Magazeti ya Shigongo yachukunguzwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Magazeti ya Shigongo yachukunguzwe

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Msema hovyo, Jul 22, 2011.

 1. Msema hovyo

  Msema hovyo Senior Member

  #1
  Jul 22, 2011
  Joined: Jul 3, 2011
  Messages: 195
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu pamoja ya kwamba mtasema ni tabia yangu kusema hovyo, lakini naona bora tu niseme.

  Hii tabia ya magazeti ya wambea kama vile uwazi, amani, ijumaa na upupu mwingine kuchapisha picha za utupu huwa imekusudia nini? Faida yake ni nini? Ina mfaidisha nani? Na ni kwa nini serikali particularly wizara ya habari haiyafungii magazeti haya kwa kukiuka sheria ya uhuru na faragha ya mtu? Ni kwa maslahi ya nani magazeti haya yanawadhalilisha watanzania? Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeweka wazi uhuru na haki ambayo mtu anayo.

  Kulingana na katiba: Banadamu wote wana Haki ya faragha na usalama wa mtu Sheria ya 1984 Na.15 ib.6
  16.-(1) Kila mtu anastahili kuheshimiwa na kupata hifadhi kwa nafsi yake, maisha yake binafsi na familia yake na unyumba wake, na pia heshima na hifadhi ya maskani yake na mawasiliano yake ya binafsi.
  (2) Kwa madhumuni ya kuhifadhi haki ya mtu kwa mujibu wa ibara hii, Mamlaka ya Nchi itaweka utaratibu wa sheria kuhusu hali, namna na kiasi ambacho haki ya mtu ya faragha na ya usalama na nafsi yake, mali yake na maskani yake, yaweza kuingiliwa bila ya kuathiri ibara hii.

  Nashangazwa na ukiukaji huu wa katiba na sheria ya nchi unaofanywa na magazeti haya kwa kuingilia uhuru wa mtu binafsi pasipo kuchukuliwa hatua za kisheria. Naamini kwamba wakiamua kufuata sheria na taratibu, wale wote waliodhalilishwa wanao uwezo wa kudai mamilioni ya fedha kwa ajili ya fidia.
   
Loading...