Mafuta ya IPTL yamenunuliwa wapi?

Mwenzenu ninatatizwa na jambo moja nalo nihili la Umeme na maswala ya Dowans....

Nikifikiri kwa makini na kwakina natatizika, kweli hakuna mkono wa namna namna katika hili swala la kukatika umeme TANZANIA na hujuma ?

Hebu fikiri Rais JK Kikwete (Mheshimiwa) alitoa tangazo kua mitambo ya IPTL iwashwe, kisha tukaambiwa na kina Mh. Ngeleja kuwa Serikali imeagiza mafuta ya kutumia kwenye mitambo ya IPTL ARABUNI, Baada ya siku chini ya sita, tukataarifiwa kuwa mafuta yameletwa na merikebu ya mizigo...na yamefika bandari ya Dar es salaam yakisubiri kupakuliwa ili mitambo hiyo iwashwe...

Sasa najiuliza meli toka Arabuni huchukua siku ngapi ? Au mafuta yaliagizwa kabla ya ikulu kuzungumza? Bado najiuliza au tuliishapata dili la IPTL tulichokuwa tunasubiri ni mitambo izimwe nchi iwe kizani ?

Mimi naogopa hapa, na Hisia kua kunakitu nyuma ya sakata zima la umeme Tanzania inanijia...

Ni mawazo yangu.

kumbuka jambo moja best yangu, suala kubwa la kitaifa huwa halianzii ktk TV pale rais anpotoa tamko ili na wananchi wasikie, lazma tangu athari za kuonekana mgao utatikea hizi logistics zilianza, so mafuta kupakuliwa bandarini sino ajabu, pia raisi siku alipotoa tamko may be angesema tueact mapema mafuta ya IPTL tayari ndani ya one week mgao off. Issue hapa ni kwamba hakuna alternative japo IPTL na matatizo yake yote ili kunusuru uchumi ambao basicaly ni mkubwa kuliko kurun IPTL ilibidi iwashwe. Why hatujajiuliza IPTL imesimama bila uzalishaji mda gani imekuwaje wapo ready ready kutembeza mitambo? Tumekuwa tukiwataka viongozi wetu kuact quickly na ndio kimefanyika, hapa labda tujadili hela imetoka wapi? na je IPTL watauza umeme Tanesco kwa bei gani? ile ya mkataba wao bei juu sana? au wamepewa amri kuzalisha bure i mean wapewe tu running cost? ndo ya kujadili hapa
 
Tanzania ni nchi inayoendeshwa kidharula sana, hiyo ndo tabu, haijalishi nini maana skendo zote katika nishati zinaanziaga kwenye huo upuuzi wa dharula, ni kama tumelaaniwa, hatuna dira wala mwelekeo, Mungu atawalaani wote waliochangia kuingia kwetu gizani
 
Tumuulize NGELEJA palepale Tegeta kuna mtambo mpya wa TANESCO utakaotumia gesi ambao utatoa MW 20.Umechelewa kuanza kazi kutokana na vifaa KUCHELEWESHWA BANDARINI.JEE KWA NINI SERIKALI HAIKUCHANGAMKIA KUTOA VIFAA VYA MKANDARASI HUYO KAMA ILIVYOCHANGAMKIA MAFUTA?Jee kwenye hii order ya mafuta ilifuata taratibu za manunuzi ya PPRA??

TUNADANGANYIKA!!!

Hapa kuna chezo limechezwa alianza Mh Zitto huyu alikuwa na fununu nadhani hata alijua futa lishaagizwa ndio maana hakuwa na wasiwasi na hoja yake kweli inashangaza futa linashughulikiwa kwa kasi hata watu hawakai ofisini mkulo kasema fedha zipo tayari, chambo KM yuko bandarini anahakikisha lipakuliwa haraka ngeleja anashinda Tegeta, kweli hapa kuna namna tunadanganyika mbona vifaa vya mtambo mpya msishughulikie hivyo(hakuna %)
 
Phuuuu....phuuuuu.......phuu....I smell corruption on here!
I see JK behind the deal...!
 
