Mwenzenu ninatatizwa na jambo moja nalo nihili la Umeme na maswala ya Dowans....
Nikifikiri kwa makini na kwakina natatizika, kweli hakuna mkono wa namna namna katika hili swala la kukatika umeme TANZANIA na hujuma ?
Hebu fikiri Rais JK Kikwete (Mheshimiwa) alitoa tangazo kua mitambo ya IPTL iwashwe, kisha tukaambiwa na kina Mh. Ngeleja kuwa Serikali imeagiza mafuta ya kutumia kwenye mitambo ya IPTL ARABUNI, Baada ya siku chini ya sita, tukataarifiwa kuwa mafuta yameletwa na merikebu ya mizigo...na yamefika bandari ya Dar es salaam yakisubiri kupakuliwa ili mitambo hiyo iwashwe...
Sasa najiuliza meli toka Arabuni huchukua siku ngapi ? Au mafuta yaliagizwa kabla ya ikulu kuzungumza? Bado najiuliza au tuliishapata dili la IPTL tulichokuwa tunasubiri ni mitambo izimwe nchi iwe kizani ?
Mimi naogopa hapa, na Hisia kua kunakitu nyuma ya sakata zima la umeme Tanzania inanijia...
Ni mawazo yangu.
Tanzania ni nchi inayoendeshwa kidharula sana, hiyo ndo tabu, haijalishi nini maana skendo zote katika nishati zinaanziaga kwenye huo upuuzi wa dharula, ni kama tumelaaniwa, hatuna dira wala mwelekeo, Mungu atawalaani wote waliochangia kuingia kwetu gizanikumbuka jambo moja best yangu, suala kubwa la kitaifa huwa halianzii ktk TV pale rais anpotoa tamko ili na wananchi wasikie, lazma tangu athari za kuonekana mgao utatikea hizi logistics zilianza, so mafuta kupakuliwa bandarini sino ajabu, pia raisi siku alipotoa tamko may be angesema tueact mapema mafuta ya IPTL tayari ndani ya one week mgao off. Issue hapa ni kwamba hakuna alternative japo IPTL na matatizo yake yote ili kunusuru uchumi ambao basicaly ni mkubwa kuliko kurun IPTL ilibidi iwashwe. Why hatujajiuliza IPTL imesimama bila uzalishaji mda gani imekuwaje wapo ready ready kutembeza mitambo? Tumekuwa tukiwataka viongozi wetu kuact quickly na ndio kimefanyika, hapa labda tujadili hela imetoka wapi? na je IPTL watauza umeme Tanesco kwa bei gani? ile ya mkataba wao bei juu sana? au wamepewa amri kuzalisha bure i mean wapewe tu running cost? ndo ya kujadili hapa
Tumuulize NGELEJA palepale Tegeta kuna mtambo mpya wa TANESCO utakaotumia gesi ambao utatoa MW 20.Umechelewa kuanza kazi kutokana na vifaa KUCHELEWESHWA BANDARINI.JEE KWA NINI SERIKALI HAIKUCHANGAMKIA KUTOA VIFAA VYA MKANDARASI HUYO KAMA ILIVYOCHANGAMKIA MAFUTA?Jee kwenye hii order ya mafuta ilifuata taratibu za manunuzi ya PPRA??
Mkuu, ni mtambo wa MW40.Tumuulize NGELEJA palepale Tegeta kuna mtambo mpya wa TANESCO utakaotumia gesi ambao utatoa MW 20.Umechelewa kuanza kazi kutokana na vifaa KUCHELEWESHWA BANDARINI.JEE KWA NINI SERIKALI HAIKUCHANGAMKIA KUTOA VIFAA VYA MKANDARASI HUYO KAMA ILIVYOCHANGAMKIA MAFUTA?
Hii serikali nimeanza kuamini imejaa retards,wanatumia 23 bilion kununua mafuta kwa mwezi kutoka kwa mwarabu kuwasha mitambo michafu kwa umeme wa siku mbili huku tumejaza clean natural gas ya kwetu wenyewe ambayo ni cheap na ingetoa ajira kwa watanzania wenzetu na tusingetumia dollars...can you imagine 23 bilion zingeingia kwenye kampuni za ndani uchumi wetu ungekuwa kiasi gani na kuhakikisha ajira za watu wetu na kupata kodi hapo hapo,hivi kwanini inakuwa ngumu sana kwa hii serikali kufanya vitu rahisi kama hivi vyenye faida kwa nchi yetu? ni 10% tuu au kuna mengine? hivi ni kweli serikali imeshindwa kununua generators mbili au moja za 100MW zitakazotumia gas yetu wenyewe? kweli this is heartbreaking!
