Magari ya mwendo kasi: kufanya Kazi kwa mazoea

Mama Mdogo

JF-Expert Member
Nov 21, 2007
2,967
2,147
Niko jijini tangu juzi. Leo nimejihimu tangu saa 12 asubuhi kuwahi bus la mwendo kasi hapa kimara. Nimekuta kituo kimejaa sana, abiria wamefika tangu saa 11. Ajabu bus la kwanza limekuja saa 12:15. Naona hawa viongozi wa DART/BRT hawajui maana ya demand and supply. Ushauri wa bure, badilikeni.
 
Asante kwa mada, pia kuna tatizo lingine la madereva wengi wa hayo mabasi KUKARIRI kuwa kila mtu anaenda mjini.
1. Ukiwa kituo cha kona na unaelekea kimara, mabasi mengi hayasimami haya uyapungie mkono kwa kigezo kuwa hawataki ukageuze na gari.
2. Unapanda basi ila vitufe havifanyi kazi, dereva anasema anashusha kila kituo ila unashangaa anakupitiliza kituo chako.
Ni kero sana.
 
Niko jijini tangu juzi. Leo nimejihimu tangu saa 12 asubuhi kuwahi bus la mwendo kasi hapa kimara. Nimekuta kituo kimejaa sana, abiria wamefika tangu saa 11. Ajabu bus la kwanza limekuja saa 12:15. Naona hawa viongozi wa DART/BRT hawajui maana ya demand and supply. Ushauri wa bure, badilikeni.
Imekuaje leo tena! Juzi juzi niliwaona barabarani alfajiri saa 4:50 tayari wakiwa kazini
 
Hayo ni matatizo ya kukosa mafunzo stahiki. Suala la fikra nchini liko chini sana. Bado tuna safari ndefu lakin tutafika tu. Poleni kwa hayo maswahibu mnayopitia
 
Back
Top Bottom