Tumuulize NGELEJA palepale Tegeta kuna mtambo mpya wa TANESCO utakaotumia gesi ambao utatoa MW 20.Umechelewa kuanza kazi kutokana na vifaa KUCHELEWESHWA BANDARINI.JEE KWA NINI SERIKALI HAIKUCHANGAMKIA KUTOA VIFAA VYA MKANDARASI HUYO KAMA ILIVYOCHANGAMKIA MAFUTA?
Mkuu, ni mtambo wa MW40.
Lakini inashangaza kweli ni kwa nini kufungwa kwa mtambo huo kumechelwa eti kwa sababu vifaa vilichelewa kutoka bandarini, inaonyesha kuwa kweli serikali yetu ni zimamoto
 
Hii serikali nimeanza kuamini imejaa retards,wanatumia 23 bilion kununua mafuta kwa mwezi kutoka kwa mwarabu kuwasha mitambo michafu kwa umeme wa siku mbili huku tumejaza clean natural gas ya kwetu wenyewe ambayo ni cheap na ingetoa ajira kwa watanzania wenzetu na tusingetumia dollars...can you imagine 23 bilion zingeingia kwenye kampuni za ndani uchumi wetu ungekuwa kiasi gani na kuhakikisha ajira za watu wetu na kupata kodi hapo hapo,hivi kwanini inakuwa ngumu sana kwa hii serikali kufanya vitu rahisi kama hivi vyenye faida kwa nchi yetu? ni 10% tuu au kuna mengine? hivi ni kweli serikali imeshindwa kununua generators mbili au moja za 100MW zitakazotumia gas yetu wenyewe? kweli this is heartbreaking!
 
hata kufika rais kutangaza kuhusu kufunguliwa mitambo tayari ilikuwa kila kitu kishaanza taratibu zake (kwa nchi nyengine huwa hivyo), so hapa nampa benefit of doubt mheshimiwa rais kuwa hakuna mchezo mchafu.

cha kujiuliza zaidi ni kwa kuwasha hiyo mitambo tanesco litakula hasara ya kiasi gani? na hiyo hasara italipwa na nani?
 
jamani mafuta yamechukuliwa mombasa na siyo arabui. Hiyo meli ilikuwa babdarini mombasa ikisubiri kupakuliwa na hilo deal lilipo tick basi ikaagizwa tu iondoke mombasa na kuja dsm.
 
Hii serikali nimeanza kuamini imejaa retards,wanatumia 23 bilion kununua mafuta kwa mwezi kutoka kwa mwarabu kuwasha mitambo michafu kwa umeme wa siku mbili huku tumejaza clean natural gas ya kwetu wenyewe ambayo ni cheap na ingetoa ajira kwa watanzania wenzetu na tusingetumia dollars...can you imagine 23 bilion zingeingia kwenye kampuni za ndani uchumi wetu ungekuwa kiasi gani na kuhakikisha ajira za watu wetu na kupata kodi hapo hapo,hivi kwanini inakuwa ngumu sana kwa hii serikali kufanya vitu rahisi kama hivi vyenye faida kwa nchi yetu? ni 10% tuu au kuna mengine? hivi ni kweli serikali imeshindwa kununua generators mbili au moja za 100MW zitakazotumia gas yetu wenyewe? kweli this is heartbreaking!

nakwambia mkuu ukifikiria jinsi serikali ya CCM inavyofanya kazi unaweza kuchanganyikiwa. Gesi asilia tunayo tena ya kwetu, songas wameisha sema wanazalisha 30% ya uwezo wao kwa nini basi wasiruhusiwe wakaongeza uzalishaji hadi 90% ya uwezo wao???

Ukijiuliza unakosa jibu. Hii wizara ya nishati na madini ina nini hasa?? kwa nini mambo hayaendi?? Kuna ile kampuni iliyo na mitambo ya kuzalisha umeme kwa gesi mtwara, ilisha sema kinacho takiwa ni serikali itoe pesa ili ijengwe line ya gridi kutoka makambako/tunduma hadi mtwara ili kampuni ile iongeze uzalishaji wa umeme kwenye gridi ya taifa lakini husikii lolote linaongelewa, kila siku utamsikia ngeleja na ngonjera zake za mazungumzo yanaendelea na IPTL.....kwani lazima IPTL????

Tunahitaji majasusi wa kuanza kuua baadhi ya mawaziri wala rushwa, mbona ukipinga maslahi ya marekani unauawa kwa nini sisi tusitumia njia hiyo kukomesha watawala wala rushwa??? kwa sababu usitegemee mtu kama makamba kihiyo afanye mabadiliko wakakti kula yake inategemea umbea na uwongo na rushwa.
 
mimi nikiwaambia hapa kuwa Kikwete na Zitto lao moja mnaanza ohh mwafrika unachuki binafsi na Zitto------

Haya sasa! tarrrrrtibu Zitto na Kikwete wanajianika wazi kuwa wote ni ... ni ... ni ...

mimi hapa mwalimu.... okay ... mwafrika toa jibu ...

wote ni mhhhh ....mhhhh... mhhhhh ....ma... ma ... ma me mi mo mu ... ma .... maphithadi
 
Mr. Nguvumali,

Kwakweli hapo nami nilichanganyikiwa its not possible at all labda iyo mipango ilipangwa tokea mwanzo wa sakata zima la Umeme toka kipindi cha Richmond si jui Dowans kuna kitu kinapikika hapo

Nataka kuuliza Nini Maana ya Ikulu?

