SI KWELI Magari yakibebwa na mafuriko huko Nairobi

SI KWELI Magari yakibebwa na mafuriko huko Nairobi

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1


1774074307466.png
 
Tunachokijua
Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi la Kenya (National Police Service) iliyotolewa Machi 23 2026, Jiji la Nairobi ni eneo lililoathirika zaidi na mafuriko kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha nchini humo, kukiwa na vifo 37 vilivyoripotiwa katika jiji hilo huku vifo vya jumla vikifikia 81 na uharibifu mkubwa ukitokea katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.


Madai

Kumekuwapo na video inayosambazwa mtandaoni ikionesha hali ya mafuriko huku magari yakisombwa na kudaiwa kuwa ni tukio lililotokea Nairobi nchini Kenya.

Je, ni upi uhalisia wa Video hiyo?

Ufuatiliaji wa JamiiCheck kupitia Google Reverse Image Search umebaini eneo halisi linaloonesha jengo la Odeon linalopatikana katika makutano ya Barabara ya Latema na Mtaa wa Tom Mboya jijini Nairobi.​

1774250956208-png.3561609
Aidha kupitia Google Earth ambayo inaonesha mazingira halisi ya eneo hilo ambapo hayafanani na video inayodai kuonesha mafuriko katika eneo hilo. Mfano saa, mabango na kadhalika havionekani katika video hiyo.​

1774250778059-png.3561608

Aidha kupitia nyenzo za kubaini maudhui yaliyotengenezwa kwa akili unde zinabainisha kuwa video hiyo imetengenezwa kwa teknolojia hiyo.

1774251582115-png.3561612
Video kama hii imetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya akili unde kwa kurejelea matukio halisi yaliyowahi kutokea jijini Nairobi, ambapo inaonyesha magari yakisombwa na maji. Hata hivyo, video hiyo inakosa uhalisia kwa kuwa inaonyesha magari yakiwa yamepinduka, jambo ambalo halilingani kikamilifu na hali halisi ya matukio hayo. kando na hivyo kwa kutumia ufuatiliaji google reverse search inabainisha picha halisi ya eneo inapatikana katika jiji la Nairobi ndani ya viunga vya Central Business Distict vikiwa na jina la ODEON
 
Kwa picha zilizopo mtandaoni muonekano wa mazingira karibu na jengo la Odeon haufanani na kwenye video ya mafuriko.
 
Back
Top Bottom