Inawezekana haya yanayoendelea huku Mafwele akiwa mtuhumiwa maarufu ni mpango wa Mungu. Mimi kama mkristo msoma biblia mzuri nimeona labda haya yote yanayotokea ni mpango wa Mungu na huyu Mafwele anatumika tu kutekeleza hiyo mipango. Mafwele ni mtu wa serikali na kama tunavyosoma kwenye biblia kwamba serikali zilizopo zimewekwa na Mungu mwenyewe. Kutii mamlaka ni muhimu.
Ukisoma biblia utaona jinsi gani Mungu alivyokuwa akitoa adhabu za kikatili kwa wote waliotenda dhambi zilizomkera hadi kukosa uvumilivu. Kuna jamaa aliuliwa na Mungu kwa kukosa la kumwagia nje wakati wa tendo (soma Mwanzo 38). Kipindi cha Nuhu watu waliuwawa kupitia gharika. Wana wa Israel jangwani waliuliwa mno.. kuna wakati Mungu aliwapelekea nyoka wenye sumu kuwagonga wadhambi wote. Ikumbukwe kabla ya waisrael kuondoka Misri ilibidi wazaliwa wa kwanza kwenye familia zote za wamisri wauliwe na Mungu mwenyewe ili Farao aweze kuwaruhusu Waisrael kuondoka.
Kimsingi visa ni vingi sana vya mauaji yaliyofanywa na Mungu mwenyewe kwa wale wote waliokuwa kinyume naye. Hata sisi tunaasubiri kuchomwa moto kwa dhambi tulizo nazo. Lakini pia tunaweza kusema haya matukio yanayoendelea ni mpango wa shetani kumbe shetani ana ruhusa kutoka kwa Mungu kufanya anayofanya. Tukumbuke kabla ya Ayubu kupitia majanga, shetani aliomba ruhusa toka kwa Mungu na kuruhusiwa afanye kila kitu ila asimuue tu Ayubu.
Huenda kuna maovu sisi watanzania tumefanya na kumchukiza Mungu ndo maana tunapita kwenye hii misukosuko na kumlaumu Mafwele. Inawezekana Mafwele ni mjumbe tu.