Magari manane yenye sukari yakamatwa Kilimanjaro

Mzee Busara

Senior Member
Feb 29, 2008
113
19
Tuesday, 08 November 2011 22:13
0diggs
digg
Fina Lyimo, Moshi

POLISI mkoani Kilimanjaro wamefanikiwa kukamata magari manane yakiwa yamesheheni sukari na mahindi, yakisafirisha kimagendo bidhaa hizo kimagendo kwenda nchini Kenya.Kaimu Kamanda wa Polisi, Yusuph Ilembo alisema katika zoezi hilo, polisi wamekamata sukari mifuko 54 na magunia ya mahindi 390.

Ilembo alisema jana kuwa sukari hiyo ilikamatwa maeneo ya kituo kikuu cha polisi cha mjini Moshi usiku wa kuamkia jana.Kwa mujibu wa Ilembo, sukari hiyo ilikamatwa katika magari mawili tofauti, moja likiwa ni la Kampuni ya Utalii aina ya Toyota Landcruicer na lingine Toyota Prado mali ya kigogo mmoja wilayani Rombo.

Pia polisi walikamata malori sita yakiwa yamesheheni mahindi yakiyasafirisha kwenda Kenya na kwamba magari hayo yanashikiliwa katika Kituo cha Polisi mji Mdogo wa Himo.

Wakati huohuo,taarifa zilizopatikana jana mchana zilisema Serikali imezifutia adhabu,kampuni tatu zilizofutiwa vibali vya kusambaza sukari inayozalishwa na Kiwanda cha TPC Limited cha mjini Moshi.

Habari zilizopatikana jana mchana zilisema uamuzi wa kuziruhusu kampuni hizo ulitolewa na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Jumanne Maghembe.Kampuni hizo ni Mohamed Enterprises Ltd,Starways Enterprises na Marenga Investment ambazo zilifutiwa vibali hivyo na Serikali miezi miwili iliyopita.

Afisa mtendaji mkuu wa TPC anayeshughulikia utawala,Jaffar Ally jana alithibitisha kupokea barua ya waziri ikimfahamisha juu ya uamuzi huo wa serikali.Hatua ya kuzirejeshea vibali inaonekana kuishtua Serikali ya Mkoa Kilimanjaro ambayo ililazimika kukutana kwa dharura jana mchana.

Mkuu wa mkoa ,Leonidas Gama alisema alilazimika kuitisha kikao hicho kujadili hali hiyo na angetoa taarifa baadaye jana.Hata hivyo hadi saa 10.00 alasiri, Gama hakuweza kupatikana kueleza kile kilichowasukuma kukutana kwa dharura kutokana na simu yake kuita bila majibu.

Wakati akizifutia vibali, Waziri alizituhumu kampuni hizo kukiuka masharti ya mikataba yao kwa kuuza sukari nje ya nchi. Waziri Maghembe alidai vitendo hivyo vilisababisha sukari katika soko la ndani kuadimika na kuuzwa hadi sh2,500 kwa kilo wakati huo.

Hata hivyo pamoja na kufungiwa kwa kampuni na kuteuliwa mawakala wapya, bado sukari ilizidi kuadimika huku bei ya kilo moja ikifikia Sh4000.Lakini habari zilizopatikana jana zilisema Waziri Maghembe alizirejeshea vibali kampuni hizo baada ya kuomba radhi .



source mwananchi
 
Hapo chadema hawezi kulaani kitendo hicho lakini sukari ikiadimika watamshambulia kikwete wakati na wao wana nafasi ya kukemea na kusemea mambo kama hayo ili kuonyesha kwamba hawaungi mkono kuuza sukari nje huku wananchi wakiteseka
 
wakati mwingine serikali inaonekana inafanya vibaya huku vyama vya upinzani vikishindwa japo tu kulaani matukio yasiyo na maslahi kwa taifa ili kuonyesha kwamba wakiingia madarakani wataweza kukemea uhalifu wa aina yoyote.
 
umejuaje? ndio hao hao wanaisumbua sana serikali

Si dio, ikiwa hata sukari wanaondoa nchini kwenda kuuza nchi jirani kama si kuisumbuwa serikali ni nini huko? wacha serikali wanasumbuwa hata raia.
 
Back
Top Bottom