Utendaji wake wa kazi na wajibu wake ni upi?

Je Ikulu walikuwa wakijua hili swala zima la mkanganyiko wa umeme?? Kwani ni jambo la kustahajabisha ndani ya muda huo wa sio chini ya siku 6, Meli ya mafuta ilisha tinga bandarini??

Twahitaji Ikulu Itupe majibu ya kimsingi na yanayo eleweka iweje tamko litoke Ikulu na mafuta yafike mapema? kama sio kulikuwa na kamati ndogo ndogo za siri zilikaaaa mapema na hata kabla ya mgao kuanza walipanga mikakati na tena hiii ni ya siri mno ya wezekana hata waziri ngereja he was aware of the Matter kabisa iweje ilo agizo limetekelezwa mapema kiasi hicho na kushindwa kuakatisha mkataba wa Richmond au kuwafukuza ndani ya nchi yetu?? na kuwaaacha wabunge wakirushiana maneno.

Hapa viongozi wetu wanatupotezea muda wetu kwanza wa ku watch TV, Kuwasikiliza majuukwaani kwenye lingo za siasa, Radioni, pia nayo magazeti yanauza na kutufirisi pesa zetu na kuwa maskini

The Government is totaly confusing us jamani, Viongozi hawaoni aibu ati

Mimi kwa kupitia angalau kidogo kwenye mjadala huu, naona kama ufanisi wa aina hii ungekuwa Tanzania hii basi Tanzania ingekuwa mojawapo ya nchi tajirii saana na zenye maendeleo makubwa sana katika Dunia hii. Hata tusingekuwa tumeingia gizani at the first place! Tungekuwa hata na vinu vya kufulia umeme wa nishati ya nyuklia.
 
nadhani mheshimiwa Rais atajibu soon, hawezi kuwaachia muanze mapema hivi ku-speculate kwamba eti wanatafuta hela za kampeni...and by the way, hivi Kikwete anavyopendwa, mnadhani kuna ulazima wa pesa mwakani??? kama mnabisha, angalieni data za REDET....
 
Mdau, hizi unazoziita "speculations", hazitoki hewani tu. Historia inaonyesha uwezekano huu upo. kuna msemo "ukinidanganya mara ya kwanza wewe utakuwa mjanja, ukinidanganya mara ya pili, mimi nitakuwa ****".
Watu hawataki kuwa mafala tena, ndiyo maana wanahoji.
 
mimi nikiwaambia hapa kuwa Kikwete na Zitto lao moja mnaanza ohh mwafrika unachuki binafsi na Zitto------

Haya sasa! tarrrrrtibu Zitto na Kikwete wanajianika wazi kuwa wote ni ... ni ... ni ...

mimi hapa mwalimu.... okay ... mwafrika toa jibu ...

wote ni mhhhh ....mhhhh... mhhhhh ....ma... ma ... ma me mi mo mu ... ma .... maphithadi
 
kuna mambo mengi yanayofanywa na serikali yanatisha sana na huwa najiuliza mara mbili mbili je ni watanzania wangapi wamejiandaa kukabiliana na hali mbaya ya maisha itayokuja kujitokeza mbeleni? au tunajiandaa vipi kuwaepusha watoto wetu kama hali hii haitotukuta tukiwa hai ? hizi hesabu za fedha zinazo fujwa kama ni za kweli basi hii nchi inaelekea pabaya na kwenye giza kubwa na sijaona muokozi wowote mpaka sasa hivi ambaye yuko serious au yuko tayari kuwa shujaa wa wa tanzania.haiwezekani kila kosa lisiwe na muhusika aliyetenda hilo kosa.
viongozi wa upinzani wanatakiwa wafanye mambo kwa vitendo na ndio wananchi nao watawaunga mkono zaidi lakini wataendelea kuwakenulia meno basi nchi itaendelea kuongozwa kifalme.
 
Mwenzenu ninatatizwa na jambo moja nalo nihili la Umeme na maswala ya Dowans....

Nikifikiri kwa makini na kwakina natatizika, kweli hakuna mkono wa namna namna katika hili swala la kukatika umeme TANZANIA na hujuma ?

Hebu fikiri Rais JK Kikwete (Mheshimiwa) alitoa tangazo kua mitambo ya IPTL iwashwe, kisha tukaambiwa na kina Mh. Ngeleja kuwa Serikali imeagiza mafuta ya kutumia kwenye mitambo ya IPTL ARABUNI, Baada ya siku chini ya sita, tukataarifiwa kuwa mafuta yameletwa na merikebu ya mizigo...na yamefika bandari ya Dar es salaam yakisubiri kupakuliwa ili mitambo hiyo iwashwe...

Sasa najiuliza meli toka Arabuni huchukua siku ngapi ? Au mafuta yaliagizwa kabla ya ikulu kuzungumza? Bado najiuliza au tuliishapata dili la IPTL tulichokuwa tunasubiri ni mitambo izimwe nchi iwe kizani ?

Mimi naogopa hapa, na Hisia kua kunakitu nyuma ya sakata zima la umeme Tanzania inanijia...

Ni mawazo yangu.

Nguvumali umeniibulia mambo ambayo sikuwa na yafikria kwa sasa,kiufupi na likely ndiyo hivyo JK alilihalisha dili hili muda mrefu sana na mafuta yaka nunuliwa huko Uarabuni labda mwezi wa 6 hivi,na wakati Meli inakaribia kufika ukanda wa Afrika Mashariki ndipo mitambo ya Dr Rashid ikazimwa ili kuwaonyesha watz umuhimu wa umeme!

Again,thx u alot Nguvumali kuibua hoja hii na kwa kweli hii ni scandal mpya ktk uongozi legelege wa JK! Yaani asema wiki iliyopita kama IPTL itawasha umeme wake na mara hii mafuta yanunuliwe then yawe yamefika bandarini TZ?shame on you JK!!
 
Inaelekea Zitto aliujua huu mchezo mapema na katika jitihada za pre-emption akashauri serikali itumie mitambo ya Dowans, kama serikali ingekubali bila shaka EL na RA wangefaidika na hivyo kuzidi kuipa nguvu kambi ya mafisadi na kuchochea mgawanyiko zaidi kwa chama chetu na pengine kuwanufaisha wapinzani japo indirectly.

nadhani muungwana akashtukia hiyo na kuamua kutumia IPTL kwa kuwa pengine hana hakika kama EL na RA watamuunga mkono financilally come yr 2010. having said that, inawezekana hii ni dili ya muungwana kutengeneza pesa kwa ajili ya uchaguzi come yr 2010...who knows...si wanasema siasa ni mchezo mchafu...pengine huu ndio katika huo uchafu...

maoni yangu tu...

Na wewe bure kabisa unasema eti chama chetu???? wewe na nani makamba au??? Chama limeoza alafu unasema ???
 
Procedure mzima ya clearing and forwarding inakataa kwa ili deal. Oil tanker inaelekea ilishakuja kitambo na kunyuti Mombasa au bahari kuu na kusubiri amri ya kuingia Dar port.

Wakisema wameagiza from Mombasa bado procedure zinakataa, order ilitoka lini, meli ilianza kupakia lini? na kutia timu Dar ndani ya siku 6? Inashusha Dar tani 8,800 kwa 30 hrs (source Dailynews Oct 26), walipakia kwa masaa mangapi?...hapa kuna tatizo. Normal cargo ship tena ya dharura inachukua 7-14 days from UAE to East Africa

May be watasema siku hizi meli zinapakia kabisa cargo na kusubiri customer? Thanks Nguvumali kwa kuliona ilo.
 
Nguvumali umeniibulia mambo ambayo sikuwa na yafikria kwa sasa,kiufupi na likely ndiyo hivyo JK alilihalisha dili hili muda mrefu sana na mafuta yaka nunuliwa huko Uarabuni labda mwezi wa 6 hivi,na wakati Meli inakaribia kufika ukanda wa Afrika Mashariki ndipo mitambo ya Dr Rashid ikazimwa ili kuwaonyesha watz umuhimu wa umeme!

Again,thx u alot Nguvumali kuibua hoja hii na kwa kweli hii ni scandal mpya ktk uongozi legelege wa JK! Yaani asema wiki iliyopita kama IPTL itawasha umeme wake na mara hii mafuta yanunuliwe then yawe yamefika bandarini TZ?shame on you JK!!

CCM haina pesa kwa ajili ya kampeni za 2010. Kama mtakumbuka chaguzi zao za vijana na UWT ziliahirishwa kutokana na ukosefu wa pesa na uchaguzi ujao mafisadi wote sidhani kama watatoa hata senti moja ili kugharamia kampenzi za CCM. Sasa ndiyo likachezwa deal bab kubwa ili wajipatie mabilioni ya kampeni hizo. Bahati mbaya ndugu yetu Nguvumali kalishtukia deal. Sasa inabidi watueleze ukweli wa mambo kuhusiana na haya mafuta.
 
Back
Top Bottom