Magari ya abiria mwisho Tegeta Nyuki na Kimara

mjingamimi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2015
Posts
46,555
Reaction score
57,569
Nimelisikia ili tangazo la SUMATRA kwenye redio kwamba magari yote ya abiria yanayotoka Bagamoyo yataishia Tegeta Nyuki, hayatofika Mwenge wala Makumbusho. Yale ya kutoka Mbezi yataishia Kimara hayatofika mjini kwa maana hiyo unatakiwa upande gari lingine ukifika Tegeta Nyuki au Kimara.

Ninachojiuliza, inakuwaje SUMATRA wanatoa utaratibu huu bila kutoa viwango vipya vya nauli? Kwa mfano ukitoka Bagamoyo unalipa 2,200 mpaka mjini. Je nauli itabaki hiyo hiyo mpaka Tegeta Nyuki halafu upande gari nyingine ulipie 500 mpaka makumbusho?

Hawaoni kama wanawaongezea gharama za maisha wananchi wa kawaida?
 
sumatra nadhani wanatafuta tu waonekani wanafanya kazi ila kila siku wanavuruga tu......... mwananchi alipe nauli mbili mbili kwa sababu zipi kwa akili zao watasema wanapunguza foleni
 
Sasa mkuu hiyo foleni hapo watakuwa wanaipunguza kwa njia ipi hao watakaoshuka Tegeta Nyuki watapanda Helicopter au watapanda gari nyingine?
Maana haimake sense kabisa kusema hiyo ndio njia ya kupunguza foleni.
 
No kamavealivyosema magari ya mwenge mwisho makumbusho na magaro ya posts tandika na mbagala kuishia stesheni na mnazi mmoja Sumatra IPO kwa ajili ya kumkamua meananchi was kaeaida badala ya kuboresha usafiri wabunge wetuvwako busy na siasa
 
Sasa mkuu hiyo foleni hapo watakuwa wanaipunguza kwa njia ipi hao watakaoshuka Tegeta Nyuki watapanda Helicopter au watapanda gari nyingine?
Maana haimake sense kabisa kusema hiyo ndio njia ya kupunguza foleni.
ndiyo hata mimi nawashangaa hawa viumbe kwa kweli .. wanatuongezea mizigo tu watu wa chini... kodi kila kona.. na nauli ishirini ishirini mfyuuuuuuuuuuuu
 
Nimelisikia ili tangazo la SUMATRA kwenye redio kwamba magari yote ya abiria yanayotoka Bagamoyo yataishia Tegeta Nyuki, hayatofika Mwenge wala Makumbusho. Yale ya kutoka Mbezi yataishia Kimara hayatofika mjini kwa maana hiyo unatakiwa upande gari lingine ukifika Tegeta Nyuki au Kimara.

Ninachojiuliza, inakuwaje SUMATRA wanatoa utaratibu huu bila kutoa viwango vipya vya nauli? Kwa mfano ukitoka Bagamoyo unalipa 2,200 mpaka mjini. Je nauli itabaki hiyo hiyo mpaka Tegeta Nyuki halafu upande gari nyingine ulipie 500 mpaka makumbusho?

Hawaoni kama wanawaongezea gharama za maisha wananchi wa kawaida?

!
!
tuwapongeze sumatra kwa maamuzi haya ya mwendokasi.
 
Mkuu ungepanda kwanza uone nauli utakayotozwa kama kuna mabadiliko au hali imezidi kuwa ngumu ndio ungekuja hapa kulalamika.
 
Sasa kama huyo aliyetoa maelekezo hajatangaza viwango vya nauli, unafikiri wamevitangaza kimya kimya? Au wewe mwenzetu unavijua viwango vipya? Tangu lini mabadiliko ya nauli yanayotekelezwa na SUMATRA yakawa siri?
 
Hawa jamaa hua wanakurupuka kutoa matangazo bila kumuangalia mtumiaji coz wao hawatumii huo usafiri
 
Sasa kama huyo aliyetoa maelekezo hajatangaza viwango vya nauli, unafikiri wamevitangaza kimya kimya? Au wewe mwenzetu unavijua viwango vipya? Tangu lini mabadiliko ya nauli yanayotekelezwa na SUMATRA yakawa siri?
Basi endeleni kuisoma namba kama alivyosema KIDUDU
 
Duh kweli balaa issue ya mafuta kushuka wamechemka, wameshindwa kushusha nauli za UDA sasa wamekimbilia kufupisha root
 
Mkuu ungepanda kwanza uone nauli utakayotozwa kama kuna mabadiliko au hali imezidi kuwa ngumu ndio ungekuja hapa kulalamika.
Sasa kama huyo aliyetoa maelekezo hajatangaza viwango vya nauli, unafikiri wamevitangaza kimya kimya? Au wewe mwenzetu unavijua viwango vipya? Tangu lini mabadiliko ya nauli yanayotekelezwa na SUMATRA yakawa siri?
Basi endeleni kuisoma namba kama alivyosema KIDUDU
Kwa sasa wanaisoma wa Dar...labda baadaye wataisoma wa Dodoma. Sisi wengine wa maporini hata kusoma hatujui kwa hiyo hatutaweza kusoma chochote.
 
Itasaidia kupunguza msongamano katika jiji la Biashara
 
SUMATRA HAIPO KWA AJILI YA WANYONGE AMBAO NDIO WENGI KWENYE NCHII BALI KWA MASLAHI YAO NA VIBARAKA WAO.....

SIKU ZOTE HAKUJAWAHI KUWA NA NAFUU KWENYE HATUA ZAO.....NI BORA TU WAWE WANAKAA KIMYA WALE MSHAHARA WA BURE....KULIKO KUJA NA NGONJERA ZAO ZINAZOZIDI KUTUUMIZA BADALA YA KUTUKOMBOA......

KATIKA HALI YA KAWAIDA....WANAWEZAJE KUTOA TAMKO KAMA HILO KATIKA HALI KAMA HII AMBAKO MWANANCHI BADO ANAKIMBIZANA NA UGALI WA KILA SIKU.....

MIMI NADHANI KABLA YA KUPATA KWENYE BAADHI YA VITENGO KUWE NA UTARATIBU WA KUWAPIMA WATU AKILI.....
 
Back
Top Bottom