Magavana wanaopinga chanjo kwa lazima kushitaki serikali

Magavana wanaopinga chanjo kwa lazima kushitaki serikali

Analogia Malenga

Platinum Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,292
Reaction score
10,844
Magavana wa chama cha Republican wanatarajiwa kuishitaki serikali kuu ya Marekani hii leo kukomesha utawala wa rais Joe Biden kutekeleza amri ya kutaka wafanyakazi wa serikali kupata chanjo dhidi ya virusi vya Corona kwa lazima.

Magavana hao wanasema amri hiyo inavunja uhuru wa watu.

Gavana wa Florida Ron DeSantis, amesema kwamba ataungana na magavana wa Georgia na Alabama katika kesi dhidi ya utawala wa Biden, kupinga amari hiyo itakayoanza kutekelezwa Januari tarehe 4.

Ron DeSantis, amesema kwamba serikali haiwezi kulazimisha sera ya kimatibabu kwa watu kwa kudai kwamba inatekeleza masharti ya kikazi.

Magavana wa Indiana, Iowa na Nebraska nao wametangaza kupinga sera hiyo mahakamani.

Gavana wa Texas Ken Paxton ambaye pia ni mrepublican, ametangaza kushitaki mahakamani sera hiyo ya serikali kuu

VOA Swahili
 
Hawa magavana wanajielewa sana.Hapa kwetu jaribu !!!!!
 
Kwa wale wapigia debe chanjo wa kwa Mtogole na Buza sijui nao wanasemaje maana huko ndiko kuna kiini cha chanjo na covid yenyewr lakin wanapinga
 
Kwa wale wapigia debe chanjo wa kwa Mtogole na Buza sijui nao wanasemaje maana huko ndiko kuna kiini cha chanjo na covid yenyewr lakin wanapinga
Sijui Ni Utahira au uwendawazimu au Ni Nini. Ni wapi pameonesha kwamba hao Magavana wanapinga chanjo? Elimu,Elimu Elimu.
 
Vizuri sana, hiyo itakuwa reflected mpaka huku nchi maskini.
 
Hiyo ndio maana ya demokrasia.kua huru,sio kupangiwa kila kitu
 
Back
Top Bottom