Magari ya Kijapan | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Magari ya Kijapan

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Anfaal, May 6, 2011.

 1. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #1
  May 6, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ukifika Tanzania magari mengi yanayoonekana barabarani kuanzia ya serikali hadi ya watu binafsi ni ya Kijapan. Ni vigumu saana kuelewa kwanini baadhi ya magari mengine hayapo kabisa au lipo mojamoja. Mfano zamani gari kama Peugeot zilikuwa nyingi lakini sasa hivi ni shida saana kuziona.

  Gari za FIAT pia nazo zinapungua, wengi na sijui kwanini tumekuwa tukipenda kuagiza magari ya Kijapan. Huenda wengi watajibu spea zake zinapatikana kwa urahisi.

  Zinapatikana kwa urahisi kwa sababu ndio magari yaliyojaa katika barabara zetu. Hapa sizungumzii ubora la hasha bali ni kuona namna tunavyokosa fursa ya kupata magari aina nyingine ambayo ni nafuu kuliko hayo ya Kijapan km Vauxhaul etc.

  Lengo la maandishi haya ni kutoa angalizo kwa wale ambao wanatarajia kuanzia magari kutoka Japan miezi kadhaa ijayo. Itakumbukwa kuwa Japan ilikumbwa na yale maafa makubwa na hivyo kusababisha uzalishaji kusuasua hasa wa parts na hivyo kupunguza uzalishaji wa magari kwa kiasi kikubwa, Japani kwenyewe na nchi nyinginezo.

  Kwa hiyo inamaana kuwa watu sasa hivi huenda wakanunua magari ya Kijapan kwa bei kubwa kwa sababu uzalishaji umepungua kwa kiasi kikubwa saana. Kwamaana hiyo wale wanaouza secondhand nao wataaamua kukaa nayo na hata wakisema wauze inamaana demand yake itakuwa kubwa na bei kubwa.

  Na pia pesa yako bado inanguvu saana na Tsh imeporomoka vilivyo.
  Hivyo kuna haja ya kufikiria brand zinyingine za magari hasa ambazo zimeshaanza kuonekana mjini.
   
 2. Mazingira

  Mazingira JF-Expert Member

  #2
  May 6, 2011
  Joined: May 31, 2009
  Messages: 1,837
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Mkuu hapa mtu si unafanya window shopping tu kwenye mtandao kisha unafahamu wapi waweza kupata gairi kwa bei rahisi? Wala haina shida kama unavyofikiria.
   
 3. Mkeshahoi

  Mkeshahoi JF-Expert Member

  #3
  May 6, 2011
  Joined: Jan 4, 2009
  Messages: 2,494
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  nahisi kuna mantiki flani katika usemayo.. nimeshuhudia hata katika miradi nyingi ya wafadhili hapa bongo... hela ya mwaka wa fedha wa 2011/2012 ni kama imepungua kwa sababu ya mtikisiko wa uchumi. nchi nyingi zajaribu kurejea kati uchumi imara... ni muhimu kawaza unapohitaji kununua vitu vya gharama toka nje kwakweli...
   
 4. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #4
  May 6, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  2kizungumzia mambo ya spear hakika kuna baadhi ya magari hapa Kwe2 ni mpk u2me ama Japan yenyewe ama kwa hawa jrn ze2 wa Kenya na haya yote yanasababishwa na ndg ze2 kuwa Mapapa kwenye vyanzo vya Mapato kwani unaweza2ma spear toka huko lkn ukifikisha zinakwamia bandari na kuwa uchafu kisa wanataka pesa mara dufu ya uliyonunua. Ukizingatia hata wao wenyewe wana magari ya si ajabu wakanunua baadae hizo spear lakini wanamind fedha balaa. Mi nilitaka kufanya hiyo biashara lakini baada ya kupata mahesabu hayo nikagairi kbs. Yani we acha2
   
 5. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #5
  May 6, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nadhani unahitaji kusoma tena nilichoandika. Vinginevyo utakuwa unafanya tu window shopping. Nimeandika kwa wale ambao wako cost sensitive na kuwashauri kufikiria wigo mwingine maana huko mbeleni huenda hawataweza hata kununua magari tena.
   
 6. Zinedine

  Zinedine JF-Expert Member

  #6
  May 8, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,189
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hapana mkuu, amejitahidi kuchangia hoja yako-usimuonee. Ukweli ni kwamba wengi wa wanaonunua magari wako sensitive kabla hawajanunua na ukweli utabaki kwamba hayo magari ya kijapani yanaendeshwa sana siyo Tz pekee-ni all-over Africa, Amerika kaskazini na kwingineko kwa kuwa yako durable, affordable na stable kwa mazingira yetu.

  Pia pamoja na tetemeko lililotokea kumbuka kwamba nchi zilizoendelea hususan Japan zina-intervene mno sekta zinazoimarisha uchumi wao ikiwa pamoja na sekta ya magari kwa japan.

  So serikali ya Japan imeshachukua hatua madhubuti kuakikisha kuwa sekta hiyo inaendelea kuwa world leading window shopping and buying.

  Magari ya Ulaya mengi yao yametengenezwa kufit environment ya ulaya na ghali mno kutokana na production cost ya kuzalisha gari ulaya kuliko Japan, China na India.

  Plz come again with concrete and constructive idea ya thread yako kwani pia ina nia njema kwa watanzania but-plz re-arrange as appropriate.
   
 7. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #7
  May 8, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Magari ya kijapani ni yepi hayo?
   
 8. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #8
  May 8, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Labda tutaje magari ya Kijapan ambayo ni common Tanzania. Kuna Honda, Toyota na NIssan. Haya ndio maarufu. Ya nchi nyingine kuna;, kuna BMW, benz, kuna audi, Lexus, Peugeot, Vauxhal, Landrover etc. Nikikurudisha nyuma. Utakumbuka miaka ya nyuma namna gari aina ya pijo na landrover zilivyokuwa zimejaa. Unataka kuniambia gari zile zilikuwa hazihimili mikikimikiki ya Tz? Pia fanya zoezi rahisi, hebu angalia bodi ya magari mengi ya Kijapan yanayotoka Ulaya na yale ya Japan moja kwa moja. Hoja ya kwamba serikali inaprotect sekta zake ni sahihi, lakini Japan sasa hivi kuna matatizo. Mfano Toyota wamesema uzalishaji wao utapungua kwa karibu 50% mwaka huu kwa kukosekana kwa parts na makampuni mengine pia ya huko yamesema hivyo. Financial report yao ya March imeonyesha sales imeshuka kwa 30%.
  Pia nadhani wewe ndio unahitaji kufanya research ya hii kitu. Ingia online angalia bei za magari wanayoyatumia Watanzania wengi kisha useme ya wapi ni ghali.
   
 9. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #9
  May 8, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,307
  Likes Received: 649
  Trophy Points: 280
  Mahindra zipo na ni brand new kwa chini ya m5 tena ei 4by4 so shaka ondoa.
   
 10. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #10
  May 8, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Mjihadhari na hayo magari ya Kijapan sasa, yasije kuwa na mihonzi hatari ya nyuklia mkasababisha maafa kwa ndugu, jamaa, marafiki na familia zenu.
   
Loading...