Magamba si mchezo: Idd Azzan aomba radhi CCM!

Magamba si mchezo: Idd Azzan aomba radhi CCM!

Mtu Mmoja

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2010
Posts
593
Reaction score
64
Idd Azzan aomba radhi CCM

MBUNGE wa Kinondoni, mkoani Dar es Salaam, Idd Azzan, ameomba radhi mbele ya kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam, kwa kitendo cha kukiuka maadili ya chama na kuwatuhumu viongozi wenzake katika vyombo vya habari.

Hayo yamesemwa jana Dar es Salaam na Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Mkoa, Juma Simba wakati akizungumza na waandishi wa habari na kuitaka Kamati ya Siasa ya Mkoa kutazama upya adhabu dhidi ya Mbunge huyo ya karipio kwa lengo la kumuondolea.

Azzan alifungiwa kwa miezi 18 kutogombea nafasi yoyote ndani ya chama pamoja na kupewa onyo kali kwa kosa la kutumia vibaya madaraka yake na kuzichafua mamlaka za CCM Mkoa wa Dar es Salaam.

Adhabu hiyo ilitolewa baada ya Azzan kuwatuhumu wajumbe wa Kamati ya Siasa na Sekretarieti ya Mkoa kuwa ni mafisadi na wala rushwa na kuwataka wajivue gamba.

Kwa mujibu wa Simba, Azzan aliomba radhi katika kikao cha kawaida cha Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa kilichofanyika juzi.

“Katika kikao hicho kilichofanyika Kinondoni pamoja na mambo mengine, kilitoa maagizo hayo kwa Kamati ya Siasa baada ya mhusika kuomba radhi,” alisema Simba.

Simba alisema kutokana na uamuzi huo wa Halmashauri ya Mkoa, Kamati ya Siasa itakutana na kuzingatia kanuni katika kutekeleza agizo hilo.

Katika hatua nyingine Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam imekubali maombi ya Khamis Kizenga ya kurejeshewa uanachama wa CCM baada ya kutumikia adhabu ya kuvuliwa uanachama kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu.

source: HabariLeo | Idd Azzan aomba radhi CCM
 
Aliogopa watamnyang'anya kadi akakosa ubunge nini???.....kweli haya magamba yamekomaa hayavuliki.
 
Aliogopa watamnyang'anya kadi akakosa ubunge nini???.....kweli haya magamba yamekomaa hayavuliki.

Jamani si walisema wameshayavua. Tatizo walikosea kuvua magamba, halafu wakabaki na damu, nawashauri wakanyonywe damu ndo ingekuwa powaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
sasa wanajamii kama mtu yuko kwenye chama na haruhusiwi kumtuhumu mwenzake ndani ya chama hicho hicho maana yake nini? Kumbe ndo maana mambo yanaharibika tu ndani ya chama kwa kuwa ni kosa kumwambia yule aliyekosea ukweli!!!! Hii ni kanuni au sheria gani katika karne hii tuliyomo jamani?? Hapa kweli panahitaji elimu kulijua hili kuwa ni tatizo ndani ya chama chetu jamani? Kwa nini wakuu mlioko kwenye CC hamlioni hili? Au kwa vile kanuni hizi zinafanikisha ninyi mlioko juu kuwa miungu watu kwenye chama chetu? kwa hali hii chama kikifa tutatafuta mchawi? Wakati sheria na kanuni zetu zinatuloga wenyewe? Jamani fungueni macho muone, mchana kweupe mnajifanya kufunga macho ili msione??? Mungu atawalaani asilani..........
 
Maneno ukiisha tema hayaru hayarudi kweli, kamalizana na hao, sasa na sisi wenyenchi aje atueleze alikuwa anamaanisha nini? alitudanganya?
 
Natumaini hata NAPE atawaomba radhi RACHEL kwa yale aliyoropoka kwenye vyombo vya habari
 
niliyajua hayo namfahamu bwana Azani hana ujasiri yule ni mwoga wa kutupwa mkwara kidogo tu kakimbia kumbe aliyoyasema sio kweli? pole sana bwana idd kama huna kifua ya nini kuvua shati?
 
Jamani si walisema wameshayavua. Tatizo walikosea kuvua magamba, halafu wakabaki na damu, nawashauri wakanyonywe damu ndo ingekuwa powaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!


Kwa elimu yangu ya darasa la nne (middle school) la mkoloni sijapata kusikia au kusoma mahali kwamba nyoka ana damu inayonyonyeka labda ile baridi; na kuitoa inahitajika sayansi nyingine.
 
Yaani unitukane unambie ooh am sore infwakt nilikuwa nimelewa sana! Waapi wewe ujumbe ushafika hata akimba radhi!
 
huyu muuza unga hana lolote majigambo yote kwenye vyombo vya habari halafu kumbe huna ushahidi? kwanza amepata ubunge kwa kuiba kura then analeta za kuleta...mwisho wake hauko mbali lol
 
Natumaini hata NAPE atawaomba radhi RACHEL kwa yale aliyoropoka kwenye vyombo vya habari

Nimekusoma kabisa, mpaka sasa hajajua wenye magamba, atakapowajua ataomba radhi, kakilia na kuomboleza:A S 103:
 
Alikuwa hafahamu kuwa JK ni kinyonga, akajiingiza kichwa kichwa. Jk keshapiga chenga na kurejea kukumbatiana na magamba!
 
Mi nilijiuliza sana huo ujasiri Iddi ameutoa wapi???? Nilijua tu akiminywa kidogo kwenye maslahi atalegea tu,
 
Kuomba radhi kama umekosea ni kitendo cha kiungwana. Hii inadhihirisha kuwa CCM ina matatizo ktk watu wake maana huyu Azan kasema kitu ambacho hawezi kukisimamia. Ndiyo maana hata maendeleo hatuna kwani viongozi wetu wanasema vitu ambavyo hawawezi kuvisimamia au kuwajibika navyo!
 
Sijui kama tutafika kwa hali ya namna hii. Matatizo ya nchi yetu ni mengi na yanahitaji ujasiri kuyakabili. Ikiwa mtu unaona jambo linaenda ndivyo sivyo unalikaripia na kukosa ujasiri kulisimamia unaloona ni sahihi ni kutuvunja moyo wananchi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom