Tusubiri wakati ukweli tunaujua? Unakumbuka kulivua gamba iliishia wapi? Hakuna mageuzi ndani ya CCM zaidi ya danganya toto. Huwezi kufanya mageuzi huku umewakumbatia watoa rushwa, wapokea rushwa, wakwapuzi wa pesa za wahanga wa tetemeko, majangili na wahuni wengine mbali mbali. Angalia kuhusu mahakama ya mafisadi, baadhi ya Watanzania walioamini usanii wa kuhusu mahakama hii wakaamini huu usanii. Sasa tunaambiwa eti mahakama hiyo iko idle kwa sababu inakosa kesi za mafisadi!!!! Kweli mafisadi wote hawa wa Lugumi, Escrow, IPTL, boti uozo n.k. halafu mahakama inakaa idle!!! Kweli!? Acheni kutuzuga banaa na kutufanya wapumbavu wa kutupa.