Labda ingechukua miezi sita kufika hapo bongo ingependeza zaidi
Mwenzenu ninatatizwa na jambo moja nalo nihili la Umeme na maswala ya Dowans....
Mimi naogopa hapa, na Hisia kua kunakitu nyuma ya sakata zima la umeme Tanzania inanijia...
Ni mawazo yangu.
Kuna uwezekano wa kuwepo na neno, hata hivyo aina nyingine ya udadisi inatia shaka....Hapana Mkuu Kibs haya maswali lazima yaulizwe maana nchi yetu ufisadi umekithiri mno! Unakumbuka ni Watanzania wa US walioanza kufuatilia kuhusu Richmond kudai ni kampuni ambayo ina HQ Houston. Baada ya kugundua kwamba hili si kweli ndiyo kidogo kidogo uwongo wa RA na Richmond yake ukaanza kudhihirika. Hapa kuna neno Mkuu.
Ta'adabuhii ni aina nyingine ya akili za mtu mwenye ukakasi wa mawazo, kuhoji namna serikali yako inavyotenda ni haki yako ya kikatiba mtanzania mwenzangu, katika mazingira ya dharula kama hivi , NDIO Richmond ilizaliwa, katika mazingira kama haya , tulisign mkataba kituko wa IPTL, DHARULA hizi wajanja hutumia katika kujineemesha ....
Akili yako lazima iwaze hatua moja kwenda mbele, usiamini kila uambiwacho na hasa hawa wanasiasa uchwara, na wezi wa mali ya umma.
Mkuu, inabidi tuelewe kuwa suala hili halikuanza kushughulikiwa siku ambayo agiza la Kikwete liliskika publicly. Mpaka siku il nchi ilikuwa kwenye mgawo kama wiki mbili hivi na wahusika walikuwa wameshaanza kulishughulikia suala hilo hata kabla mgawo haujaanza. Agizo la Kikwete kwa akina Ngeleja lilitolewa siku ambapo walipeleka taarifa Ikulu kuwa kutakuwa na mgawo wa umeme, na hili lilifanyika hata kabla mgawo haujaanza. Hivyo suala hili lilianza kushughulikiwa zamani isipokuwa tu haiukuelezwa hadharani ni nini kilikuwa kinafanyika.Mkuu Nguvumali, swali lako ni zuri sana hata mimi hili nililitafakari kwamba inakuwaje hata siku 10 hazijapita tangu Kikwete aiamrishe IPTL kuwasha mtambo wake tunaambiwa mafuta yaliyoagizwa na Serikali yameshaingia nchini. Hapa naona kuna neno na si ajabu kuna ufisadi wa hali ya juu. Maana hili tatizo la umeme nchini linatumiwa na wengi sasa kujitajirisha kwa kuifisadi nchi yetu. Si ajabu mafuta hayo itadaiwa yamenunuliwa kwa bei mbaya na pia kuna uwezekano yalikuwepo nchini siku nyingi sasa wameamua kutumwagia changa la macho ili kuonyesha kama yameagizwa toka nje.
Hata hakieleweki ndugu yangu,Kila mara namwona ngeleja kwenye Tv akitangaza tarehe tofauti tofauti za kuisha mgawo.Mara aseme mwisho wa Novemba tunatesti mashine, mara kesho,mara mwisho wa mwezi huu.Kuna uwezekano wa kuwepo na neno, hata hivyo aina nyingine ya udadisi inatia shaka....
Anyway tuendelee kukata ishu, Vipi huo mgao umeshakwisha? manake huku Zenj haukufika!
.
Kwenye hili suala la meli kuwahi sio ajabu. Mambo kadhaa yanaweza kuwa yamefanyika mafuta haya yakawahi. Kwanza, International trade ya bulk cargo (mafuta ya magari, mafuta ya kutengeneza sabuni na kula, sukari, ngano, mkaa wa mawe na kadhalika), wauzaji wanaweza kupakia mzigo bila mnunuzi kufahamika. Meli huamua kuelekea ukanda fulani kulingana na mahitaji. Mara nyingi meli hupakia mafuta na kuja ukanda wa pwani ya Afrika Mashariki, zikakaa hapo kusuburi order. Mnunuzi akipatikana tu, mzigo unakuwa karibu. Ngano inaweza kupakiwa kutoka Canada na kuja ukanda wa Africa mashariki kusubiri Order, Azam wakinunua tu ngano inakuwa karibu kabisa na eneo linalohusika. Haya mafuta ni hayatumiki IPTL pekee, inawezekana yalikwa yanapelekwa sehemu nyingine lakini kutokana na umuhimu TOTAL wakaamua walete kiasi Tanzania baada ya kupewa order na umuhimu wake. Tujue kuwa meli hiyo inabeba mafuta mengi zaidi ya hayo.
