Maghorofa kadhaa jijini yatadondoka mda wowote | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maghorofa kadhaa jijini yatadondoka mda wowote

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mozila, Sep 1, 2012.

 1. Mozila

  Mozila Senior Member

  #1
  Sep 1, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 172
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Mtanzania ambaye amebobea katika masuala ya chuma amesema majengo kadhaa (majina ninayaifadhi) yatadondoka anytime kutokana na vyuma vyake kutokupimwa ubora wake
   
 2. Columbus

  Columbus JF-Expert Member

  #2
  Sep 1, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,010
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Likitokea litakalotokea TBS ndio wa kuubeba huo msalaba kwa sababu wao ndio wenye dhamana ya kusimamia na kudhibiti ubora wa bidhaa zinazoingia na kuzalishwa hapa nchini. Wameajiriwa kisheria na wanalipwa kodi zetu kisheria na kama wameshindwa kazi hiyo hawajakataliwa kuachia ngazi watanzania wengine waifanye. Siku hizi unakuta nondo zinavunjika kama muwa na hazina urefu wa futi 40 kama inavyostahili, mfuko wa cement una kilo 45-48 badala ya kilo 50. TBS wanawaogopa au wanashirikiana na wahindi kuchakachua bidhaa ikiwemo magodoro,sabuni,dawa za mbu hazifikii ujazo na haziui mbu. NCHI HII UTAFIKIRI HAKUNA SERIKALI.
   
 3. Mama Mdogo

  Mama Mdogo JF-Expert Member

  #3
  Sep 1, 2012
  Joined: Nov 21, 2007
  Messages: 2,867
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  Wakati natafuta nondo za kujengea nilielezwa na wauzaji wataka nondo original au zitokanazo na chuma chakavu? Nikauliza hizo zitokanazo na chuma chakavu zikoje? Nikajibiwa hizo zinatengenezwa na viwanda vya chuma vya hapa nchini (Dar, Mwanza etc) na zinatokana na kuyeyusha vitanda banco vya zamani, kengele za shuleni, man hole covers, sufuria, mabakuli, magari mabovu nk na baadaye mchanganyiko huu wanaujazia mchanga wa bahari. Baada ya somo hilo nikaomba niuziwe nondo original nikaondoka zangu, na hivyo haya yanayosemwa sishangai. Swali TBS na Baraza la Ujenzi wako wapi???
   
 4. georgeallen

  georgeallen JF-Expert Member

  #4
  Sep 2, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 3,758
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  na ukaridhika kuwa umenunua nondo original? Hii nchi hakuna kitu original
   
 5. Mozila

  Mozila Senior Member

  #5
  Sep 2, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 172
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Nahisi hata lile la Tanesco makao makuu ni moja wapo.
   
 6. Mozila

  Mozila Senior Member

  #6
  Sep 2, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 172
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Nchi haina VIONGOZI ina WATAWALA
   
 7. Columbus

  Columbus JF-Expert Member

  #7
  Sep 2, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,010
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mbona wakoloni walikuwa watawala lakini mambo yalikuwa yakienda kwa kufuata taratibu na sheria? hawa waliopo hawafai hata kuitwa watawala.
   
 8. D

  Danniair JF-Expert Member

  #8
  Sep 4, 2012
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 361
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Siyo nondo tu, hata zege lenyewe linabebwa vichwani. Ukiiningia ndani ya nyumba hizi utafurahia mipasuko na nyumba zenyewe hata miaka 6 hazina. Mkandarsi ni mmpja tu jiji lote, 'LINZA'
   
Loading...