Maghorofa machafu yenye ukungu Kariakoo, ni umaskini au tabia?

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
37,908
43,821
Hivi unawezaje kumiliki ghorofa la bilioni 10 Kariakoo halafu unashindwa hata kuliweka katika hali ya unadhifu?!

NHC walijirekebisha hasa baada ya mchechu kuchukua ofisi, ila kuna hawa waarabu ambao hawaishi hapa nchini, wao kazi yao ni kuja kukusanya kodi na kwenda kutumbua Dubai.

Ila cha ajabu hayo maghorofa yanautandu kama wa chooni na yanachafua mandhari ya jiji, eneo la mbele ya jengo halina pavement na ni chafu mno Kama choo.

Hivi ni umaskini au ndio tumezoea tu?!
 
Ila hii hali ya uchafu kwenye majengo haipo hapa tu hata ukienda India Singapore na kwenye miji mingine hali ni mbaya nadhani ni mazoea kama unavofikiri
 
picha mkuu!
wengine tupo mwaloni hatujawahi yaona hayo mabugando machafu!

mabugando=ghorofa
 
picha mkuu!
wengine tupo mwaloni hatujawahi yaona hayo mabugando machafu!

mabugando=ghorofa

Jengo la klabu ya Simba, ni chafu unaweza kudhani mabanda ya njiwa
 
Attachments

  • SAM_0446.JPG
    SAM_0446.JPG
    46 KB · Views: 100
Ila hii hali ya uchafu kwenye majengo haipo hapa tu hata ukienda India Singapore na kwenye miji mingine hali ni mbaya nadhani ni mazoea kama unavofikiri

Angalia Utanzania wako usizidi kipimo, yaani uchafu nao tuutafutie excuse badala ya solution? Pambaf, kwa India tuige teknoojia na mawasiliano ya reli, maghorofa tuige Paris na Geneva
 
Huo ni ubishi wa kijinga. Hayo ni mafuriko, natural disaster, pale sokoni hakufuriki ni uchafu tu unaoletwa na viongozi wachafu wasio na maono.

Hapo jangwani kuna mafuriko, pale Msimbazi kuna nini kama sio uchafu?
Na jengo lako ni safi? Ati ubishi wa kijinga......unaweka uso kwenye mzinga wa nyuki unategemea kupakwa poda?
 
Mwana Mtoka Pabaya post: 16019851 said:
Jengo la klabu ya Simba, ni chafu unaweza kudhani mabanda ya njiwa
Hivi kwani ndoo ya rangi ni shilingi ngapi? Halafu tujifunze kufanya finishing za Majengo ambazo zinaresist ukungu na uchafu, sio lazima tutumie plaster na rangi. Tutumie aluco bonds na glass materials
 
Na jengo lako ni safi? Ati ubishi wa kijinga......unaweka uso kwenye mzinga wa nyuki unategemea kupakwa poda?

Nini wewe, jengo la Yanga utafananisha na hayo mabanda ya njiwa? Pale umeonesha mafuriko ambayo ni janga, lkn hujanieleza ulinganifu na la kwako ambako lipo sehemu isiyo na mafuriko.
 
Attachments

  • IMG_2293.JPG
    IMG_2293.JPG
    82.9 KB · Views: 95
Na jengo lako ni safi? Ati ubishi wa kijinga......unaweka uso kwenye mzinga wa nyuki unategemea kupakwa poda?

Ukielezwa ukweli jitazame sio unakurupuka kubishana na Wakimataifa. Jengo lenu ni chafu sbb uchafu ni zao la fikra.

Kuna tofauti ya mtu mwenye ugonjwa wa ngozi na mchafu. Mmoja anaumwa, mwingine hataki kuoga.

NENDA KAOGE
 
Mheshimiwa mkuu wa mkoa, tuondolee taswira mbaya ya jiji, majengo machafu hayahitaji mshauri mwelekezi kutoka Uswis, anza na Mchangani FC, wachafu sana.
 
Nimeona ghorofa la CCM pale lumumba, kwa kweli ni mfano wa kuiga maana ghorofa safi kabisa, hebu wekeni picha za ghorofa la CHADEMA na CUF makao makuu tuone.
 
Hivi unawezaje kumiliki ghorofa la bilioni 10 Kariakoo halafu unashindwa hata kuliweka katika hali ya unadhifu?! NHC walijirekebisha hasa baada ya mchechu kuchukua ofisi, ila kuna hawa waarabu ambao hawaishi hapa nchini, wao kazi yao ni kuja kukusanya kodi na kwenda kutumbua Dubai. Ila cha ajabu hayo maghorofa yanautandu kama wa chooni na yanachafua mandhari ya jiji, eneo la mbele ya jengo halina pavement na ni chafu mno Kama choo.Hivi ni umaskini au ndio tumezoea tu?!
Hizo n tabia ya kutopenda usafi
 
Mkuu sio waarabu wa Dubai tu,ila mengine wenyewe wapo Makete ni Wakinga,wengine ni wapemba..
 
Mkuu sio waarabu wa Dubai tu,ila mengine wenyewe wapo Makete ni Wakinga,wengine ni wapemba..
Ofcourse, Wakinga na Wapemba nao wanaendekeza uchafu kwa kuacha mijengo inapata ukungu na utandu kama wa vyoo vya manzese.wachukuliwe hatua za kinidhamu
 
Ofcourse, Wakinga na Wapemba nao wanaendekeza uchafu kwa kuacha mijengo inapata ukungu na utandu kama wa vyoo vya manzese.wachukuliwe hatua za kinidhamu

Hapo karibu na kituo cha polisi cha Msimbazi kuna nyumba mbili tatu zinafanania NHC sijui nani anakaa hapo wallah! Last time nimeyaona hali ilikuwa inatisha
 
Maisha yetu kwa kiasi kikubwa tunapigana vita dhidi ya Umasikini ba Ujinga. Na hayo maswala yanatawala kiasi kikubwa ya maisha ya kila siku. Sasa kams watu wanamiliki ghorofa au hata nyumba ya kawaida zinazowapatia kipato, hao hawasumbuliwi na umasikini bali ni ujinga.
 
Basi huu ni ujinga mbaya kabisa, waelimishwe
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom