Magari ya serikali na matumizi ya hovyo

Asante

JF-Expert Member
Dec 18, 2009
2,086
1,081
Katika eneo ambalo serikali inapoteza pesa nyingi za walipa kodi ni katika kuhudumia magari yake. Imekuwa ni jambo la kawaida sana kwa mawaziri, manaibu waziri, makatibu wakuu, wakuu wa mikoa/wilaya na wakurugenzi wa idara wanapoteuliwa kushika nafasi hizo, familia zao nao wanakuwa ni sehemu ya cheo cha waziri.

Wanakuwa na magari ya kuhudumia familia, kupeleka na kuchukua watoto shuleni, kumchukua mama nyumbani na kumpeleka kazini kwake, gari kumchukua mtumishi wa nyumbani kwenda sokoni, na gari la serikali kutumika kwenda kwenye starehe usiku.

Kuna mapungufu makubwa kwenye usimamizi wa magari ya serikali, eneo pekee la serikali ambalo usimamizi wa magari upo vizuri kiasi ni Jeshi la Wananchi (JWZT), juhudi za serikali kukusanya kodi ziende sambamba na kuzuia maeneo yaliyokosa usimamizi makini, ili kuzuia matumizi ya hovyo ya magari ya serikali kama yanavyotumiwa sasa hivi.

Napendekeza serikali kuchukua hatua hizi kusimamia na kudhibiti matumizi ya magari yake.

1. Magari yote ya serikali yawe kwenye eneo la maegesho ya gari kuanzia saa 9 wakati muda wa kazi unapofika, isipokuwa magari yaliyo kwenye shughuli maalum. Iwe ni kosa kwa gari la serikali kukutwa limelazwa mitaani kama ilivyo kwa magari ya JWTZ. Dereva wa gari anatakiwa kufika ofisini asubuhi na kusubiri apangiwe kazi za kufanya. Sasa hivi gari linampeleka afisa Bunju, dereva anaishi Mbagala, anaondoka na gari na kuilaza Mbagala, asubuhi anaondoka Mbagala anamfuata afisa Bunju na kumpeleka ofisi mjini, kwa maana rahisi safari za gari hiyo jioni na asubuhi ni umbali wa kwenda Morogoro kutoka Dar es Salaam.

2. Wanaoruhusiwa kutumia magari ya serikali kupelekwa na kuchukuliwa nyumbani ni Rais/Makamu, Waziri Mkuu, Mawaziri, Manaibu, Katibu mkuu, Mkuu wa majeshi, Jaji Mkuu, Spika wengine watumie usafiri wao binafsi, daladala, bajaji, baiskeli n.k.

3. Serikali isimamishe manunuzi ya magari kwa muda, magari yaliyokuwa yanatumiwa kuhudumia familia yapelekwe maeneo yenye upungufu wa magari hasa wilayani.

4. Zipo safari za viongozi ni mzigo kwelikweli kwa serikali, utakuta kiongozi ana mkutano Arusha wa siku moja anapanda ndege kwenda Arusha, lakini utakuta dereva alishatangulia kwa gari, huyu kiongozi anatumia gari kwa masaa machache anapanda tena ndege anarudi Dar es Salaam, dereva naye anangurumisha tena gari kurudi haya ni majipu ya kutumbuliwa haraka.
 
Kwahiyo Wakurugenzi na wakuu wa Idara Wizarani, wakuu wa Taasisi za umma kama TRA, TANROADS, BOT, TIC, SUMATRA etc etc Wakurugenzi wa majiji, Manispaa, miji na wilaya nk nk watembee kwa bajaji kwenda kazini italeta tija? Hapo hujaongelea vyombo vya ulinzi na usalama.

vinginevyo wakopeshwe magari kama wabunge.
 
Katika eneo ambalo serikali inapoteza pesa nyingi za walipa kodi ni katika kuhudumia magari yake. Imekuwa ni jambo la kawaida sana kwa mawaziri, manaibu waziri, makatibu wakuu, wakuu wa mikoa/wilaya na wakurugenzi wa idara wanapoteuliwa kushika nafasi hizo, familia zao nao wanakuwa ni sehemu ya cheo cha waziri. Wanakuwa na magari ya kuhudumia familia, kupeleka na kuchukua watoto shuleni, kumchukua mama nyumbani na kumpeleka kazini kwake, gari kumchukua mtumishi wa nyumbani kwenda sokoni, na gari la serikali kutumika kwenda kwenye starehe usiku.

Kuna mapungufu makubwa kwenye usimamizi wa magari ya serikali, eneo pekee la serikali ambalo usimamizi wa magari upo vizuri kiasi ni Jeshi la Wananchi (JWZT), juhudi za serikali kukusanya kodi ziende sambamba na kuzuia maeneo yaliyokosa usimamizi makini, ili kuzuia matumizi ya hovyo ya magari ya serikali kama yanavyotumiwa sasa hivi.

Napendekeza serikali kuchukua hatua hizi kusimamia na kudhibiti matumizi ya magari yake.

1. Magari yote ya serikali yawe kwenye eneo la maegesho ya gari kuanzia saa 9 wakati muda wa kazi unapofika, isipokuwa magari yaliyo kwenye shughuli maalum. Iwe ni kosa kwa gari la serikali kukutwa limelazwa mitaani kama ilivyo kwa magari ya JWTZ. Dereva wa gari anatakiwa kufika ofisini asubuhi na kusubiri apangiwe kazi za kufanya. Sasa hivi gari linampeleka afisa Bunju, dereva anaishi Mbagala, anaondoka na gari na kuilaza Mbagala, asubuhi anaondoka Mbagala anamfuata afisa Bunju na kumpeleka ofisi mjini, kwa maana rahisi safari za gari hiyo jioni na asubuhi ni umbali wa kwenda Morogoro kutoka Dar es Salaam.

2. Wanaoruhusiwa kutumia magari ya serikali kupelekwa na kuchukuliwa nyumbani ni Rais/Makamu, Waziri Mkuu, Mawaziri, Manaibu, Katibu mkuu, Mkuu wa majeshi, Jaji Mkuu, Spika wengine watumie usafiri wao binafsi, daladala, bajaji, baiskeli n.k.

3. Serikali isimamishe manunuzi ya magari kwa muda, magari yaliyokuwa yanatumiwa kuhudumia familia yapelekwe maeneo yenye upungufu wa magari hasa wilayani.

4. Zipo safari za viongozi ni mzigo kwelikweli kwa serikali, utakuta kiongozi ana mkutano Arusha wa siku moja anapanda ndege kwenda Arusha, lakini utakuta dereva alishatangulia kwa gari, huyu kiongozi anatumia gari kwa masaa machache anapanda tena ndege anarudi Dar es Salaam, dereva naye anangurumisha tena gari kurudi haya ni majipu ya kutumbuliwa haraka.
 
Kwahiyo Wakurugenzi na wakuu wa Idara Wizarani, wakuu wa Taasisi za umma kama TRA, TANROADS, BOT, TIC, SUMATRA etc etc Wakurugenzi wa majiji, Manispaa, miji na wilaya nk nk watembee kwa bajaji kwenda kazini italeta tija? Hapo hujaongelea vyombo vya ulinzi na usalama.

vinginevyo wakopeshwe magari kama wabunge.

Watumie magari yao binafsi wakiwa maofisini watumie magari ya ofisi kwa kazi za ofisi tu. Kumbuka wana fursa ya kipekee kwa watumishi wa ofisi za serikali na mashirika ya uma wanatoa dhamana ya kupata mikopo bank kitu ambacho ni shida kidogo kwa kampuni na watu binafsi.
 
Watumishi wote wa serikali wanakopesheka bila tatizo lolote na mabenki yote kwa kugombewa mradi tu asiwe na mkopo mwingine.
 
Hiyo mikopo tunajengea nyumba na kuweka vibishara vya kusupplement mishahara finyu ya serikali. Hata nikinunua gari hela ya mafuta mwezi mzima nitaitoa wapi mshahara huu? Nikipanda daladala nitachelewa kisha mnaotaka huduma mtaanza kulalamika. Wacheni tu tujiachie kwa STK maana hakuna namna sasa.
 
mm bosi wangu anaishi mbweni na mm gongo la mboto na lazima nifumfuate nyumbani kila siku asubuhi ndio twende mjini ofisini mjini(posta)
 
Hiyo mikopo tunajengea nyumba na kuweka vibishara vya kusupplement mishahara finyu ya serikali. Hata nikinunua gari hela ya mafuta mwezi mzima nitaitoa wapi mshahara huu? Nikipanda daladala nitachelewa kisha mnaotaka huduma mtaanza kulalamika. Wacheni tu tujiachie kwa STK maana hakuna namna sasa.

Ni bora serikali ikawalipa watumishi wengine wanaositahili fuel allowance kuliko kuendelea kuruhusu matumizi ya hovyo ya magari yake.
 
mm bosi wangu anaishi mbweni na mm gongo la mboto na lazima nifumfuate nyumbani kila siku asubuhi ndio twende mjini ofisini

Kuna umbali gani kutoka Gongo la Mboto hadi Mbweni kwa safari isiyokuwa na tija kwa serikali?
 
Du rais naye achukuliwe na kurudishwa nyumbani upo serious kweli muleta hoja?
 
Back
Top Bottom