The redemeer
JF-Expert Member
- Jan 28, 2025
- 4,780
- 8,155
Katika ulimwengu wa kiroho, watu wengi hujikuta wakivutiwa na matumizi ya mafusho (udi, ubani karafuu mdalasini na aina mbali mbali za mafusho kulingana na nyota yako), vito , na vitakasa mbalimbali vya kiroho kama maji ya kutakasa, chumvi, n.k.
Hivi vyote vina nafasi yake. Ni kama mafuta kwenye injini ya gari – vinasaidia kupunguza msuguano, kuondoa uzito wa nishati chafu, na kuleta urahisi wa mzunguko wa nguvu. Lakini ni lazima tukubali jambo moja la msingi:
Hivi siyo tiba. Ni vilainishi tu.
Ni msaada tu wa mchakato, si suluhisho la mwisho wa matatizo ya maisha. Havitatatua changamoto zako moja kwa moja. Havitaleta pesa au utulivu kama ndani yako bado kuna misukosuko, giza, hofu, na nia zisizo safi.
Tiba ya kweli huanza unapobadilika kutoka ndani kwenda nje – si kinyume chake.
Watu wengi wameishia kujuta na kulaumu:
“Natumia mafusho lakini sioni mabadiliko,” “Navaa vito lakini bado natatizika,” “Nimefanyiwa spiritual cleansing mara kadhaa lakini maisha yangu hayaendi.”
Na kisha husema:
“Wataalamu hawa wa mambo ya kiroho ni waongo.”
Lakini ukweli ni huu: Tatizo si wataalamu. Tatizo huanzia kwako.
Unapopewa vitakasa, elewa maana yake. Ni kama sabuni. Sabuni haiwezi kubadilisha ubora wa nguo, bali kazi yake ni kufua na kuondoa vumbi. Ubora wa nguo upo kwenye material yaliyotumika kuitengeneza.
Vivyo hivyo, maisha yako hayawezi kubadilika kwa nje tu. Lazima utakase ndani yako kwanza. Nia yako. Imani yako. Mawazo yako. Mielekeo yako.
Msingi ni huu: Takasa ndani yako – ndipo utakapoona nguvu ya kweli ya vifaa vya kiroho.
Kama hujatakasa nia, hisia, na historia yako ya ndani, hakuna mafusho, hakuna kioo, wala chumvi itakayoweza kubadilisha maisha yako. Unahitaji kurudi kwenye chimbuko lako – kwenye mizizi ya nafsi yako.
Wengine wenu mnateseka si kwa sababu ya maisha yenu ya sasa, bali kwa sababu ya laana za ukoo, madeni ya mababu, na vizuizi vilivyorithiwa kizazi kwa kizazi. Huwezi kuziponya haya kwa mafusho tu.
Ni lazima uzikate. Ni lazima uzikomboe.
Kwa wanaojifunza unajimu wa kiroho (spiritual astrology), hili linaonekana wazi kwenye nyumba ya 4 katika ramani ya kuzaliwa (natal chart). Hapo ndipo siri za ukoo, mizizi, na mizigo ya kurithi hujificha. Usiporudi hapo, unaweza kujaribu kila njia ya nje – lakini ndani bado unafungwa.
Tiba ya kweli ni mabadiliko ya ndani. Ni uamsho wa nafsi yako. Ni kujua kuwa hakuna msaada wa nje utakaoleta mabadiliko ya kweli kama ndani yako kuna uharibifu. Mafusho yatafanya kazi – kama moyo wako uko tayari. Vito vitang’aa – kama roho yako imeamka. Vitakasa vitasaidia – kama tayari umeamua kuishi kwa ukweli.
Je, uko tayari kutakasa nia yako Kuachilia yaliyopita Kukata minyororo ya ukoo? Kufufuka kutoka ndani? Hapo ndipo mafusho yako, vito vyako, na maji yako ya kutakasa yatageuka kuwa daraja la kweli,
ASANTENI.SANA KARIBU TUJIFUNZE HEKIMA.NA MAARIFA