kbm
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 5,224
- 1,687
Majiji mengi yaruhusiwa kuzuia matumizi ya magari ya dizeli ifikapo mwaka 2025.
Mameya kutoka miji minne mikubwa duniani wamesema watapiga marufuku magari na malori yanayotumia mafuta ya Diesel katika miji yao ifikapo mwaka 2025.
Viongozi hao kutoka miji ya Paris, Mexico City, Madrid na Athens wamesema wanataka kuhakikisha uwepo WA hewa safi.
Shirika la Afya duniani (WHO) linakadiria kwamba watu milioni tatu hufariki kila mwaka kutokana na hewa chafu duniani.
Azimio la mameya hao liliafikiwa kwenye kongamano la kimataifa nchini Mexico.
Wataalamu wa afya wanasema moshi unaotoka kwenye magari yanayotumia Diesel huingia kwa mapafu ya binadamu na kusababisha ugonjwa na kupumua na moyo.
Mameya hao wamesema wataweka magari mbadala yanayotumia umeme na nishati zingine.