Magazeti Na Ufisadi

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
Mabadiliko ya nchi yetu yatapatikana siku vyombo vya habari vitakapoacha tabia zao za unafiki katika uhandishi na kufanya kazi yao kama inavyopaswa kuwa. Mwandishi wa habari anatakiwa awe ni mtu mwenye kuweza kufanyia jambo utafiti wa kutosha kabla ya kulitoa kwa wananchi mara tu apatapo taarifa haijalishi imetolewa na nani.Jambo la msingi ni kufanya utafiti na kuona je habari hiyo ina ukweli?,na utafiti wa kweli lazima uambatane na ushahidi.mfano tarehe 8/4/2008 spika wa bunge alijibu baadhi ya tuhuma zinazo mkabili hasa ile ya matumizi mabaya ya fedha za umma. Akasema amemuagiza katibu wa bunge bwana Foka andae taarifa ya matumizi yake ya fedha tangu 2005 hadi sasa na wabunge wapewe copy.Kwa mwandishi mwenye kuelewa kazi yake hapo ndiyo angeanzia utafiti baada ya riport ya bwana foka,Hii ripoti inatosha kukanusha au kukubali kama tuhuma ni za kweli au ni Uongo.

Mfano wa pili ni kuhusu vimada wa spika kutumia magari ya bunge vibaya.Mwandishi anatakiwa kujua je ni kweli hiyo RAV 4 ya bunge intumiwa na huyo mama sitta wa upanga(Kimada),labda alipewa lift siku moja tu!!!!!,mwandishi anatakiwa kuelewa ni mara ngapi amekuwa akiitumia hiyo RAV;kama inatumika mara kwa mara anatakiwa kutafiti zaidi ,spika kama kiongozi mkubwa kuna sheria yoyote ya nchi hii inayompa mamlaka kuwa tunza vimada(sio mkewe) kwa mali ya umma? jibu linaweza kuonyesha kama tuhuma hiyo ni ya kweli au ni majungu tu.

Mfano wa mwisho ni tuhuma kuwa kuna kimada mwingine wa spika wa hospital ya agakan ambaye spika alisema apewa per diem ya siku 50 ,pesa za serekali zikilipwa huwa lazima zisainiwe,sasa mwandishi wa kweli lazima achunguze kama hakuna malipo kama hayo basi hayo,kama hayapo basi ni majungu.

Nimeamua kueleza hiyo mifano kutokana na gazeti la mwanahalisi la tarehe 9/4/2008. Mwandishi alikurupuka tu na kuandika habari za kukanusha tuhuma za spika bila hata utafiti wowote. Nina uhakika hakufanya utafiti kutokana na mfano wa kwanza kuwa spika alielezea bungeni tarehe 8/4/2008 vizuri kuwa katibu ataandaa taarifa fedha ya matumizi ya bunge na kuwapa wa bunge. Maajabu tarehe 9/4/2008 mwandishi wa mwanahalisi akandika kuwa sio kweli ni njama za mafisadi wa EPA na richmond.mimi nikajiuliza kama tunaangalia maslahi ya taifa na zama za uwazi mwandishi hawezi tu kudanganya taifa waamini hivyo bila evidence ya utafiti. pia habari inaweza ikatolewa na mtu yoyote point ya msingi kwa umma ni ya ukweli wa habari hiyo.Sisi wana JF hatujali ni nani source ya habari ila tunajali ukweli wake.

Hapa naanza kuona yale yale ambayo yamekuwa yakiandikwa kuwa huwa wahandishi wa habari wanapewaga rushwa ili waandike habari za uongo kwa malengo na sababu wanazozijua wenyewe. Hivi kweli kama ni hivyo tutaweza kujenga hiyo Tanzania tunayoiimba???.

Nasikitika kusema baadhi magazeti unakuta kama yameanzishwa kwa nia ya kumchafua mtu au kikundi cha watu fulani tu. Mfano gazeti la Tanzania Daima lilifanya utafiti kwa mahojiano na katibu wa bunge na kupata ufafanuzi wa baadhi ya tuhuma lakini gazeti la mwanahalisi la tarehe 2/4/2008 likakanusha katika ukurasa wa pili na kuwaponda sana.Ila ukweli ni kwa gazeti Tanzania Daima halina ubaguzi katika kutoa habari za matukio nchini

Wananchi wanasoma magazeti yote kwa lengo la kupata habari za matukio yanayotokea sasa kama magazeti yatakuwa yanatoa habari kwa upendeleo wananchi wanabaki njia panda bila kuelewa ukweli na uzushi ni upi????.WAHANDISHI wafanye utafiti na waandike kilicho kweli na sio kufunika ufisadi.

Pia waache matumizi ya lugha chafu,kwani kama mwandishi anataka kufikisha ujumbe kwa jamii akieleza kwa lugha safi bado ukweli utakuwepo pale pale na jamii itaelewa hivyo hivyo .kuna toleo la mwanahalisi la marchi,2008 kabla ya kikao cha BUTIAMA walimtukana raisi kwa kumwambia kuwa ana kimbele mbele,ile sio lugha ya uhandishi hata kama rohoni uliona ana kimbele mbele mwandishi angeandika facts zote ili msomaji aone rohoni mwake kuwa rahisi anachofanya ni kile alichokita kimbele mbele.Wakati mwingine ukisoma magazeti ya Tanzania unashindwa kutofautisha habari ya gazetini na ya makuli kariako au wale piga debe wa stand ubungo kutonana na matumizi ya lugha zao kufanana. Lazima wahandishi watoe taarifa zao tofauti na watu wa mitaani bila kupotosha ukweli na maana ya habari.Pia Rais kama kiongozi wa nchi anapaswa kuheshimiwa na pia wananchi wote tuheshimiane ,tunaweza kupeana ukweli kwa kutumia lugha safi na tutaelewana tu.

Mwisho napenda kutoa rai na changamoto kwa watanzania kuwa wasisite kuwafichua mafisadi wanaotumia mali ya umma vibaya,kazi imeenza aluta kontiniwa
 
mkuu sio tatizo lao bali wanatumiwa hao,unajua kipindi cha Ben alikuwa anawapiga mikwara ila muungwana yeye hawapigi mikwala ila anawaua kisomi na ndio Dunia ya sasa,anawatumia mamluki wanakurupuka then hoja zote zinaonekana ni pumba na kupoteza maana nzima.
Mimi nadhani waandishi wenye uchungu wasisite kuanikana ili kuwaondoa kapuni wale mamluki,ni hayo tu nawahi Chaofani yangu isije ikaungua..
 
Kaka Mimi sio mwandishi by proffessional lakini najua kutofautisha makala na habari, makala iliyoandikwa na mtu mwingine gazeti likaichapa inaweza kutofautiana na habari iliyoandikwa na gazeti lenyewe am not sure lakini naona ndo system kwa kuwa magazeti yetu yako hivyo, lakini hawa viongozi wamezidi mbona unaongelea vimada ujaonegelea vitu vya msingi ambavyo hata six mwenyewe amekubali kuwa nikweli he was being paid 2m per week kwa ajiri ya dawa za miguu, vimanda ni miner issue kwa maendeleo ya waTZ isipokuwa yule ambaye anatumia gari la serikali na hii imedhibitishwa na magazeti mengine acha mwanahalisi, usiwe biased tunajua unawapenda CCM lakini ni mafisadi na hata wao wameshakiri kuwa ni mafisadi pia kwa kuwa na nyumba ndogo nyingi in some threads here wakati tunaongelea uchaguzi wa UVCCM.
let be objective katika kuakikisha chama chetu kitukufu kinajisafisha na kuendelea kufanya mambo mazuri kwa taifa. mojawapo ya mambo ambayo yanasababisha wanakuwa mafisadi ni kuwa na wanawake kila kona ya nchi na spika anajulikana kwa hilo
 
hivi viandishi vya bongo ni uharo mtupu, wakati watu wenye akili timamu wnahaha kuhakikisha hela za BOT zinarudi, utakuta mwandishi anapamba gazeti kwa kichwa kikubwa cha habari "wawaaa balali" kisha ukienda kuisoma hiyo habari yenyewe sasa uanaweza kutapika...
 
Ni kweli mimi mwenyewe binafsi napata shida sana nikiwa Tz kuyaelewa magazeti yetu,lipi ni gazeti bora na lipi ni bora gazeti, to be honest waandishi wetu wa habari they are far from being better when it comes to comparisons with our neighbours countries.

Penngine tatizo ni juu ya ukweli kwamba taalumu ya habari (mass communication) ni changa bado sana nchini kwetu na still wanahabari wetu wana mengi ya kujifunza.

Lakini pamoja na hayo Shy, its looks like ur thread ipo subjective kiasi flani au imelenga katika ''kuwatetea'' watu fulani at the same time ''kuwakandamiza'' watu fulani, all in all u ve come with a good food of mind.
 
mkuu sio tatizo lao bali wanatumiwa hao,unajua kipindi cha Ben alikuwa anawapiga mikwara

mkuu kilongwe,

kabla ya mkapa kuwa waziri alishwahi kuwa mhariri wa Gazeti la serikali,hivyo anajau utaratibu mzima wa habari unavyotoka na ilikuwa si rahisi kwa yeye kuanikwa hadharani zaidi ya kuandamwa na GAZETI la RAI la kipindi hicho.

na sasa kuna gazeti la MWANAHALISI NA RAIA MWEMA,na sijui lengo lao ni lipi..isije ikawa ndio mambo haya haya,watu wanajipigia kampeni kwa kuponda na kufichua maovu ya wengine ili waaminiwe.Ila Mwanakijiji alishasema kwa sasa wakitaka kutuzuga watuzuge tukazugika.

Mie nafikiri siku zote,tuweke azimio na lengo moja,Tuhakikishe katika serikali za Mitaa na Wabunge kuwepo na ushindani,yaani tuchague viongozi wengi kutoka upinzani ili tuharakishe maendeleo.ila kwa Urais wapinzani bado sana tunahitaji kuwa na kina Mwanakijiji 100,Kina Zitto 50,kina FMES 100,kina Gembe 50,Halisi 39 na mwafrika wa kike 10,then ndio tuanze kufikiria urahisi
 
Ni kweli mimi mwenyewe binafsi napata shida sana nikiwa Tz kuyaelewa magazeti yetu,lipi ni gazeti bora na lipi ni bora gazeti, to be honest waandishi wetu wa habari they are far from being better when it comes to comparisons with our neighbours countries.

Penngine tatizo ni juu ya ukweli kwamba taalumu ya habari (mass communication) ni changa bado sana nchini kwetu na still wanahabari wetu wana mengi ya kujifunza.

I have long stopped reading alot of papers back home. I prefer Daily Nation Newspaper and watch the news in the evening. good thing my office back home provides a notice board with Newspaper cuttings that are important in a sense.
The closest I get to buying a newspaper is the Citizen na Mwananchi. Wengine naona bado kabisa
 
Lakini kakabraza ushishangae aina ya uandishi wa bongo. Yote ni matokeo ya ubangaizaji. Ukifanya a simple research juu ya cvs za waandishi wengi wa bongo unaweza kukuta wengi wao ni wale waliofeli skuli aidha walidualisha au walipata 4 zisizobebeka. Na kwa kuwa mfumo wa elimu enzi hizo haukutoa kipaumbele katika taaluma ya mass communications, wamiliki wa vyombo vya habari walijikuta wakiwakimbilia aina ya waandishi waliopo kwa kuwa ni cheap.
 
nafikiri tatizo kubwa sana kwa waandishi habari tanzania ni uwezo mdogo wa kuchambua mambo na uwoga wa kupambana na changamoto za kiuandishi..........Si Lazima mtu awe amenunuliwa ili kuandika pumba inawezekana uwezo wake wa kutafakari uliishia hapo ambao wewe mwenye uliyetafakari vizuri unaona kama anatumiwa....(Pia kitu kiitwacho exposure kwa waandishi wetu ni muhimu sana )
THE MOST IMPORTANT THING IN COMMUNICATION IS TO UNDERSTAND THE UNSPOKEN WORDS
 
Ninavyojua mimi, kuna magazeti ya vyama, binafsi, udaku, michezo, comedy nk. Upande wa magazeti ya chama, yapo ya CCM na Upinzani. kuwa gazeti la chama siyo lazima limilikiwe na chama ila linakuwa na mwelekeo wa chama fulani.

Shy usishangae hayo. Ila ninapingana nawewe kwamba "Mabadiliko ya nchi yetu yatapatikana siku vyombo vya habari vitakapoacha tabia zao za unafiki katika uhandishi na kufanya kazi yao kama inavyopaswa kuwa" mabadiliko yanachangiwa na vitu vingi sana siyo waandishi wa habari peke yao.
[/SIZE]
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom