Yona F. Maro
R I P
- Nov 2, 2006
- 4,201
- 238
Mabadiliko ya nchi yetu yatapatikana siku vyombo vya habari vitakapoacha tabia zao za unafiki katika uhandishi na kufanya kazi yao kama inavyopaswa kuwa. Mwandishi wa habari anatakiwa awe ni mtu mwenye kuweza kufanyia jambo utafiti wa kutosha kabla ya kulitoa kwa wananchi mara tu apatapo taarifa haijalishi imetolewa na nani.Jambo la msingi ni kufanya utafiti na kuona je habari hiyo ina ukweli?,na utafiti wa kweli lazima uambatane na ushahidi.mfano tarehe 8/4/2008 spika wa bunge alijibu baadhi ya tuhuma zinazo mkabili hasa ile ya matumizi mabaya ya fedha za umma. Akasema amemuagiza katibu wa bunge bwana Foka andae taarifa ya matumizi yake ya fedha tangu 2005 hadi sasa na wabunge wapewe copy.Kwa mwandishi mwenye kuelewa kazi yake hapo ndiyo angeanzia utafiti baada ya riport ya bwana foka,Hii ripoti inatosha kukanusha au kukubali kama tuhuma ni za kweli au ni Uongo.
Mfano wa pili ni kuhusu vimada wa spika kutumia magari ya bunge vibaya.Mwandishi anatakiwa kujua je ni kweli hiyo RAV 4 ya bunge intumiwa na huyo mama sitta wa upanga(Kimada),labda alipewa lift siku moja tu!!!!!,mwandishi anatakiwa kuelewa ni mara ngapi amekuwa akiitumia hiyo RAV;kama inatumika mara kwa mara anatakiwa kutafiti zaidi ,spika kama kiongozi mkubwa kuna sheria yoyote ya nchi hii inayompa mamlaka kuwa tunza vimada(sio mkewe) kwa mali ya umma? jibu linaweza kuonyesha kama tuhuma hiyo ni ya kweli au ni majungu tu.
Mfano wa mwisho ni tuhuma kuwa kuna kimada mwingine wa spika wa hospital ya agakan ambaye spika alisema apewa per diem ya siku 50 ,pesa za serekali zikilipwa huwa lazima zisainiwe,sasa mwandishi wa kweli lazima achunguze kama hakuna malipo kama hayo basi hayo,kama hayapo basi ni majungu.
Nimeamua kueleza hiyo mifano kutokana na gazeti la mwanahalisi la tarehe 9/4/2008. Mwandishi alikurupuka tu na kuandika habari za kukanusha tuhuma za spika bila hata utafiti wowote. Nina uhakika hakufanya utafiti kutokana na mfano wa kwanza kuwa spika alielezea bungeni tarehe 8/4/2008 vizuri kuwa katibu ataandaa taarifa fedha ya matumizi ya bunge na kuwapa wa bunge. Maajabu tarehe 9/4/2008 mwandishi wa mwanahalisi akandika kuwa sio kweli ni njama za mafisadi wa EPA na richmond.mimi nikajiuliza kama tunaangalia maslahi ya taifa na zama za uwazi mwandishi hawezi tu kudanganya taifa waamini hivyo bila evidence ya utafiti. pia habari inaweza ikatolewa na mtu yoyote point ya msingi kwa umma ni ya ukweli wa habari hiyo.Sisi wana JF hatujali ni nani source ya habari ila tunajali ukweli wake.
Hapa naanza kuona yale yale ambayo yamekuwa yakiandikwa kuwa huwa wahandishi wa habari wanapewaga rushwa ili waandike habari za uongo kwa malengo na sababu wanazozijua wenyewe. Hivi kweli kama ni hivyo tutaweza kujenga hiyo Tanzania tunayoiimba???.
Nasikitika kusema baadhi magazeti unakuta kama yameanzishwa kwa nia ya kumchafua mtu au kikundi cha watu fulani tu. Mfano gazeti la Tanzania Daima lilifanya utafiti kwa mahojiano na katibu wa bunge na kupata ufafanuzi wa baadhi ya tuhuma lakini gazeti la mwanahalisi la tarehe 2/4/2008 likakanusha katika ukurasa wa pili na kuwaponda sana.Ila ukweli ni kwa gazeti Tanzania Daima halina ubaguzi katika kutoa habari za matukio nchini
Wananchi wanasoma magazeti yote kwa lengo la kupata habari za matukio yanayotokea sasa kama magazeti yatakuwa yanatoa habari kwa upendeleo wananchi wanabaki njia panda bila kuelewa ukweli na uzushi ni upi????.WAHANDISHI wafanye utafiti na waandike kilicho kweli na sio kufunika ufisadi.
Pia waache matumizi ya lugha chafu,kwani kama mwandishi anataka kufikisha ujumbe kwa jamii akieleza kwa lugha safi bado ukweli utakuwepo pale pale na jamii itaelewa hivyo hivyo .kuna toleo la mwanahalisi la marchi,2008 kabla ya kikao cha BUTIAMA walimtukana raisi kwa kumwambia kuwa ana kimbele mbele,ile sio lugha ya uhandishi hata kama rohoni uliona ana kimbele mbele mwandishi angeandika facts zote ili msomaji aone rohoni mwake kuwa rahisi anachofanya ni kile alichokita kimbele mbele.Wakati mwingine ukisoma magazeti ya Tanzania unashindwa kutofautisha habari ya gazetini na ya makuli kariako au wale piga debe wa stand ubungo kutonana na matumizi ya lugha zao kufanana. Lazima wahandishi watoe taarifa zao tofauti na watu wa mitaani bila kupotosha ukweli na maana ya habari.Pia Rais kama kiongozi wa nchi anapaswa kuheshimiwa na pia wananchi wote tuheshimiane ,tunaweza kupeana ukweli kwa kutumia lugha safi na tutaelewana tu.
Mwisho napenda kutoa rai na changamoto kwa watanzania kuwa wasisite kuwafichua mafisadi wanaotumia mali ya umma vibaya,kazi imeenza aluta kontiniwa