Magamba yatatuua yatatumaliza, watch out. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Magamba yatatuua yatatumaliza, watch out.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MPadmire, Nov 27, 2011.

 1. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #1
  Nov 27, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Eeeheee, naumwa Kichwa.

  Ikulu kuna nini? Mbona Mwalimu Nyerere alitoka mwembamba?

  Nashangaa sasa hivi watu wanapigana vikumbo wanataka Ikulu, kuna nini sasa hivi.

  Watu wanagombania Ikulu kwenda kuwatumikia Watanzania kweli?

  Mawaziri hawapo tena katika kutumikia wananchi, wanafikiri zaidi jinsi ya kuingia Ikulu, uhayawani huo!!!!......

  Hawa wakuu wanatakiwa watumie akili zao kubuni mbinu za kuinua uchumi, kuboresha huduma za afya, kuinua elimu..

  Hospitali hazina dawa, wanafunzi hawana mikopo, shule za sekondari hazina maabara, shillingi imekufa, mfumuko wa bei....

  Hivi kwa matatizo haya, mawaziri kwa nafasi zao hawataki kushughulikia kwa umoja wao au kwa mchango wa kila mmoja katika baraza la mawaziri.

  Je huyo waziri akija kugombea uraisi atatuambia nini watanzania tumuelewe na tumpe kura, hapana. Watu kama hawa watakosa ushawishi kwa wananchi, na watanyimwa kura. Na kwa sababu wana uchu na Ikulu, wakikosa kura, wataiba kura.

  Hapo ndo sasa haya magamba yatatuuwa yatumalize, maana kamwe hiki kizazi cha dot com hakitakubali tena kura ziibwe.

  Hii ni mbaya mno, mbaya kuliko kawaida, hapa magamba yatapiga mabomu ya machozi, risasi za moto na watatumia vyombo vya dola kutumaliza watanzania. Watch out.... Hapa magamba yataiba kura na yatatumia vyombo vya dola kuiba kura na kuhalalisha wizi.

  hapa tu kwenye katiba wanataka kuchakachua, Natabiri maafa, maana haki imepotea, demokrasia hakuna, uchumi kwishney, umasikini umezidi, ajira hakuna na huduma za afya hakuna. Kwa hali hii magamba hawatapata kura hata moja ila wao watatumia nguvu za dola.

  Ole wao, maana wameanza kutuuwa kwa kutunyima huduma za afya, wametunyima elimu, wametufanya masikini na wametuibia.

  Wanakula kodi zetu na hawafanyi kazi wanawaza tu uraisi, what for? kama umeshindwa kuwa mwaminifu kwa uwaziri, je uraisi ndo itakuwaje??

  Mimi sioni Candidate for presida kutoka magambani mie....
   
Loading...