Mafuta ya IPTL yamenunuliwa wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mafuta ya IPTL yamenunuliwa wapi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nguvumali, Oct 27, 2009.

 1. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #1
  Oct 27, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Mwenzenu ninatatizwa na jambo moja nalo nihili la Umeme na maswala ya Dowans....

  Nikifikiri kwa makini na kwakina natatizika, kweli hakuna mkono wa namna namna katika hili swala la kukatika umeme TANZANIA na hujuma ?

  Hebu fikiri Rais JK Kikwete (Mheshimiwa) alitoa tangazo kua mitambo ya IPTL iwashwe, kisha tukaambiwa na kina Mh. Ngeleja kuwa Serikali imeagiza mafuta ya kutumia kwenye mitambo ya IPTL ARABUNI, Baada ya siku chini ya sita, tukataarifiwa kuwa mafuta yameletwa na merikebu ya mizigo...na yamefika bandari ya Dar es salaam yakisubiri kupakuliwa ili mitambo hiyo iwashwe...

  Sasa najiuliza meli toka Arabuni huchukua siku ngapi ? Au mafuta yaliagizwa kabla ya ikulu kuzungumza? Bado najiuliza au tuliishapata dili la IPTL tulichokuwa tunasubiri ni mitambo izimwe nchi iwe kizani ?

  Mimi naogopa hapa, na Hisia kua kunakitu nyuma ya sakata zima la umeme Tanzania inanijia...


  Ni mawazo yangu.
   
 2. P

  Papa Sam Senior Member

  #2
  Oct 27, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  umefikiri kwa kina mkuu, lakini kweli inaacha maswali, kweli inawezekanaje meli itoke Arabuni ndani ya siku tatu ikawa imetia nanga Dar.
   
 3. M

  Mvutakamba Member

  #3
  Oct 27, 2009
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  It was a politicak move wakiwa hawajakaa yema ikawa pre empted na wajuvi sasa hawana la kufanya . Fuatilia nyuma ya tender ya mafuta hiyo utajua kiasi halisi cha gharama na Tanzania imelipa kiasi gani . They mapensa ya uchaguzi bwana weeeeeeeee
   
 4. D

  Dawson Member

  #4
  Oct 27, 2009
  Joined: Mar 6, 2009
  Messages: 43
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tulichokua tunasubiri ni mitambo izimwe nchi iwe kizani ? Nguvumali nchi hii kila kitu kinafanywa kwa zima moto unakumbuka issue ya mabasi kupata ajali za kufululiza tamko likatolewa magari yenye chassis cha malori yatolewe barabarani, as if walikuwa hawajui kuwepo kwa haya magari b4 " ewe Tanzania mambo haya yangeipata Sodoma ingelitubu ole wako wewe"
   
 5. P

  Papa Sam Senior Member

  #5
  Oct 27, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwakweli sielewi , hebu fikiri mwenyewe siasa inavyogharimu maendeleo ya nnchi hii, kweli jiulize ile meli ilikua Mombasa au bandari za hapo Msumbiji ? kweli unaweza kutoa order leo ya mamia ya tonne ya mafuta Arabuni kisha baada ya siku tano ngoma iko Dar port. inatia shaka
   
 6. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #6
  Oct 27, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
 7. M

  Mwanjelwa JF-Expert Member

  #7
  Oct 27, 2009
  Joined: Jul 29, 2007
  Messages: 961
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Ya. Hapo kuna maswali kibao bila majibu.
   
 8. M

  Mwanjelwa JF-Expert Member

  #8
  Oct 27, 2009
  Joined: Jul 29, 2007
  Messages: 961
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Hii kwa kweli inaacha maswali kibao bila majibu
   
 9. Che Guevara

  Che Guevara JF-Expert Member

  #9
  Oct 27, 2009
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 1,178
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  Mhh hii ni kali. Kuna kitu hapa.

  Tar 21/10/2009 Kikwete alitoa agizo kuwa mitambo ya IPTL iwashwe.

  Tar 25/10/2009 tayari meli yenye shehena ya mafuta imewasili Dar kwa ajili ya kutumika kwenye mitambo ya IPTL.


  Swali:
  Mafuta yaliagizwa lini hadi yawe yameshawasili Dar tarehe 25/10/2009?
   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  Oct 27, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,533
  Likes Received: 81,947
  Trophy Points: 280
  Mkuu Nguvumali, swali lako ni zuri sana hata mimi hili nililitafakari kwamba inakuwaje hata siku 10 hazijapita tangu Kikwete aiamrishe IPTL kuwasha mtambo wake tunaambiwa mafuta yaliyoagizwa na Serikali yameshaingia nchini. Hapa naona kuna neno na si ajabu kuna ufisadi wa hali ya juu. Maana hili tatizo la umeme nchini linatumiwa na wengi sasa kujitajirisha kwa kuifisadi nchi yetu. Si ajabu mafuta hayo itadaiwa yamenunuliwa kwa bei mbaya na pia kuna uwezekano yalikuwepo nchini siku nyingi sasa wameamua kutumwagia changa la macho ili kuonyesha kama yameagizwa toka nje.
   
