Magari ya serikali yakampenia CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Magari ya serikali yakampenia CCM

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Zak Malang, Aug 26, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Aug 26, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  LICHA ya sheria na kanuni za Uchaguzi kuzuia matumizi ya magari ya serikali, msafara wa mgombea urais wa CCM Jakaya Kikwete umetumia magari kadhaa ya serikali katika mikoa ya Mwanza, Geita na Kagera.

  Mbali na magari hayo, wakuu wa wilaya waliokuwa wameshiriki msafara wa mwenyekiti huyo wa CCM, walitumia magari yao ya kazi yakiwa yamewekwa namba binafsi huku wakivalia sare za chama hicho.

  Ukiondoa magari maalumu ya walinzi wa mgombea huyo ambaye pia ni rais, magari mengine ya wakuu wa wilaya na wakuu wa idara mbalimbali za serikali, yalitumika na kuwekwa namba binafsi.

  Kwa mujibu wa habari tulizozipata kutoka vyanzo vyetu zinaeleza kuwa hivi sasa Ikulu ya Dar es Salaam ina upungufu kwa kuwa wafanyakazi wa Ikulu hasa madereva pamoja na wapishi na wagawa vinywaji (waandazi), wanatumika katika kampeni za Rais Kikwete.

  Wapishi na waandazi hao wamepelekwa mikoani kulingana na ziara za kampeni.

  "Cha ajabu ni kuwa baadhi ya wafanyakazi wa Ikulu hasa madereva, wapishi na waandazi wanatumika katika kampeni za CCM kupitia Rais Kikwete.

  "Wamegawanywa katika mikoa tofauti kulingana na ratiba za ziara za kampeni za rais,'' kilisema chanzo chetu.

  Juzi jijini Mwanza Mkuu wa wilaya Ilemela, Serenge Mrengo ambaye alifika majira ya saa 4:35 asubuhi uwanja wa ndege na gari lenye namba za STK 3551 huku wote wawili na dereva wake wakiwa wamevalia sare za CCM, lakini baada ya kusalimiana na viongozi wenzake, aliondoka.

  Akiwa wilayani Geita, Mkuu wa wilaya hiyo Philemon Shelutete alitumia gari lake la serikali ambalo lilikuwa limebandikwa namba T 804 BCZ huku akiwa amevalia sare za CCM. Pia gari la Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Benson Katala lilitolewa namba za serikali na kubandikwa namba T 180 BKW.

  Mkuu wa mkoa wa Mwanza Abbas Kandoro alitetea hatua hiyo akisema sio kosa kwa kuwa Kikwete bado ni rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanania.

  Kandoro, alikiri kutumika kwa magari hayo ya serikali na kusema kuwa viongozi hao waliyatumia kumpokea na baadhi yao waliambatana naye katika ziara hiyo kwa kuwa mbali na kuwa mgombea wa CCM pia anayo hadhi ya urais.

  "Huyu ni Rais, amekuja kama kiongozi licha ya kwamba anagombea, bado hajavuliwa urais, sasa ma-DC walikuja kama viongozi wa serikali kumpokea rais. Kama kuna mkuu wa wilaya alivaa shati la CCM alivaa kwa sababu ya mapenzi yake kwa chama," alifafanua Kandoro ambaye alitumia gari binafsi la kiongozi mmoja wa CCM Kanda ya Ziwa.

  "Makosa ni kiongozi wa serikali kufanya kazi za chama na sioni kama kuna kiongozi wa serikali ambaye alifanya kazi za chama,"alisema

  Msafara wa Kikwete kuambatana na magari ya serikali haukuishia Mwanza na Geita pekee bali pia hata mkoani Kagera ambako magari mengi yalikuwa na namba za STK.

  Katika hatua nyingine, uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Bugando umetoa ufafanuzi kwamba uamuzi wake wa kutoa gari la kubebea wagonjwa katika msafara wa mgombea urais wa CCM kuhakikisha usalama wa mgombea huyo.

  Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Dk Charles Majinge alisema kwa kawaida jukumu la kutoa magari huwa lipo mikononi mwa uongozi wa mkoa ambao uliomba gari kwao na wao waliamua kutoa gari hilo la wagonjwa namba T 848 AWN.

  "Sisi hatutoi ambulance kwa wagombea, ila tulitoa kwa Kikwete kutokana na kuwa ni kiongozi wa nchi. Kutoa magari huwa ni kazi ya uongozi wa mkoa, lakini sisi kama watalaamu wa matibabu tulichukua tahadhari na kuweka gari hilo," alieleza Dk Majinge.

