Mmiliki wa mojawapo ya
nyumba maeneo ya Sakina jijini Arusha
kwamba nyoka aliekua akimfuga kwa
siku nyingi na kuhusishwa na imani za
kishirikina, ameuwawa na Wananchi.
Wananchi walimuua nyoka huyo na kisha
kumkata kata vipandevipande ambapo
baada ya hizi taarifa kusambaa mmiliki
wa nyumba hii aliomba kuongea na
mtandao wa ili kutoa
maelezo yake ambayo anadai ndio ukweli
wenyewe.
millardayo.com
Mr. Joseph Paschal Magesa anasema
"Mimi kama mimi kwanza ni Mkristo safi
na mzee wa kanisa na niliondoka
nyumbani jana na mke wangu kutoka
Arusha kuelekea Dar es salaam, sijui
lolote kuhusiana na hicho kitu ila
nilipofika maeneo ya Mwanga na Same
nikapigiwa simu kwamba kuna nyoka
huku ndani ya eneo la garden nyumbani,
kuna vijana niliwaacha wawili pale
nyumbani nikawaambia waambieni watu
wawasaidie kumuua huyo nyoka'
‘Wakamuita jirani yangu hapo ndipo nae
akanipigia simu nikamwambia bwana
wewe si una bunduki nisaidie kumuua
huyo nyoka ila alivyokata simu nilijua
ametekeleza kumbe aliondoka, baadae
napiga tena simu nauliza vipi naambiwa
bado yupo na watu wamejaa nikawauliza
kwani hao watu hawawezi kumuua
mpaka bunduki wakasema wanaweza
ndio baadae wakanambia wamemvuta
mkia wamemuweka nje ya geti'
‘Nikawauliza anavutika asije akawa
analeta shida wakasema anavutika,
nikawaambia mpelekeni kanisani kwa
sababu nyumbani kwangu ni jirani na
kanisa ndio wakamvuta hadi kanisani
wakammwagia maji ya baraka kisha
wakamkatakata ndo ikawa mwisho wake
hapo'.
‘Kusema kwamba nilikua nafuga kwamba
huyu nyoka ni mtoto wangu wa
kwanza….. sasa kama ni mtoto wangu wa
kwanza si inamaana na mtoto wangu
angekufa na yeye? mimi nasema
namwachia Mungu tu…….. sijawahi
kusikia Nyoka kuishi maeneo hayo toka
nimeanza kuishi kwa karibu miaka 8,
hata na mimi inanitatiza manake
nimetumiwa picha Nyoka amefungwa
kitambaa chenye maandishi mekundu
kama ya kiarabuarabu hivi…..'
‘Taarifa kwamba Nyoka huyu amevunja
kioo cha dirisha akiwa anatokea ndani ya
nyumba, sio kweli…. haipo kabisa hiyo
kitu eti kwamba ametokea ndani, hayo ni
mambo ya watu tu… hicho kioo nilikifunja
mimi wakati napanga mizigo ya ofisi
yangu… sifahamu chochote kuhusu huyu
Nyoka, Watanzania waniamini haya
ninayosema ndio yanayotoka moyoni
mwangu'