Magari yanayohitajika Tanzania

Magari yanayohitajika Tanzania

punguzo

Member
Joined
Jul 9, 2011
Posts
51
Reaction score
6
Ndugu,
Mimi nipo UK na Nimpango wa kurudi nyumbani hivi karibuni, ningependa kununua gari ambalo ninaweza kuliuza kiurahisi au ambalo limekaa kibiashara kwa mazingira ya kiTanzania.Hivyo basi napenda kuwaomba ushauri wana JF wenzangu ni gari gani ninaweza kununua na kuliuza kwa urahisi nikifika Tanzania au ni magari gani yapo kwenye mahitaji kwa sasa?

Natumaini nitapata ushauri mzuri na wenyekufaa

Natanguliza shukrani zangu

MwanaJF
 
Kwa uozo wa barabara za kibongo, lete Land Rover, do not bring any salon car as hapa Tanzania hakuna barabara za kuendeshea hayo magari kwa sababu ya kuwa na mashimo kila sehemu. Watu wanakuja na masalon hapa baad ya miezi mitatu yako juu ya mawe. Gari zuri la kuendesha hapa Bongo ni any SUV ambalo limepanda juu kidogo, Land Rover (not Ranges as they are too low), that's it. Apart from that unajiletea hasara tu huku.
 
Your choice should be, a 4WD vehicle any model brand should work in Bongoland roads. Cheers!
 
kwani we una uwezo wa kuleta gari gani? Watu wanataka ma range, landrover, hata yale ya paund laki 3 lete tu
 
isije kuwa nyie ni wale matapeli mnasema gari gani mara tuma dola 4 mnaingia kizani
 
isije kuwa nyie ni wale matapeli mnasema gari gani mara tuma dola 4 mnaingia kizani

Usiwe na wasi wasi ndugu yangu, mimi ni mtanzania niliyehitaji ushauri tu, na wala badiko langu halina viashiria vya kitaperi, ila wewe tu na wasiwasi wako usio na msingi ambao unatufanya sisi watanzania tusiendelee! sijakutaka au sijauliza mtu wa kununua, nimeomba ushauri wa gari gani zinahitajika tanzania ila hata nikitaka kuuza nisipate shida. ni karesearch tu kadogo ndugu yangu
 
kwani we una uwezo wa kuleta gari gani? Watu wanataka ma range, landrover, hata yale ya paund laki 3 lete tu

kaka, yale ya £300,000/= sina uweze nayo ila mtu akitaka kufanya deal na mimi nipo tayari! ha! ha! ha! haaaaaaaaaaa!
uwezo wangu ni wa gari kwa matumizi ya kawaida kwa mtu wa wastani au gari ya kibiashara, inayoweza kukidhi mahitaji kama ya kupeleka wanafunzi shule na mahitaji mengine ya kibiashara kwa mazingira ya kiTZ!
 
Jamani vipi na freelander?? Maana kila watu wana hadithi zao?? Naomba ushauri wa dhati wana J4
 
Gari lolote unaloweza kununua chukua tu ila lisiwe made europe kwani spare zitakusumbua kupatikana na hasa kama ni kitu ambacho hakibadilishwi mara kwa mara. Hata saloon zipo nyingi tu wala wasikutishe ila mini-SUV ni nzuri zaidi in terms of engine, fuel consumption and wakati wa mvua/mashimo. Siku hizi unaweza toka na saloon Dar mpk mwanza, then musoma, kisumu, nairobi, arusha, manyara, singida, dodoma, morogoro, iringa, mbeya na ukarudi Dar..ni sehemu chache sana huwezi kwenda na saloon na kama ni mfanyakazi Dar basi hakuna tatizo labda wkt wa msimu wa mvua na uwe unakaa jangwani mtoni
 
Njoo na Scania 93H,M HP 280,250. Pia kama una nguvu kubwa njoo na 133HP360.
Kwa gari ndogo njoo na Toyota Avensis huwa zinapatikana UK japo manual lkn utapiga deal kuna wanaopenda manual hasa mikoani
 
Usiwe na wasi wasi ndugu yangu, mimi ni mtanzania niliyehitaji ushauri tu, na wala badiko langu halina viashiria vya kitaperi, ila wewe tu na wasiwasi wako usio na msingi ambao unatufanya sisi watanzania tusiendelee! sijakutaka au sijauliza mtu wa kununua, nimeomba ushauri wa gari gani zinahitajika tanzania ila hata nikitaka kuuza nisipate shida. ni karesearch tu kadogo ndugu yangu
yupo jamaa mmoja tapeli sana ameniuza bado namlia taiming ya kumuanika kwenye mitandao yo yote duniani anajifanya yupo hongkog ni rafiki yangu nitamuanika kwa majina yake yote matatu na paspot namba yake na picha yake
 
mkuu fanya hivyo haraka tusije na sisi ndugu zako tukaingizwa mkenge ... tutakosa wote .... kama amekutapeli usimwonee nyani aibu ... weka hadharani
 
mkuu fanya hivyo haraka tusije na sisi ndugu zako tukaingizwa mkenge ... tutakosa wote .... kama amekutapeli usimwonee nyani aibu ... weka hadharani
nitamwanika soon kanirudisha nyuma sana huyu nguruwe
 
Back
Top Bottom