  Alisema kwa vile akiwa jijini Mwanza aliwahi kuanguka, basi waliamua kuchukua tahadhari kuepuka kukosa huduma haraka iwapo jambo hilo lingejirudia akiwa mbali na hospitali ya rufaa.

  Akizungumzia gari hilo, Kandoro alisema uwapo wake ni utaratibu wa kawaida katika misafara ya viongozi wa serikali.

  "Huu ni utaratibu wa kawaida katika misafara ya viongozi, tumetoa kama utaratibu wa kawaida….unajua huyu ni kiongozi wa nchi, sasa unataka wakija na wagombea wengine wa upinzani nao tuwapatie magari ya wagonjwa, wao ni akina nani?" alieleza na kuhoji Kandoro ambaye pia aligombea kura za maoni kuwania kuteuliwa na CCM kuwa mgombea ubunge Jimbo la Kalenga na kushindwa.

  Akizungumza kwa sharti la kutotaja jina gazetini mmoja wa viongozi ambao walikuwa wakishughulika na kuratibu msafara huo alieleza kuwa gari hilo la wagonjwa ni lile ambalo lilitolewa na serikali ya Ujerumani chini ya ushirikiano wa Jiji la Mwanza na Wurzburg.

  "Gari hili liliandaliwa kutokana na maofisa wa usalama kuliomba na hili agizo limetolewa katika mikoa yote ambako atafika, kwani katika kampeni anakuwa amekwenda hadi katika wilaya ambazo haina hospitali na ikitokea dharura akimbizwe haraka hospitali huku akiendelea kupatiwa matibabu" alieleza kiongozi huyo wa chama.

  Hata hivyo, alisema gari hilo wao kama chama hawakuambiwa wala kuelekezwa kulilipia kwa vile ofisi ya mkoa ilisema watachukua wao katika hospitali ya Bugando, baada ya kuwasiliana na ofisi ya mganga mkuu wa mkoa.

  Chanzo: Mwananchi
   
 2. Shoo Gap

  Shoo Gap JF-Expert Member

  #2
  Aug 26, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 236
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  KATIBA KATIBA KATIBA IMEOZA. Anagombea Rais na raia wapi na wapi?
   
 3. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #3
  Aug 26, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Tujifunze kenya wamebadili katiba... Taifa lina furaha, taifa limevunja mgawanyiko, taifa linakwenda mbele

  Katiba ndio chanzo cha matatizo
   
 4. M

  Mutu JF-Expert Member

  #4
  Aug 26, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mashtaka hapa yanatikiwa kwenda api,mahakamani au wapi?tuache kusema tutende accordingly
   
 5. Bramo

  Bramo JF Bronze Member

  #5
  Aug 26, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 9,452
  Likes Received: 2,502
  Trophy Points: 280
  My Take:
  CCM Ndo wanatumia kivuli cha urais wa JK kuvunja sheria za gharama za uchaguzi,Tendwa kakaa kimyaaa,Werema Kakaaa Kimyaa,Jugde Makame kakaa kimyaaa
  CCM wnataka ktupeleka wapi?
  SAY NO TO CCM,SAY NO JK
   
 6. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #6
  Aug 26, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Kila kitu kina mwisho, mgombea mwenyewe ana wasaidizi kibao=bodyguards+wa kumdaga asijibwage chini.
   
 7. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #7
  Aug 26, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Bora ya JK aliyeanguka mkutanoni mbele ya umma,kuliko yule Padre aliyeanguka bafuni peke yake na kuvunja mkono,jiulize swali 'Je alikuwa anafanya mchezo gani bafuni hadi ukamzidia na kudondoka chini pwaaaa,mkono geju!'Nahua jibu unalo ila kwa hila hutozungumza.
  Sema ndio palipo ndio na Sio pasipo Sio.
   
 8. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #8
  Aug 26, 2010
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nafikiri kesi ifunguliwe dhidi ya shauri hili na wahusika wote wawekwe korokorini
   
 9. Joel

  Joel JF-Expert Member

  #9
  Aug 26, 2010
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 908
  Likes Received: 259
  Trophy Points: 80
  kwa kweli kila kitu kina mwisho kama Tendwa haoni, makame haoni, werema haoni, wajue dhahiri Mungu anaona na analipa hapa hapa Duniani.
   