 11. P

  Papa Sam Senior Member

  #11
  Oct 27, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  KWAKWELI TANZANIA ni nchi yenye wanasiasa wa ajabu, kwakweli mimi naamini kuna hujuma katika swala zima la umeme, na hii inaanzia kwenye skendo la Richmond, dada yake Dowans, blahblah za kutaka kununua mitumba ya dada Dowans.
   
 12. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #12
  Oct 27, 2009
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Mr. Nguvumali,

  Kwakweli hapo nami nilichanganyikiwa its not possible at all labda iyo mipango ilipangwa tokea mwanzo wa sakata zima la Umeme toka kipindi cha Richmond si jui Dowans kuna kitu kinapikika hapo

  Nataka kuuliza Nini Maana ya Ikulu?

  Utendaji wake wa kazi na wajibu wake ni upi?

  Je Ikulu walikuwa wakijua hili swala zima la mkanganyiko wa umeme?? Kwani ni jambo la kustahajabisha ndani ya muda huo wa sio chini ya siku 6, Meli ya mafuta ilisha tinga bandarini??

  Twahitaji Ikulu Itupe majibu ya kimsingi na yanayo eleweka iweje tamko litoke Ikulu na mafuta yafike mapema? kama sio kulikuwa na kamati ndogo ndogo za siri zilikaaaa mapema na hata kabla ya mgao kuanza walipanga mikakati na tena hiii ni ya siri mno ya wezekana hata waziri ngereja he was aware of the Matter kabisa iweje ilo agizo limetekelezwa mapema kiasi hicho na kushindwa kuakatisha mkataba wa Richmond au kuwafukuza ndani ya nchi yetu?? na kuwaaacha wabunge wakirushiana maneno.

  Hapa viongozi wetu wanatupotezea muda wetu kwanza wa ku watch TV, Kuwasikiliza majuukwaani kwenye lingo za siasa, Radioni, pia nayo magazeti yanauza na kutufirisi pesa zetu na kuwa maskini

  The Government is totaly confusing us jamani, Viongozi hawaoni aibu ati
   
 13. N

  Nanu JF-Expert Member

  #13
  Oct 27, 2009
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hata mimi nashangaa. Meli hii imekuja imebeba shehena ya HFO (mitambo ya IPTL) na diesel. Hivyo shehena ilishaagizwa muda mrefu tu.
   
 14. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #14
  Oct 27, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  unaona sasa, habari kua ilikua imebeba na mitambo ya IPTL, kama ni kweli inaongeza wigo wa mashaka na hofu, hivi watawala wetu wanataka kutuambia nini ? kipo kitu hapa..
   
 15. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #15
  Oct 27, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Labda ingechukua miezi sita kufika hapo bongo ingependeza zaidi
   
 16. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #16
  Oct 27, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,533
  Likes Received: 81,947
  Trophy Points: 280
  Hapana Mkuu Kibs haya maswali lazima yaulizwe maana nchi yetu ufisadi umekithiri mno! Unakumbuka ni Watanzania wa US walioanza kufuatilia kuhusu Richmond kudai ni kampuni ambayo ina HQ Houston. Baada ya kugundua kwamba hili si kweli ndiyo kidogo kidogo uwongo wa RA na Richmond yake ukaanza kudhihirika. Hapa kuna neno Mkuu.
   
 17. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #17
  Oct 27, 2009
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  muanzisha mada hii kama vile alikuwepo akilini kwangu, yani ameandika exactly tulichokua tunaongea leo asubuhi may be ni mtu wangu wa karibu huyu, na kama siyo basi mawazo yake na yangu na ya yule tuyekuwa tunaogea naye asubuhi are exactly the same. hapa kuna mchezo mchafu hata mtoto mdogo anaweza kuyelewa. wizi mtupu.
   
 18. Freddy81

  Freddy81 Member

  #18
  Oct 27, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kwani kutoka Huko Uarabuni hadi DSM ni umbali gani? au meli huwa inachukua muda gani hadi kufika huku ikitokea uarabuni, Msidhani meli ni baiskeli jamani, siku hizi technolojia imekua si kama zamani waarbu walikuja kwa mashua mkadhani hali ni ileile.
  Ulizeni hizo fedha za kununua hayo mafuta zimetoka wapi na misingi ipi. Suala la Meli kuwahi ni nafuu kwetu. ingechukua mwezi kuja hapa ingekuwa kero.
  Halafu serikali imeagiza mafuta kupitia kampuni ya Total Tanzania wao wanajua hiyo meli walipoitoa
   
 19. P

  Papa Sam Senior Member

  #19
  Oct 27, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hii ni aina nyingine ya akili za mtu mwenye ukakasi wa mawazo, kuhoji namna serikali yako inavyotenda ni haki yako ya kikatiba mtanzania mwenzangu, katika mazingira ya dharula kama hivi , NDIO Richmond ilizaliwa, katika mazingira kama haya , tulisign mkataba kituko wa IPTL, DHARULA hizi wajanja hutumia katika kujineemesha ....
  Akili yako lazima iwaze hatua moja kwenda mbele, usiamini kila uambiwacho na hasa hawa wanasiasa uchwara, na wezi wa mali ya umma.
   
 20. P

  Papa Sam Senior Member

  #20
  Oct 27, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  eti mafuta siku tatu, kwani hiyo ni chumvi dukani au chupi zimening'inizwa pale manzese. Au gazeti barabarani thubutu.
   
Loading...