carbohydates
JF-Expert Member
- Oct 13, 2026
- 318
- 787
Jeshi la Magereza nchini Tanzania limekanusha taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikidai kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, amegoma kula chakula akiwa gerezani na kwamba mawakili wake watatu wamezuiwa kumuona.
Akitoa taarifa kwa umma, Msemaji wa Jeshi la Magereza, Elizabeth Mbezi, amesema taarifa hizo si za kweli na zinalenga kupotosha umma.
Mbezi amesema Lissu yupo salama na hajaanza mgomo wa kula chakula kama inavyodaiwa kwenye mitandao ya kijamii.
Aidha, amesema mawakili wa Lissu wanaendelea kumuona kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa.
Jeshi la Magereza limewataka wananchi kupuuza taarifa hizo na kujiepusha na kusambaza habari zisizothibitishwa, likionya kuwa usambazaji wa taarifa za aina hiyo unaweza kuwa kosa la kisheria.
Kauli hiyo ya Jeshi la Magereza imekuja siku nne baada ya Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Dk. Rugemeleza Nshala, kueleza kuwa Lissu...
Chanzo : Magereza
Pia soma: Lissu atangaza mgomo wa kula chakula kuanzia Jumatatu, 26/10/2026