 10. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #10
  Aug 26, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Halafu NEC ya L. Makame inajifanya bubu, kipofu, kiziwi. Kwa nini angalau isitoe tamko kali kukemea hili? Mr Makame, you and your institution are not independent, you are obnoxiously pro-CCM!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Oh yes you are!!!!!
   
 11. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #11
  Aug 26, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Aiseee uanamaana ataanguka tena?
   
 12. N

  Nanu JF-Expert Member

  #12
  Aug 26, 2010
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  it is difficult to differentiate between the ruling party and the govt especially on the not transparent governance. someone should be highly ethical in order to be able to put the dividing line.
   
 13. Epason

  Epason JF-Expert Member

  #13
  Aug 26, 2010
  Joined: Nov 9, 2009
  Messages: 427
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Nafikiri na wapinzani wawekewe utaratibu wa kutumia magari, watumishi wa serikali(eg madereva etc) kwenye kampeni kwa ratiba maalum, pia wajumuishe gharama hizo kwenye gharama za kampeni. IPO complex, inamaana amtumie mlinzi wa chama chake

  Sijui sheria hapa inasemaje
   
 14. MTWA

  MTWA JF-Expert Member

  #14
  Aug 26, 2010
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 1,024
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Mambo mabaya ndani ya hizi sheria ni zaidi ya haya tunayojadili. CCM inavunja kila sheria sasa maana hili la kubadili namba na kuwa za bandia linafanyika na vyombo vya sheria navyo vipo kimya. Halafu watafanya nini wakati mgombea bado ana madaraka yake ya urais kama kawa.
  Katiba zetu Africa lazima zibainishe mambo haya.
  ndo maana huwa hawakubali kushindwa au wanashinda kwa kishindo kwa sababu wanatumia nguvu zetu kufanya compaign.
   
 15. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #15
  Aug 26, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,171
  Likes Received: 5,594
  Trophy Points: 280
  Magari ya serikali yapamba kampeni za CCM Send to a friend Thursday, 26 August 2010 06:57

  [​IMG]Frederick Katulanda, Mwanza na Sadick MtulyLICHA ya sheria na kanuni za Uchaguzi kuzuia matumizi ya magari ya serikali, msafara wa mgombea urais wa CCM Jakaya Kikwete umetumia magari kadhaa ya serikali katika mikoa ya Mwanza, Geita na Kagera.

  Mbali na magari hayo, wakuu wa wilaya waliokuwa wameshiriki msafara wa mwenyekiti huyo wa CCM, walitumia magari yao ya kazi yakiwa yamewekwa namba binafsi huku wakivalia sare za chama hicho.

  Ukiondoa magari maalumu ya walinzi wa mgombea huyo ambaye pia ni rais, magari mengine ya wakuu wa wilaya na wakuu wa idara mbalimbali za serikali, yalitumika na kuwekwa namba binafsi.

  Kwa mujibu wa habari tulizozipata kutoka vyanzo vyetu zinaeleza kuwa hivi sasa Ikulu ya Dar es Salaam ina upungufu kwa kuwa wafanyakazi wa Ikulu hasa madereva pamoja na wapishi na wagawa vinywaji (waandazi), wanatumika katika kampeni za Rais Kikwete.

  Wapishi na waandazi hao wamepelekwa mikoani kulingana na ziara za kampeni.

  “Cha ajabu ni kuwa baadhi ya wafanyakazi wa Ikulu hasa madereva, wapishi na waandazi wanatumika katika kampeni za CCM kupitia Rais Kikwete.

  “Wamegawanywa katika mikoa tofauti kulingana na ratiba za ziara za kampeni za rais,’’ kilisema chanzo chetu.

  Juzi jijini Mwanza Mkuu wa wilaya Ilemela, Serenge Mrengo ambaye alifika majira ya saa 4:35 asubuhi uwanja wa ndege na gari lenye namba za STK 3551 huku wote wawili na dereva wake wakiwa wamevalia sare za CCM, lakini baada ya kusalimiana na viongozi wenzake, aliondoka.

  Akiwa wilayani Geita, Mkuu wa wilaya hiyo Philemon Shelutete alitumia gari lake la serikali ambalo lilikuwa limebandikwa namba T 804 BCZ huku akiwa amevalia sare za CCM. Pia gari la Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Benson Katala lilitolewa namba za serikali na kubandikwa namba T 180 BKW.

