Magari ya serikali na matumizi ya hovyo

Kwa Uzi mzuri ivi siwezi ongezea neno , nitachafua. Kuna mahala umesema ukweli uliopitiliza. Kama kwenye magari kwenda starehe na gesti bubu. Mfano izi v8 dar ndio usiseme, night club unakuta v8 tena STK, zingine tinted alaf linanguruma silence kama masaa2 ...imagine!! Na kodi tunalipa sisi.
Hata izi stl na STK na dfp sana sana new model za rav4 , ivi gesti, chochoro za mitaani, disco na night club huwa zinawafuata mabosi uku?
Sichangii huu uzi....nitaharibu!!
 
TRUE SCENARIO: Bosi anakaa Salasala, gari ni Cruiser V8 Turbo direct injection engine 4.2. Derva anaishi Buza kwa lulenge. Kila siku kumfuata bosi tu na kumrudisha bado shughuli za nyumbani mtoto shule,mama shopping,harusi vicoba.meetings ni feha nyingi.sana zetu walipa kodi zinateketea. Suluhu ni kwanini hawa watu wasipewe Rav 4 na wajiendeshe wenyewe mpaka ofisini wakifika ndio madereva washike hatamu
 
Pia Ikiwa Tunasema SERIKALI Inahitaji Kupunguza Na Kubana MATUMIZI Yake Na KUONGEZA Nguvu Ktk Maendeleo, Basi Iachane Na Manunuzi Ya Ma VX Kwa MATUMIZI Ya MAWAZIRI Na MAAFISA Wake!! Otherwise Ni Vichekesho Tu!! Maana Hayo Magari Ni Gharama Kubwa Kuyanunua, Kuyatumia, Kuyafanyia Service Na Mafuta!!
 
Gharama halisi zinazotumia kuendeshea magari ya serikali ni pungufu ya asilimia 20% gharama zilizobaki ni ufisadi wa kodi za wananchi
 
Atakujibu rais anaishi ofisini yani ikulu....ah ah ah

Rais siyo lazima aishi ikulu, Marehemu Nyerere makazi yake yalikuwa nje ya ikulu, zipo gharama za usafiri za kumleta ofisini na kumrudisha nyumbani. Rais aliyepo anaweza akahamia kwenye makazi yake nje ya ikulu pia.
 
Katika eneo ambalo serikali inapoteza pesa nyingi za walipa kodi ni katika kuhudumia magari yake. Imekuwa ni jambo la kawaida sana kwa mawaziri, manaibu waziri, makatibu wakuu, wakuu wa mikoa/wilaya na wakurugenzi wa idara wanapoteuliwa kushika nafasi hizo, familia zao nao wanakuwa ni sehemu ya cheo cha waziri.

Wanakuwa na magari ya kuhudumia familia, kupeleka na kuchukua watoto shuleni, kumchukua mama nyumbani na kumpeleka kazini kwake, gari kumchukua mtumishi wa nyumbani kwenda sokoni, na gari la serikali kutumika kwenda kwenye starehe usiku.

Kuna mapungufu makubwa kwenye usimamizi wa magari ya serikali, eneo pekee la serikali ambalo usimamizi wa magari upo vizuri kiasi ni Jeshi la Wananchi (JWZT), juhudi za serikali kukusanya kodi ziende sambamba na kuzuia maeneo yaliyokosa usimamizi makini, ili kuzuia matumizi ya hovyo ya magari ya serikali kama yanavyotumiwa sasa hivi.

Napendekeza serikali kuchukua hatua hizi kusimamia na kudhibiti matumizi ya magari yake.

1. Magari yote ya serikali yawe kwenye eneo la maegesho ya gari kuanzia saa 9 wakati muda wa kazi unapofika, isipokuwa magari yaliyo kwenye shughuli maalum. Iwe ni kosa kwa gari la serikali kukutwa limelazwa mitaani kama ilivyo kwa magari ya JWTZ. Dereva wa gari anatakiwa kufika ofisini asubuhi na kusubiri apangiwe kazi za kufanya. Sasa hivi gari linampeleka afisa Bunju, dereva anaishi Mbagala, anaondoka na gari na kuilaza Mbagala, asubuhi anaondoka Mbagala anamfuata afisa Bunju na kumpeleka ofisi mjini, kwa maana rahisi safari za gari hiyo jioni na asubuhi ni umbali wa kwenda Morogoro kutoka Dar es Salaam.

