Magari yanauzwa Zanzibar

Magari yanauzwa Zanzibar

chamlungu

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2012
Posts
326
Reaction score
339
Aina tofauti za magari yako katika hali nzuri. Yanapatikana Zanzibar kama ifuatavyo: Toyota Prado ya 2003 kwa 27m, Toyota Harrier ya 2005 kwa 27m,Nissan Xtrail kwa 13m. Aliye serious anipm. Note: Kuja kuyaona/kuyakagua kwa gharama zako
 
Magari yanauzwa hamna hata picha au hayo magari hayafai kuweka humu .
 
Weka picha tuyaone mdani, nje, injini etc katika muonekano wa nyuma, mbele na pembeni...... unaficha nini?
 
Hiyo bei inajumuisha gharama za kulisafirisha na kulitoa bandarini?
 
Hiyo bei inajumuisha gharama za kulisafirisha na kulitoa bandarini?

hiyo ni bei ya kuuzia. Haijumuishi gharama hizo na nyingine zozote. Ila kutokana na uzoefu wetu tunaweza kukusaidia
 
Weka picha tuyaone mdani, nje, injini etc katika muonekano wa nyuma, mbele na pembeni...... unaficha nini?

yapo mengi na aina tofauti. Nipm kama Una whasApp nikutumie picha. Na utakuwa umenisaidia ukinitajia aina ya gari uitakayo
 
Magari yanauzwa hamna hata picha au hayo magari hayafai kuweka humu .

inawezekana mkuu,lakini simu inagoma kuapload files. Naweza kukutumia kwenye WhasApp ukinipa namba
 
Ushauri wa bure kwa muweka post:-
Nikupe dili la biashara kwa uzoefu wangu wa hapa Zanzibar na Mainland.
Watu lazima tuamke na tuache biashara za kizamani za kusubiri mteja mlango.

Zanzibar kiwastan wa eneo la mraba,ndio inaongoza kwa kuwa na Yard nyingi za magari ndani ya mji,Mjini Magharibi.
Cha kushangaza,hakuna hata yard moja yenye website,zaidi ya watu kusubiri wateja mlango.
97% ya soko la magari Linategemea wateja kutoka Mainland.Na dunia kama kijiji unapo mfeed mtu maelezo ya kutosha kuhusu bidhaa ndio jinsi unavyoweza kumshawishi aweze kuwa na dhamira sahihi ya ununuzi.
Niliwahi kumpa mtu hili wazo tena ni mmiliki wa Yard,lakini jibu lake ni kwamba yeye anauzoefu wa miaka mingi na hayo mambo yamekuja juzi tu ya mitandao.So,haimuathiri kitu.

Lakini ukweli ni kwamba kuna baadhi Yard hapa Zanzibar haziuzi gari zaidi ya mbili kwa mwezi.Sasa unajiuliza mtu unaweka mamilioni ya pesa halafu unashindwa kufanya juhudi ya kutangaza biashara yako katika hali ya ushindani wa soko la sasa.

Watu wengi wa Bara wanania na hamu kubwa ya kuja kununua magari na bidhaa nyingine huku,lakini wanashindwa na pia wanasita kuja kununua gari huku kwa kukosa information za kutosha.
Nakushauri mleta mada,kama ni dalali basi najua ni ngum kwako,ila kam una Yard basi badilika uwe kisasa zaidi.
Maana najua kwanini picha hujaweka,hii ni kutokana na mazingira ya bisahara zetu hapa unguja hasa kwa dalali.

Tabia ya Biashara za hapa Zanzibar ni kuiga,akianza mmoja basi watu mia watafuata,hembu tubadilike.
 
Ngoja mie nijipange mwakani.
Nahisi nitakuwa na muda wa kutosha wa kufanya mzunguu kwenye yard mbali mbali na kupost.
Acha nimalizie mipango yangu kwa sasa,maana inahitaji muda na kujipanga.Ili nilete mapinduzi mapya ya biashara hii kisasa zaidi.Ili mtu akija anakuja na full infor na sio kuja kuzurura kutwa nzima
Nitatengeneza website kwa kazi hiyo tu.Mwezi ujao naenda kenya kuna jamaa nataka nimpe majukum ya kuifanya na mwisho wa Janurary au February mtapata website ya kisasa kabisa kuhusu biashara ya magari Zanzibar.
 
Mkuu kama una Suzuki Jimny miaka kati ya 2005 na 2007 nipe bei ili nije huko kipindi hiki cha sikukuu
 
Aina tofauti za magari yako katika hali nzuri. Yanapatikana Zanzibar kama ifuatavyo: Toyota Prado ya 2003 kwa 27m, Toyota Harrier ya 2005 kwa 27m,Nissan Xtrail kwa 13m. Aliye serious anipm. Note: Kuja kuyaona/kuyakagua kwa gharama zako

Aisee napata Toyota IST....kama ipo ni bei gan......nichek kwa PM

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom