Mafuta 'yanayowafanya wanaume kumea maziwa'

Mafuta 'yanayowafanya wanaume kumea maziwa'

Rashford Lingard

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2018
Posts
938
Reaction score
1,152
_100451625_essentialoils_gettyimages-185279091.jpg

Uhusiano kati ya matiti yasio ya kawaida ambayo humea miongoni mwa wavulana na utumizi wa mafuta ya mti wa lavender na ule wa chai umetoa uzito tofauti baada ya utafiti kubaini kwamba kemikali nane zinazopatikana katika mafuta ya miti hiyo uharibu kazi ya homoni za kiume.

Utafiti huo wa Marekani umebaini kwamba kemikali muhimu katika mafuta hayo hupiga jeki homoni za kike na kuharibu homoni za kiume.

Mafuta ya mimea hiyo hupatikana katika bidhaa tofauti kama vile sabuni, mafuta ya kujipaka mafuta ya kuosha nywele pamoja na na bidhaa za kutengeza nywele.

Pia ni maarufu sana katika bidhaa za kuosha mbali na matibabu. Kiongozi wa utafiti huo, J.Tyler Ramsey kutoka taasisi ya kitaifa kuhusu mazingira ya sayansi ya afya katika jimbo la Carolina Kaskazini alionya watu kutahadhari wakati wa utumizi wa mafuta hayo.

''Jamii yetu huona mafuta hayo ya asilia kuwa salama. Hatahivyo humiliki kiwango kikubwa cha kemikali na ni sharti yatumiwe na tahadhari kwa kuwa baadhi yao husababisha uharibifu wa homoni''.

Visa kadhaa vya tatizo la kumea matiti miongoni mwa wanaume vimeripotiwa kutokana na utumizi wa mafuta hayo yenye manukato.

Baada ya kusitisha utumizi wa mafuta hayo tatizo hilo huisha lenyewe. Utafiti wa awali uliofanywa na Daktari Kenneth Korach - ambaye alichunguzwa kutokana na utafiti huo ulibaini kwamba mafuta ya mti wa Lavender na ule wa chai ulikuwa na ishara za kuharibu homoni zinazodhibiti tabia za kiume ambazo zinaweza kuathiri kubalehe na ukuwaji.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mafuta asilia yakitiwa katika chupa
Utafiti mpya uliangazia kemikali nane muhimu kati ya 100 zinazotumika kutengeza mafuta . Kemikali nne zilizokaguliwa zilipatikana katika mafuta yote huku nyengine zikipatikana katika mafuta hayo yenye manukato.

Zilijaribiwa katika seli za saratani miongoni mwa binadamu katika maabara ili kupima mabadiliko.

Watafiti walibaini kwamba mafuta hayo yamekuwa yakipiga jeki homoni za kike na kuharibu zile za kiume.

''Mafuta ya Lavender na yale ya mchai yanasababisha madhara ya kimazingira na yanafaa kuchunguzwa'' , alisema bwana Ramsey. Kemikali nyingi zilizojaribiwa hazikuwa na madhara mabaya.

Tahadhari ya kutumia mafuta hayo.
  • Tahadhari lazima ichukuliwe unapotumia mafuta ya Lavender na yale ya mchai.
  • Usijipake mafuta ambayo hayajakuwa majimaji katika mwili wako moja kwa moja
  • Usitumie mafuta yasio majimaji kwa watoto walio chini ya miaka mitatau.
  • Iwapo ni mjamzito lazima upate ushauri wa daktari wako kabla ya kutumia mafuta hayo.
  • Iwapo mafuta hayo yatatumika vyema ni salama kwa familia nzima.
  • chanzo: Aromatherapy Trade Council
 
Hili nilishawahi kulisikia.

Sabuni nyingi zile zenye manukato zimetengenezwa na kuwekwa kemikali maalumu ambazo zina vichocheo vya ushoga.

Na hili halijawekwa kwa bahati mbaya.
 
Nimewahi sikia wanawake wanaongelea sabuni za "kukuza" makalio. Itakuwa ndo hizi hizi
 
Back
Top Bottom