2. Wanaoruhusiwa kutumia magari ya serikali kupelekwa na kuchukuliwa nyumbani ni Rais/Makamu, Waziri Mkuu, Mawaziri, Manaibu, Katibu mkuu, Mkuu wa majeshi, Jaji Mkuu, Spika wengine watumie usafiri wao binafsi, daladala, bajaji, baiskeli n.k.

3. Serikali isimamishe manunuzi ya magari kwa muda, magari yaliyokuwa yanatumiwa kuhudumia familia yapelekwe maeneo yenye upungufu wa magari hasa wilayani.

4. Zipo safari za viongozi ni mzigo kwelikweli kwa serikali, utakuta kiongozi ana mkutano Arusha wa siku moja anapanda ndege kwenda Arusha, lakini utakuta dereva alishatangulia kwa gari, huyu kiongozi anatumia gari kwa masaa machache anapanda tena ndege anarudi Dar es Salaam, dereva naye anangurumisha tena gari kurudi haya ni majipu ya kutumbuliwa haraka.

Inasokitisha sana kwanza madereva wamejigeuza ndio mabosi,haya magari ilitakiwa siku ambazo sio za kazi nayo wayapark ofisini lakini chaajabu yako busy kama ni ya mtu binafsi,yaan unakuta gari ni ya office inakaa mtaa ambao kuna watu wa ofisini lakini dereva anadrive peke yake
 
Kama serikali kama inataka kupunguza gharama za magari ingeiga mfumo wa JWTZ, huwezi kukuta gari zao zimelazwa mitaani.
 
Mengine ni sawa na baadhi umeyakuza mno: nakubali kupunguza matumizi ya magari lakini baada ya serikali kukopesha watumishi magari kama wabunge....vinginevyo haitawezekana
 
Mleta mada nakupongeza kwa mada nzuri
Serilali ina matumizi makubwa yasiyo na ulazima, magari mengi ya fahari,
Serikali ibadilike ibane matumizi gari la serikali ni kwa matumizi ya serikali sio usiku unalikuta mitaani kwenye shuhuli haihusiani na serikali,
Raisi tunakuomba uwabane watendaji wako na wao watawabana walio chini yao, otherwise utamaliza muda wako wa miaka mitano kutumbua majibu yatakayojitokeza kila leo,
 
Kweli Kabisa Mkuu, Yaani Siku Kama Hizi Za Mapumziko Ya Sikukuu, Lkn Unakutana Na Magari Ya SERIKALI Mitaani KIBAO, Tena Usiku!! Sasa Swali La Kujiuliza Hayo Mafuta Wanayoyachoma Yananunuliwa Na Nani, Kama Ni SERIKALI, Je MATUMIZI Hayo Ni Kwa Faida Ya Nani!!!!??? Maana Ni KODI Zetu, So Lazima TUJUZANE!!!
 
Mengine ni sawa na baadhi umeyakuza mno: nakubali kupunguza matumizi ya magari lakini baada ya serikali kukopesha watumishi magari kama wabunge....vinginevyo haitawezekana

Mabasi yaendayo kasi yatawasadia kuwahi ofisini, magari ya serikali yabaki ofisini kwa kazi za serikali tu.
 
Mkakati wa kuzibiti matumizi ya hovyo ya magari ya serikali kuanza muda wowote
 
kwa serikali makini duniani huwa hawawanunulii viongozi wao magari bali wanakodisha kama serikali ikitumia huduma ya kukodisha magari itaokoa pesa nyingi sana ingawa najua pia ajira za ndugu zetu madereva zitapotea.Hata kama wakilipa laki 2 kwa siku lakini hizo gari hazitatumika siku za jumapili na siku nyingine zisizo na kazi wala hawatawajibika kwa wizi wa mafuta au magari kutumika nje ya muda wa kazi kwani kila afisa atatakiwa kusaini muda aliorudisha gari na kama atasaini amerudisha nje ya muda wa kazi atatkiwa kueleza alikuwa anafanya nini
 
Katika eneo ambalo serikali inapoteza pesa nyingi za walipa kodi ni katika kuhudumia magari yake. Imekuwa ni jambo la kawaida sana kwa mawaziri, manaibu waziri, makatibu wakuu, wakuu wa mikoa/wilaya na wakurugenzi wa idara wanapoteuliwa kushika nafasi hizo, familia zao nao wanakuwa ni sehemu ya cheo cha waziri.

Wanakuwa na magari ya kuhudumia familia, kupeleka na kuchukua watoto shuleni, kumchukua mama nyumbani na kumpeleka kazini kwake, gari kumchukua mtumishi wa nyumbani kwenda sokoni, na gari la serikali kutumika kwenda kwenye starehe usiku.

