SHELL ilikuwa kampuni kubwa ya kuuza mafuta kama ilivyokua Total, esso, CALTEX, Agip, BP nk. SHELL ilipigwa marufuku pamoja na kampuni zake tanzu kuendesha biashara Tanzania, baada ya wamiliki wa kampuni hiyo kujihusisha na siasa za Zimbabwe. walimuunga mkono Ian Smith.Simith, mzungu aliyekuwa na uraia wa Zimbabwe, zamani ikiitwa Rhodesia. Smith alipewa madaraka kinafiki na Uingereza ili kuwatuliza wapigania Uhuru wa nchi hiyo wakiongozwa na ZANU PF. Tanzania iliyokuwa mwenyekiti wa nchi zilizo mstari wa mbele kwenye ukombozi wa nchi za kuzini mwa Afrika zilimkataa Ian Smith na hivyo SHELL ikatimuliwa Tanzania. Kwakuwa ilikuwa na vituo vingi vya kuuzia nishati hiyo jina lake bado linatamba. SHELL walikuwa wanatumia logo hii hapa
View attachment 786380