Magari ya kubeba watoto wa shule

abdallahtase

Member
Aug 20, 2013
37
17
Habari zenu wana Jamvi....
Nimeleta mada hii mbele yenu kutokana na kero ninayoiona kwa shule za awali na Msingi ambazo zinaitwa " English Medium "
Na kero hii si nyingine bali ni UBOVU wa magari ya kusafirishia watoto kwenda shule na kutoza gharama kubwa katika huduma hiyo ya usafiri. wakati mwingine utakuta watoto wakichelewa kufika madarasani au kurudi nyumbani kwao kutokana na ubovu huo, Kurundikana watoto wengi ndani ya gari moja, kukaa muda mrefu vituoni wakisubiri magari hayo na tabia mbaya za madereva wanaoyaendesha magari hayo. kero hii inaweza kuwa sababu ya baadhi ya watoto kutokuwa na maendeleo mazuri kitaaluma.

Ninachotaka kusisitiza hapa ni wingi wa magari hayo mabovu kiasi kwamba kama mamlaka husika zimefumba macho mpaka tutakaposikia au kuona magari hayo yakisababisha maafa kwa watoto wetu wapendwa kutokana ubovu ndio waanze kuchukua hatua.
Nashauri wenye mammlaka kuangalia eneo hili kwa umakini mkubwa, kwa kuwa hayo magari hayafai kuwa barabarani, na madereva waoyaendesha magari hayo watazamwe tabia zao ili iwe sababu ya kuharibu watoto wetu.

Naomba kuwasilisha
 
Nahisi unaisema gari ya shule wanayosoma wanangu.

Tumeshasema tukachoka,na mmiliki wa shule badala alifanyie kazi tatizo anaweka vinyongo na wazazi wanaosema kuhusu ubovu wa school bus.
 
Back
Top Bottom