Kuna mapungufu makubwa kwenye usimamizi wa magari ya serikali, eneo pekee la serikali ambalo usimamizi wa magari upo vizuri kiasi ni Jeshi la Wananchi (JWZT), juhudi za serikali kukusanya kodi ziende sambamba na kuzuia maeneo yaliyokosa usimamizi makini, ili kuzuia matumizi ya hovyo ya magari ya serikali kama yanavyotumiwa sasa hivi.

Napendekeza serikali kuchukua hatua hizi kusimamia na kudhibiti matumizi ya magari yake.

1. Magari yote ya serikali yawe kwenye eneo la maegesho ya gari kuanzia saa 9 wakati muda wa kazi unapofika, isipokuwa magari yaliyo kwenye shughuli maalum. Iwe ni kosa kwa gari la serikali kukutwa limelazwa mitaani kama ilivyo kwa magari ya JWTZ. Dereva wa gari anatakiwa kufika ofisini asubuhi na kusubiri apangiwe kazi za kufanya. Sasa hivi gari linampeleka afisa Bunju, dereva anaishi Mbagala, anaondoka na gari na kuilaza Mbagala, asubuhi anaondoka Mbagala anamfuata afisa Bunju na kumpeleka ofisi mjini, kwa maana rahisi safari za gari hiyo jioni na asubuhi ni umbali wa kwenda Morogoro kutoka Dar es Salaam.

2. Wanaoruhusiwa kutumia magari ya serikali kupelekwa na kuchukuliwa nyumbani ni Rais/Makamu, Waziri Mkuu, Mawaziri, Manaibu, Katibu mkuu, Mkuu wa majeshi, Jaji Mkuu, Spika wengine watumie usafiri wao binafsi, daladala, bajaji, baiskeli n.k.

3. Serikali isimamishe manunuzi ya magari kwa muda, magari yaliyokuwa yanatumiwa kuhudumia familia yapelekwe maeneo yenye upungufu wa magari hasa wilayani.

4. Zipo safari za viongozi ni mzigo kwelikweli kwa serikali, utakuta kiongozi ana mkutano Arusha wa siku moja anapanda ndege kwenda Arusha, lakini utakuta dereva alishatangulia kwa gari, huyu kiongozi anatumia gari kwa masaa machache anapanda tena ndege anarudi Dar es Salaam, dereva naye anangurumisha tena gari kurudi haya ni majipu ya kutumbuliwa haraka.
Mkuu huu Uzi kama alivyandika mdau mmoja kuwa hachangii maana umemaliza kila kitu ni kweli kabisa. Nami nasema walau ningekua na pesa ningelipia ITV airtime ya masaa 4 tufanye mjadala wa kitaifa juu ya ubadhirifu huu.

Serikali kupitia fedha za walala hoi (walipa kodi ) hapa kwenye magari ya the so called viongozi na maofisa wa serikali kuna mamilioni ya fedha zinazofujwa.

Ufujaji umejikita katika matumizi mabaya ya nafasi zao juu ya vyombo hivyo vya usafiri walivyopewa , aidha afisa/kamishina/mkurugenzi/naibu/katibu mkuu/naibu waziri/waziri mmoja ana magari zaidi ya moja kwa matumizi yaliyoainishwa kwenye hoja mbalimbali humu. Na mengine yana namba zaidi ya moja.

Siku mmoja kule old terminal nilikua nasafiri kwa hizi ndege ndogo na wakati naingia airport nilitangulizana na gari ya waziri (jina nalihifadhi) aliposhuka na kuingia ndani dereva akatoa plate number ikabaki number ya kawaida kama zetu hizi ambao sijui ndio utaratibu au ni figisifigisi.

Ukienda mawizarani na kwenye taasisi za umma hao makanishina kwa kushirikiana na madereva wao wanafoji service, matairi na spare parts kubwa kubwa kuwa zimenunuliwa wakati hamna kilichofanyika na kujipatia fedha.

Kama rais ana nia ya kweli kama anavyodai/anavyofanya kule kwa yule wa vitambulisho vya uraia against voters card, ukwepaji kodi, mishahara ya 35mil , vikao vya board nje ya nchi au kwenye 5star hotel, airticket daraja la mabwenyenye na kadharika hili la magari ya serikali ni DONDA NDUGU na kuna millions of tax payers that can be served and be used somewhere else meaningful/wisely .

Naomba kuwasilisha
 
Back
Top Bottom