  Mkuu wa mkoa wa Mwanza Abbas Kandoro alitetea hatua hiyo akisema sio kosa kwa kuwa Kikwete bado ni rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanania.

  Kandoro, alikiri kutumika kwa magari hayo ya serikali na kusema kuwa viongozi hao waliyatumia kumpokea na baadhi yao waliambatana naye katika ziara hiyo kwa kuwa mbali na kuwa mgombea wa CCM pia anayo hadhi ya urais.

  “Huyu ni Rais, amekuja kama kiongozi licha ya kwamba anagombea, bado hajavuliwa urais, sasa ma-DC walikuja kama viongozi wa serikali kumpokea rais. Kama kuna mkuu wa wilaya alivaa shati la CCM alivaa kwa sababu ya mapenzi yake kwa chama,” alifafanua Kandoro ambaye alitumia gari binafsi la kiongozi mmoja wa CCM Kanda ya Ziwa.

  "Makosa ni kiongozi wa serikali kufanya kazi za chama na sioni kama kuna kiongozi wa serikali ambaye alifanya kazi za chama,"alisema

  Msafara wa Kikwete kuambatana na magari ya serikali haukuishia Mwanza na Geita pekee bali pia hata mkoani Kagera ambako magari mengi yalikuwa na namba za STK.

  Katika hatua nyingine, uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Bugando umetoa ufafanuzi kwamba uamuzi wake wa kutoa gari la kubebea wagonjwa katika msafara wa mgombea urais wa CCM kuhakikisha usalama wa mgombea huyo.

  Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Dk Charles Majinge alisema kwa kawaida jukumu la kutoa magari huwa lipo mikononi mwa uongozi wa mkoa ambao uliomba gari kwao na wao waliamua kutoa gari hilo la wagonjwa namba T 848 AWN.

  “Sisi hatutoi ambulance kwa wagombea, ila tulitoa kwa Kikwete kutokana na kuwa ni kiongozi wa nchi. Kutoa magari huwa ni kazi ya uongozi wa mkoa, lakini sisi kama watalaamu wa matibabu tulichukua tahadhari na kuweka gari hilo,” alieleza Dk Majinge.

  Alisema kwa vile akiwa jijini Mwanza aliwahi kuanguka, basi waliamua kuchukua tahadhari kuepuka kukosa huduma haraka iwapo jambo hilo lingejirudia akiwa mbali na hospitali ya rufaa.

  Akizungumzia gari hilo, Kandoro alisema uwapo wake ni utaratibu wa kawaida katika misafara ya viongozi wa serikali.

  “Huu ni utaratibu wa kawaida katika misafara ya viongozi, tumetoa kama utaratibu wa kawaida….unajua huyu ni kiongozi wa nchi, sasa unataka wakija na wagombea wengine wa upinzani nao tuwapatie magari ya wagonjwa, wao ni akina nani?” alieleza na kuhoji Kandoro ambaye pia aligombea kura za maoni kuwania kuteuliwa na CCM kuwa mgombea ubunge Jimbo la Kalenga na kushindwa.

  Akizungumza kwa sharti la kutotaja jina gazetini mmoja wa viongozi ambao walikuwa wakishughulika na kuratibu msafara huo alieleza kuwa gari hilo la wagonjwa ni lile ambalo lilitolewa na serikali ya Ujerumani chini ya ushirikiano wa Jiji la Mwanza na Wurzburg.

  “Gari hili liliandaliwa kutokana na maofisa wa usalama kuliomba na hili agizo limetolewa katika mikoa yote ambako atafika, kwani katika kampeni anakuwa amekwenda hadi katika wilaya ambazo haina hospitali na ikitokea dharura akimbizwe haraka hospitali huku akiendelea kupatiwa matibabu” alieleza kiongozi huyo wa chama.

  Hata hivyo, alisema gari hilo wao kama chama hawakuambiwa wala kuelekezwa kulilipia kwa vile ofisi ya mkoa ilisema watachukua wao katika hospitali ya Bugando, baada ya kuwasiliana na ofisi ya mganga mkuu wa mk
   
 16. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #16
  Aug 26, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hata kama alikuwa na mkewe, kwani tatizo liko wapi?
   
 17. Bramo

  Bramo JF Bronze Member

  #17
  Aug 27, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 9,452
  Likes Received: 2,502
  Trophy Points: 280
  Hiv wewe ni wa kike au ????Hoja zako zimekaa ki Changu changu kabisa yan,kama sio Punga
   
Loading...