Mafuta yapo haya yamulikwe

Mafuta yapo haya yamulikwe

mapessa

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2014
Posts
664
Reaction score
1,168
1. Mafuta yapo, wanaoleta shida ni wenye vituo kuzuia kuuza stock ya mafuta wakisubiri bei mpya iende juu ili faida yao iwe kubwa.

2. Serikali ifanye msako na kutoa adhabu kwa vituo vinavyofanya ghasia hii kwa sababu ni uhujumu uchumi.

3. Inawezekana pia vituo hivi vinatumiwa na wapinzani au mataifa ya nje kuleta taharuki kwenye siasa za ndani na utulivu wa nchi yetu hivyo mbali na adhabu wamiliki wamulikwe zaidi mara kwa mara.

4. Suala la utoaji wa leseni za vituo vya mafuta litazamwe kama suala la uhai na usalama wa nchi. Kama ambavyo tunatumia muda mwingi kufanya vetting ya leseni za makampuni ya mbegu za mimea yanayokuja nchini, NGOs, leseni za benki n.k. Umefika wakati sasa kuwa na utaratibu makini zaidi kutoa leseni za wafanyabiashara ya mafuta ili kuzuia uhujumu tunaouona mara kwa mara.

NB subiri uone kama muda huu kila kituo hakijawa na mafuta.! Bei mpya zimetoka.
 
Hapo namba 3 hayo mawazo ya mwaka 47 mtayaacha lini? Mtaacha lini kujificha kwenye vichaka vya upinzani na mabeberu kwa uzembe wa serikali?

Ishu hapa ni serikali imelala usingizi wa pono! Rais yupo usingizini, waziri mkuu yupo usingizini, waziri mwenye dhamana yupo usingizini, watu wanajiamulia wanavyotaka, ni la manyani aka utawala binafsi. Nchi imekuwa yatima.

Kwenye mambo kama haya ndipo Magufuli alikuwa akijichukulia pointi 3 muhimu, hayo mafuta wanayoyabania kusubiri bei zipande wangeyanywa na familia zao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama wenye vituo hawana mafuta kwa kuwa yameisha, unataka wafanyeji ili kukuhakikishia kwamba mafuta yameisha?

Leo ni tarehe 6 ya mwezi wa tisa, kwa nini ewura hawajatoa bei elekezi siku zote hizi?

Nikienda depot kuchukua mafuta kwa bei ya sasa na punde ewura wakatoa bei kikomo chini ya bei niliyonunulia hiyo hasara utaibeba wewe?
 
1. Mafuta yapo, wanaoleta shida ni wenye vituo kuzuia kuuza stock ya mafuta wakisubiri bei mpya iende juu ili faida yao iwe kubwa.

2. Serikali ifanye msako na kutoa adhabu kwa vituo vinavyofanya ghasia hii kwa sababu ni uhujumu uchumi.

3. Inawezekana pia vituo hivi vinatumiwa na wapinzani au mataifa ya nje kuleta taharuki kwenye siasa za ndani na utulivu wa nchi yetu hivyo mbali na adhabu wamiliki wamulikwe zaidi mara kwa mara.

4. Suala la utoaji wa leseni za vituo vya mafuta litazamwe kama suala la uhai na usalama wa nchi. Kama ambavyo tunatumia muda mwingi kufanya vetting ya leseni za makampuni ya mbegu za mimea yanayokuja nchini, NGOs, leseni za benki n.k. Umefika wakati sasa kuwa na utaratibu makini zaidi kutoa leseni za wafanyabiashara ya mafuta ili kuzuia uhujumu tunaouona mara kwa mara.

NB subiri uone kama muda huu kila kituo hakijawa na mafuta.! Bei mpya zimetoka.
Mpinzani ana ubavu wa kuzuia mafuta?
 
Back
Top Bottom