Magamba ya CCM bado ni mengi

emalau

JF-Expert Member
Apr 25, 2009
2,775
3,100
Toka juzi habari iliyotawala vyombo vya habari ni ile ya CCM kudai kwamba imejivua gamba, nimetafakari kwa undani juu ya kauli hii nikagundua ni usanii mtupu. Wameamua kuchua mbuzi wa kafara wachache akina Chenge, EL, RA ili kuwalaghai watanzania kwamba sasa wameamua kuwa serious. na sasa nasikia kwamba wanataka kuanza ziara za mikoani kusherehekea usanii huu kama mazuzu.

Nionavyo mimi kama wameamua kujivua gamba hakuna hasiyefahamu kwamba kampeni za anasa za mwaka 2005 zilitokana na pesa za EPA. Kwa hiyo kama kweli wameamua kujivua gamba warudishe pesa za EPA walizokwapua na wawaombe msamaha watanzania kwa kwa wizi huo, hapo ndo nitaamini kwamba wameamua kujivua gamba.

Wakija mikoani na mbwembwe zao waulizeni mbona pesa mlizokwapua hamjarudisha?

Magamaba ya CCM yako mengi ikiwa ni pamoja na mbinu chafu za wizi wa kura, n.k lakini kwa leo naishia hapa

Naomba kuwakilisha wana Jf
 
Back
Top Bottom