Mr. Nguvumali,
Kwakweli hapo nami nilichanganyikiwa its not possible at all labda iyo mipango ilipangwa tokea mwanzo wa sakata zima la Umeme toka kipindi cha Richmond si jui Dowans kuna kitu kinapikika hapo
Nataka kuuliza Nini Maana ya Ikulu?
Utendaji wake wa kazi na wajibu wake ni upi?
Je Ikulu walikuwa wakijua hili swala zima la mkanganyiko wa umeme?? Kwani ni jambo la kustahajabisha ndani ya muda huo wa sio chini ya siku 6, Meli ya mafuta ilisha tinga bandarini??
Twahitaji Ikulu Itupe majibu ya kimsingi na yanayo eleweka iweje tamko litoke Ikulu na mafuta yafike mapema? kama sio kulikuwa na kamati ndogo ndogo za siri zilikaaaa mapema na hata kabla ya mgao kuanza walipanga mikakati na tena hiii ni ya siri mno ya wezekana hata waziri ngereja he was aware of the Matter kabisa iweje ilo agizo limetekelezwa mapema kiasi hicho na kushindwa kuakatisha mkataba wa Richmond au kuwafukuza ndani ya nchi yetu?? na kuwaaacha wabunge wakirushiana maneno.
Hapa viongozi wetu wanatupotezea muda wetu kwanza wa ku watch TV, Kuwasikiliza majuukwaani kwenye lingo za siasa, Radioni, pia nayo magazeti yanauza na kutufirisi pesa zetu na kuwa maskini
The Government is totaly confusing us jamani, Viongozi hawaoni aibu ati
nadhani mheshimiwa Rais atajibu soon, hawezi kuwaachia muanze mapema hivi ku-speculate kwamba eti wanatafuta hela za kampeni...and by the way, hivi Kikwete anavyopendwa, mnadhani kuna ulazima wa pesa mwakani??? kama mnabisha, angalieni data za REDET....
Mwenzenu ninatatizwa na jambo moja nalo nihili la Umeme na maswala ya Dowans....
Nikifikiri kwa makini na kwakina natatizika, kweli hakuna mkono wa namna namna katika hili swala la kukatika umeme TANZANIA na hujuma ?
Hebu fikiri Rais JK Kikwete (Mheshimiwa) alitoa tangazo kua mitambo ya IPTL iwashwe, kisha tukaambiwa na kina Mh. Ngeleja kuwa Serikali imeagiza mafuta ya kutumia kwenye mitambo ya IPTL ARABUNI, Baada ya siku chini ya sita, tukataarifiwa kuwa mafuta yameletwa na merikebu ya mizigo...na yamefika bandari ya Dar es salaam yakisubiri kupakuliwa ili mitambo hiyo iwashwe...
Sasa najiuliza meli toka Arabuni huchukua siku ngapi ? Au mafuta yaliagizwa kabla ya ikulu kuzungumza? Bado najiuliza au tuliishapata dili la IPTL tulichokuwa tunasubiri ni mitambo izimwe nchi iwe kizani ?
Mimi naogopa hapa, na Hisia kua kunakitu nyuma ya sakata zima la umeme Tanzania inanijia...
Ni mawazo yangu.
Inaelekea Zitto aliujua huu mchezo mapema na katika jitihada za pre-emption akashauri serikali itumie mitambo ya Dowans, kama serikali ingekubali bila shaka EL na RA wangefaidika na hivyo kuzidi kuipa nguvu kambi ya mafisadi na kuchochea mgawanyiko zaidi kwa chama chetu na pengine kuwanufaisha wapinzani japo indirectly.
nadhani muungwana akashtukia hiyo na kuamua kutumia IPTL kwa kuwa pengine hana hakika kama EL na RA watamuunga mkono financilally come yr 2010. having said that, inawezekana hii ni dili ya muungwana kutengeneza pesa kwa ajili ya uchaguzi come yr 2010...who knows...si wanasema siasa ni mchezo mchafu...pengine huu ndio katika huo uchafu...
maoni yangu tu...
Nguvumali umeniibulia mambo ambayo sikuwa na yafikria kwa sasa,kiufupi na likely ndiyo hivyo JK alilihalisha dili hili muda mrefu sana na mafuta yaka nunuliwa huko Uarabuni labda mwezi wa 6 hivi,na wakati Meli inakaribia kufika ukanda wa Afrika Mashariki ndipo mitambo ya Dr Rashid ikazimwa ili kuwaonyesha watz umuhimu wa umeme!
Again,thx u alot Nguvumali kuibua hoja hii na kwa kweli hii ni scandal mpya ktk uongozi legelege wa JK! Yaani asema wiki iliyopita kama IPTL itawasha umeme wake na mara hii mafuta yanunuliwe then yawe yamefika bandarini TZ?shame on you JK!!