Magari ya kubebea wanafunzi ni janga la taifa

babalao 2

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
5,421
3,287
Wakuu poleni na Majukumu

Kwanza niwapongeze kwa kuendelea kuhabarishana na kuelimishana mambo mbalimbali ulimwenguni.

Hoja yangu ni juu ya hili tatizo la Usafiri kwa Wanafunzi, hasa shule binafsi ambapo ndipo hutumika zaidi magari kupeleka watoto shule.

Mosi Magari ni chakavu yasiyo na sifa ya kubeba Binadamu aliye hai kutokana na uchakavu mithili ya vyuma chakavu, na kwa hapa sijui kwanini askari wa barabarani wanayafumbia macho haya magari hebu tuamke tuokoe watoto wetu na janga hili.

Pili ni UJAZO wa hayo magari hauna kipimo maalumu, gari ya watu 30 itabebeshwa wanafunzi 90. Mfano ni Jana kwa trafic jijini Dar kukamata gari aina ya Noah 3 zenye uwezo wa kupakia watu 8 kila moja imebeba watoto 34 kila gari, je Wizara husika Hawalioni hili ama ni mpaka Yatokee Maafa ndo tuchukue hatua? Waziri Ndalichako Sema neno watoto wetu Wapone.

[IMG
4b97fb14bb8644c3d23cdbfa7990f031.jpg
][/IMG]
 
Mabasi Chakavu hilo ni kawaida na sijawahi kuona School bus ambalo ni jipya. Hii yote ni kupenda urahisi pindi wanunuapo hayo mabus.

Hilo la kujaza watoto kama nyanya kwenye tenga limeshakuwa ni tatizo na watu wa usalama barabarani wanaona lakini hatua hazichukuliwi.

Kikubwa waombee Uzima wasipatwe na janga lolote.
 
hiyo gari sio school bus ni mwananchi msamalia kaamua kuwapa lift watoto ..maana naona kuna uniform za ndalichako na za kina fulani....
 
Huyo jamaa atakuwa mtaalam na mzoefu wa kusafirisha wasomali si bure.Yule mama aliyekuwa mbele nae ni muuaji kabisa
 
Hilo la kujaza watoto kama nyanya kwenye tenga limeshakuwa ni tatizo na watu wa usalama barabarani wanaona lakini hatua hazichukuliwi

Wanasubiri waonekane kwenye igizo la kujifanya wanasikitika na kutoa kauli yao ya miaka yote "KUANZIA SASA HATUTAWAONEA AIBU WALA KUWAFUMBIA MACHO"
 
hiyo gari sio school bus ni mwananchi msamalia kaamua kuwapa lift watoto ..maana naona kuna uniform za ndalichako na za kina fulani....
Kuna mtu alingalia taharifa ya habari. Ni hivi, yani hiyo gari inafanya biashara ya kupitia watoto wa shule tofauti za mjini kuwapeleka na kuwachukua toka shule.

Unajua baadhi ya shule za katikati ya mji (kama si zote) hazina school bus. Unakuta watoto wa shule kama 4 wanatumia gari moja.

Swali je ni nanin ana coordinate hilo...nani wa kukamatwa...mzazi hajui hili? Shule haijui hili? Hao ni watoto wa shule za maeneo ya Upanga na Kisutu nasikia na wala si msaada ni biashara...labda ni cheap ...maswali ni mengi
 
Tatizo viongozi wengi wanamiliki au kuwa na Ubia kwenye hizo shule hivo hupelekea mgongano wa maslahi na utendaji wao.
 
Tutunze kumbukumbu hapa Jf tunalia na mambo mengi ila Yanafumbiwa Macho.
 
Leo imetukia Ajali tunasema ni Janga la Taifa ilihali hayo magari ndyo janga kuu
 
Wakuu poleni na Majukumu

Kwanza niwapongeze kwa kuendelea kuhabarishana na kuelimishana mambo mbalimbali ulimwenguni.

Hoja yangu ni juu ya hili tatizo la Usafiri kwa Wanafunzi, hasa shule binafsi ambapo ndipo hutumika zaidi magari kupeleka watoto shule.

Mosi Magari ni chakavu yasiyo na sifa ya kubeba Binadamu aliye hai kutokana na uchakavu mithili ya vyuma chakavu, na kwa hapa sijui kwanini askari wa barabarani wanayafumbia macho haya magari hebu tuamke tuokoe watoto wetu na janga hili.

Pili ni UJAZO wa hayo magari hauna kipimo maalumu, gari ya watu 30 itabebeshwa wanafunzi 90.
Mfano ni Jana kwa trafic jijini Dar kukamata gari aina ya Noah 3 zenye uwezo wa kupakia watu 8 kila moja imebeba watoto 34 kila gari, je Wizara husika Hawalioni hili ama ni mpaka Yatokee Maafa ndo tuchukue hatua? Waziri Ndalichako Sema neno watoto wetu Wapone.
[IMG
4b97fb14bb8644c3d23cdbfa7990f031.jpg
][/IMG]
MBONA MABASI YAKAWAIDA UNAPANDA NA YAMECHOKA TENA UNAPITIA DIRISHANI KUWAHI SITI
 
sitaki kabisa kuamini hawa watoto walikuwa kwenye boot ya noah, watakuwa walipozi tu wapigwe picha, kamanda sirro usipolitolea ufafanuzi hili hatukuelewi.
 
Kwakweli hili ni tatizo
Mfano ajali ya leo huko Karatu wanadai watoto waliofariki ni 31 pamoja na walimu wao na majeruhi ni wanne
Sasa swali hiyo Gari ilikuwa na abiria 35
Uliiangalia hiyo Gari si ajabu seating capacity yake ni 25psg sasa hao 10 walikaa wapi?
Je hawakupita kwenye vituo vya ukaguzi asubuhi ya leo?
Je kwanini hatua hazikuchukuliwa?
Nani awajibishwe?
Pia kuna tetesi kwamba dereva wa basi hilo alikuwa kondakta sijui lakini kikubwa hapa ni je huyo dereva alikuwa na leseni yenye madaraja yanayotakiwa kwa udereva wa basi la abiria(wanafunzi)?
 
tuchukue hatua kali kwa wamiliki wa shule kuwa amewekeza kwenye majengo pesa nyingi pia awekeze kwenye usafiri wa shule pesa nyingi kuokoa maisha ya watoto wengi .gari za shule ni mbovu hasa kwa kuwa ni gari zilifanya kazi za daladala na kuchoka ndio hupelekwa kubeba watoto wetu .sababu wanayotoa ni kuwa eti njia mbovu ,hatukatai ila zipo gari kwa ajili ya njia mbovu ,mfano canter zinahimili lakini lazima ziwe zimejengwa maalum kwa kazi hiyo ,wadau tuchukue hatua sasa tusingoje litokee balaa jingine ,
 
school bus zinahesabika ni private transport wengi wao wanakuwa na lesseni class D kimsingi hawana sifa za kubeba watoto wa shule,
 
tatizo ni mfumo wetu wa uongozi, bus aina ya tata jipya ni mil 100, shule gani itawekeza hapo?
Bus kama hili shule ngapi zina uwezo wa kununua?
124.jpg
 
school bus zinahesabika ni private transport wengi wao wanakuwa na lesseni class D kimsingi hawana sifa za kubeba watoto wa shule,
Kama ni hivyo basi sheria zetu pia bado zinamapungufu
Kwani abiria ni nani? kisheria
Ni tatizo kwakweli ina maana madereva wa mabasi ya shule hawana class C ?
Uwiiii Mungu wangu
 
Back
Top Bottom