Magari ya abiria mwisho Tegeta Nyuki na Kimara

Magari ya abiria mwisho Tegeta Nyuki na Kimara

Nimelisikia ili tangazo la SUMATRA kwenye redio kwamba magari yote ya abiria yanayotoka Bagamoyo yataishia Tegeta Nyuki, hayatofika Mwenge wala Makumbusho. Yale ya kutoka Mbezi yataishia Kimara hayatofika mjini kwa maana hiyo unatakiwa upande gari lingine ukifika Tegeta Nyuki au Kimara.

Ninachojiuliza, inakuwaje SUMATRA wanatoa utaratibu huu bila kutoa viwango vipya vya nauli? Kwa mfano ukitoka Bagamoyo unalipa 2,200 mpaka mjini. Je nauli itabaki hiyo hiyo mpaka Tegeta Nyuki halafu upande gari nyingine ulipie 500 mpaka makumbusho?

Hawaoni kama wanawaongezea gharama za maisha wananchi wa kawaida?
Basi waseme kila kituo unalipa pesa ijulikane tu sasa
 
Sasa kama huyo aliyetoa maelekezo hajatangaza viwango vya nauli, unafikiri wamevitangaza kimya kimya? Au wewe mwenzetu unavijua viwango vipya? Tangu lini mabadiliko ya nauli yanayotekelezwa na SUMATRA yakawa siri?

Kwa sasa wanaisoma wa Dar...labda baadaye wataisoma wa Dodoma. Sisi wengine wa maporini hata kusoma hatujui kwa hiyo hatutaweza kusoma chochote.
Kumbe na wewe sio wa "Dar?"
 
Ngozi nyeusi wapo kwa ajili ya kukomoana.
Wanataka kulazimisha kila mtu apande hizo takataka za mwendokasi?
 
Hakuna lolote ni zaid kutubebesha tu mzigo wananchi wa nauli afu ndio serikali ambayo kla cku inajitangaza rafik wa wananchi maskini
 
mleta uzi eleza vizuri, je magari ya mizigo vipi kwasababu wameongelea ya abiria tuh
 
Duh kweli balaa issue ya mafuta kushuka wamechemka, wameshindwa kushusha nauli za UDA sasa wamekimbilia kufupisha root

endeleeni kuisoma namba sie wa pugu na g/mboto tunafaidi treni letu la mwendokasi tena la kisasa kabisa full ac,choo,ulinzi mzuri yaani burudaniiiiiii kabisa!
[HASHTAG]#HAPA[/HASHTAG] SIFA TU!
 
Foleni husababishwa na private cars na sio daladala.Angalia siku za Jpili na za sikukuu,ambapo watu hawaendi maofisini;huwa foleni hakuna kabisa.
 
Nimelisikia ili tangazo la SUMATRA kwenye redio kwamba magari yote ya abiria yanayotoka Bagamoyo yataishia Tegeta Nyuki, hayatofika Mwenge wala Makumbusho. Yale ya kutoka Mbezi yataishia Kimara hayatofika mjini kwa maana hiyo unatakiwa upande gari lingine ukifika Tegeta Nyuki au Kimara.

Ninachojiuliza, inakuwaje SUMATRA wanatoa utaratibu huu bila kutoa viwango vipya vya nauli? Kwa mfano ukitoka Bagamoyo unalipa 2,200 mpaka mjini. Je nauli itabaki hiyo hiyo mpaka Tegeta Nyuki halafu upande gari nyingine ulipie 500 mpaka makumbusho?

Hawaoni kama wanawaongezea gharama za maisha wananchi wa kawaida?
Huku ni kukulupuka inawaumiza RAIA wa kawaida,kama wanataka kupunguza foleni waweke ushulumkubwa kwa magari ya binafsi kama walivyo weza kwenye piki piki
 
Nimelisikia ili tangazo la SUMATRA kwenye redio kwamba magari yote ya abiria yanayotoka Bagamoyo yataishia Tegeta Nyuki, hayatofika Mwenge wala Makumbusho. Yale ya kutoka Mbezi yataishia Kimara hayatofika mjini kwa maana hiyo unatakiwa upande gari lingine ukifika Tegeta Nyuki au Kimara

Mleta uzi unanipa hamasa ya kufika na mie huko Dasilamu nipaone pakoje! ila Muomba Mungu hachoki ngoja nivune kaufuta kangu then niuze nipate nauli ya kuja huko na mie nioshe macho
 
SUMATRA HAIPO KWA AJILI YA WANYONGE AMBAO NDIO WENGI KWENYE NCHII BALI KWA MASLAHI YAO NA VIBARAKA WAO.....

SIKU ZOTE HAKUJAWAHI KUWA NA NAFUU KWENYE HATUA ZAO.....NI BORA TU WAWE WANAKAA KIMYA WALE MSHAHARA WA BURE....KULIKO KUJA NA NGONJERA ZAO ZINAZOZIDI KUTUUMIZA BADALA YA KUTUKOMBOA......

KATIKA HALI YA KAWAIDA....WANAWEZAJE KUTOA TAMKO KAMA HILO KATIKA HALI KAMA HII AMBAKO MWANANCHI BADO ANAKIMBIZANA NA UGALI WA KILA SIKU.....

MIMI NADHANI KABLA YA KUPATA KWENYE BAADHI YA VITENGO KUWE NA UTARATIBU WA KUWAPIMA WATU AKILI.....
kama una gari nitafute mkuu
 
Duuuuuu hivi hii serkali kila kiongozi akiamka anakuja tu na tamko bila mipango?
 
Back
Top Bottom