Mafuriko Malawi yaua watu 28

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,382
2,000
Idadi ya watu waliokufa kutokana na mvua kubwa zilizosababisha mafuriko Kusini mwa Malawi imefikia watu 28.
Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi hiyo iliyotolewa Jumamosi imesema kuwa wakati huohuo idadi ya walioathirika inakadiriwa kuongezeka mara dufu.
Msemaji wa Wizara hiyo anayehusika na udhibiti wa maafa Chipiliro Khamula, amesema watu 124 wamejeruhiwa huku takribani wengine zaidi ya 200,000 wamelazimika kuhama makazi yao katika jumla ya wilaya 14.
Wakati huohuo Rais wa Malawi, Arthur Peter Mutharika ametangaza tukio hilo kuwajanga la kitaifa baada ya dhoruba kali kusababisha kuta za mito kubomoka na mafuriko kufunika vijiji hivyo.
Katika maeneo hayo umeme umekatika na huduma ya maji inakosekana.
Rais Mutharika ameelekeza misaada ya dharura kuelekezwa katika maeneo hayo yaliyoathirika kuratibiwa kwa haraka ikiwemo na kulitaka Jeshi la Malawi kusaidia katika zoezi la uokozi.
Dhoruba kama hiyo pia imesababisha mafuriko katika baadhi ya mikoa nchini Msumbiji.

Voa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom