Kwa muda mrefu tumekuwa tukiyaona magari yanayopaa kama sinema ya yule kachero maarufu James Bond...kwenye sinema zake. Ebu zuru hapa kwa taarifa zaidi.
iyo itapunguza foleni, kama natoka kimara kwenda posta, nikiona kuna lifoleni ubungo mataa,shekilango,mapipa na fire...narusha gari yangu juuuuu naenda dondokea akiba afu namalizia pale kwenda posta. hapo vipi!
Kisa cha ndege ya jeshi kutumia barabara ya magari..sijui itakuaje kwa magari kama haya kutumia anga kwa nchi kama bongo ambapo hata trafiki polisi hwawezi kusaidia kuzuia ajali..how will it be for air traffic controllers..na mbwembwe zetu za kutaka kupita hata service road wakati wa foleni na pengine ukiwa kwenye ngoma kali unataka kufunga breki kila mara kuwasalimia wadau ili wakuone... sasa huko angani si itakuwa vibweka unapokutana na ngoma ya mrembo utataka usalimie kwa kuigandisha gari hewani?. I do think pia unahitaji courage na utaalamu wa kutosha kurusha aina hii ya gari/ndege..is extra cost kwa mazingira yetu.