Pili, ni speculation za kibishara. Kuwa walitonywa tangu siku ya kwanza ya mgao wa umeme kuwa IPTL itawashwa hivyo wakasogeza mzigo karibu.
hii ina shangaza sana tufanyaje juu ya watu hawa maana kuna ukweli ndani yake Mungu asikie kilio chetu kama alivyo sikia cha wana wa israeli atutumie Musa wa sasa tutoke utumwani laana ilisha sasa inakuwajeMhh hii ni kali. Kuna kitu hapa.
Tar 21/10/2009 Kikwete alitoa agizo kuwa mitambo ya IPTL iwashwe.
Tar 25/10/2009 tayari meli yenye shehena ya mafuta imewasili Dar kwa ajili ya kutumika kwenye mitambo ya IPTL.
Swali:
Mafuta yaliagizwa lini hadi yawe yameshawasili Dar tarehe 25/10/2009?
Mwenzenu ninatatizwa na jambo moja nalo nihili la Umeme na maswala ya Dowans....
Nikifikiri kwa makini na kwakina natatizika, kweli hakuna mkono wa namna namna katika hili swala la kukatika umeme TANZANIA na hujuma ?
Hebu fikiri Rais JK Kikwete (Mheshimiwa) alitoa tangazo kua mitambo ya IPTL iwashwe, kisha tukaambiwa na kina Mh. Ngeleja kuwa Serikali imeagiza mafuta ya kutumia kwenye mitambo ya IPTL ARABUNI, Baada ya siku chini ya sita, tukataarifiwa kuwa mafuta yameletwa na merikebu ya mizigo...na yamefika bandari ya Dar es salaam yakisubiri kupakuliwa ili mitambo hiyo iwashwe...
Sasa najiuliza meli toka Arabuni huchukua siku ngapi ? Au mafuta yaliagizwa kabla ya ikulu kuzungumza? Bado najiuliza au tuliishapata dili la IPTL tulichokuwa tunasubiri ni mitambo izimwe nchi iwe kizani ?
Mimi naogopa hapa, na Hisia kua kunakitu nyuma ya sakata zima la umeme Tanzania inanijia...
Ni mawazo yangu.
Kwani kutoka Huko Uarabuni hadi DSM ni umbali gani? au meli huwa inachukua muda gani hadi kufika huku ikitokea uarabuni, Msidhani meli ni baiskeli jamani, siku hizi technolojia imekua si kama zamani waarbu walikuja kwa mashua mkadhani hali ni ileile.
Ulizeni hizo fedha za kununua hayo mafuta zimetoka wapi na misingi ipi. Suala la Meli kuwahi ni nafuu kwetu. ingechukua mwezi kuja hapa ingekuwa kero.
Halafu serikali imeagiza mafuta kupitia kampuni ya Total Tanzania wao wanajua hiyo meli walipoitoa
Nafikiri wakati hili linaendelea kujadiliwa( yaani hili la kasi ya ajabu katika uwajibikaji wa serikali ya awamu hii), hebu tuwatafute hawa wafuatao na ku-connect the dots:-
Wamiliki na wanahisa wa IPTL ni wakina nani?
Watu wa serikali walioipigia pande IPTL mpaka wakafanikiwa ni kina nani?
Wakati IPTL inapikwa nani walikuwa; Waziri wa Nishati na Madini
Naibu waziri-Nishati na madini,
Katibu Mkuu- Nishati na madini.
Waziri wa fedha
Katibu mkuu-Hazina na
Mwanasheria mkuu?
Leo hao wahusika wako wapi? Ikiwa kipindi hicho walipewa chochote kitu na IPTL leo watashindwaje kutengeneza mgogoro utakao wapa kula nyingine tena?