Magari ya kampeni ya JK yazuiwa Serengeti | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Magari ya kampeni ya JK yazuiwa Serengeti

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Wambugani, Sep 28, 2010.

 1. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #1
  Sep 28, 2010
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Katika tukio jingine, jana magari ya msafara wa Rais Kikwete yalizuiwa kupita katika hifadhi ya Serengeti kwa madai kuwa hayana kibali kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii.

  Magari manane likiwamo linalombeba Rais Kikwete lenye namba Toyota Land Cruiser namba T 979 BHS, yalizuiwa kwa saa nzima na maofisa wa hifadhi hiyo wakati yanataka kupita kwenda Mugumu yalipo Makao Makuu ya wilaya ya Serengeti.

  Magari hayo yalikuwa yametoka kumpeleka uwanja wa ndege wa Loliondo wilayani Ngorongoro baada ya kumaliza mkutano wake wa kwanza katika kijiji cha Loliondo, kata ya Orgorosok wilayani humo.

  Maofisa hao walisisitiza kuwa kama hawana kibali cha wizara wasingeruhusiwa kupita, vinginevyo wahusika wake walipe fedha kama ilivyo kwa watu wengine.

  Baada ya vuta nikuvute iliyodumu kwa takribani saa nzima, maofisa waliokuwa ndani ya magari hayo waliamua kuyalipia na watu waliokuwa katika msafara huo.

  Magari yote manane yalilipiwa jumla ya Sh. 8,000 na watu 27 waliokuwa katika magari hayo walilipiwa jumla ya Sh. 40,500, ikiwa ni wastani wa Sh.1,500 kwa kila mtu.

  Alipotafutwa ili atoe idhini magari hayo yapite, Mkuu wa Idara ya Utalii ndani ya hifadhi hiyo aliyefahamika kwa jina la Kimaro alisema hata kama ni ya Rais Kikwete, kama hayakuwa na kibali kutoka wizarani yasiruhusiwe kupita.

  “Nasema hata kama ni ya mgombea urais wa CCM yasipite bila kulipa kama hayana kibali cha wizara, maana Kikwete ni mgombea tu wa CCM hakikisheni wanalipa kama hawana kibali,” aliyasema hayo huku watu wote wakisikia kwani iliwekwa 'loud speaker' ili watu wote wasikie msimamo wa uongozi wa juu.

  Baada ya malipo kufanyika, magari hayo yaliendelea na safari kuelekea alipo mgombea huyo mwendo wa saa tatu na yalifika saa 12 Mugumu muda wa kampeni ukiwa umekwisha.

  Akizungumza na wakazi wa kata ya Orgorosok, Rais Kikwete serikali yake itahakikisha miaka mitatu ijayo hakutakuwa na shida ya walimu kwani itakuwa ikizalisha walimu 19,000 kila mwaka.

  Alisema atahakikisha kila sekondari ina maabara ya kisasa na zile za zamani zitaboreshwa ikiwa ni mkopo wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB).

  Aliwataka kutenganisha maeneo ya wakulima na wafugaji ili kuepuka migogoro baina yao mifugo inapokula mazao.

  Leo Rais Kikwete anatarajiwa kufanya kampeni zake katika wilaya za Musoma Vijijini, Bunda na Musoma Mjini.

  CHANZO: NIPASHE
  ___________________________________________________

  Wars are caused by undefended wealth - Ernest Hemingway
   
 2. Kudadeki

  Kudadeki JF-Expert Member

  #2
  Sep 28, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ingekuwa wakati wa dikteta maarufu, hiyo mamlaka nzima ya hifadhi ingefutiliwa mbali. :becky:
   
 3. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #3
  Sep 28, 2010
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145


  Huu ni mfano wa kuigwa. Hii inadhirisha wazi kwamba Watanzania sasa wameondokana na nidhamu ya woga na wanafanya kazi kama invyostahili kwa mujibu wa utaratibu wa kazi yao.


  ________________________________________________________

  Wars are caused by undefended wealth - Ernest Hemingway
   
 4. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #4
  Sep 28, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Mwandishi hajatajwa.
  naamini yupo kwenye kikwete 2010 press team
   
 5. F

  Froida JF-Expert Member

  #5
  Sep 28, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  SAFIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIi sana
   
 6. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #6
  Sep 28, 2010
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Gazeti la mwananchi limeandika Kikwete na msafara wake walikula nyama ya myumbu na pofu wakashiba kabisa!
   
 7. JOYCE PAUL

  JOYCE PAUL JF-Expert Member

  #7
  Sep 28, 2010
  Joined: Jan 8, 2010
  Messages: 1,007
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Katimizaza wajibu wake safi.
   
Loading...