
Nabaki ninalo shaka, kama nisomacho ndicho
Naweza hata kubisha, labda uje thibitisho
kukujibu kwa ushairi siwezi ila mohamed kashakujibu on behalf,,ukiendelea jela miezi 6,,,au unanisifia kwa mafumbo nini!!
We mshairi wa ukweli. Kweli kiswahili lugha yako. Ila naomba kama ulikuwa na maana ya rais wangu dr.Slaa naomba urejee ID yake vizuri,kama una member mwingne poa ,ila kwa rais wangu dr. Slaa iyo si ID yake. Mwisho nakupongeza kwa kipaji cha utunzi.
Wow yaani hata mwezi bado humu umewajua wote hawa??? Au ulikuwa unatumia jina lingine humu before???
Nice one kama mwezi bado na unashinda humu
Senksi yangu ya via mobile kama siioni vile!!Asante MS...me like you too!Ngoja na mimi nijipange kuangusha kitu!
Maandalizi muhimu wewe!Wengine tunatafuta washairi watusaidie tusije jiaibisha bure!Senks yako haifjafika labda ipo niani lol. Kumbe ndio maana viewers wengi wanaochangia wachache kumbe mnaenda kujipanga!
Maandalizi muhimu wewe!Wengine tunatafuta washairi watusaidie tusije jiaibisha bure!
M.Shossi nakupa mia, kwa tungo zako murua,
yaonekana umekamia, malenga wakongwe kuwabidua,
Kimokole natazamia, shairi lijalo kuingia,
Screen naitumbulia, mimacho kodokodo nimeitoa
Kimokole moyoni nafarijika, malenga tukikutanika,
Ya haki kuyatamka, batili kuzifunika,
Kheri ikaminika jamvini tukanufaika.
Bwana Kimokole, nakushukuru hakika
Malenga mkijuana, furaha yashika hatamu,
Tutafunika kila kona, JF wasiishe hamu,
Ingawa maisha yabana, JK kutuhujumu,
Tutakomaa kinamna, hadi haki ishike hatamu.